Mkongo wa Taifa ulivyoongeza, kurahisisha mawasiliano nchini


Mkongo wa Taifa ulivyoongeza, kurahisisha mawasiliano nchini

Mpaka mwaka 2001, matumizi ya simu za mkononi yaliyazidi yale ya simu za mezani. Takwimu zinaonyesha hadi Juni mwaka huu kulikuwa na watumiaji milioni 43.7 wa simu, wateja milioni 23.1 wa intaneti, wengi wao wakitumia simu za kisasa.

Mpaka mwaka 1995, simu za mezani zilikuwa zinatumika kwa wingi zaidi. Wakati huo, asilimia 97.6 ya mawasiliano ya simu nchini, yalikuwa yanafanywa kwa simu hizo zilizokuwa zinamilikiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) huku simu za mkononi zikiwa ni asilimia 2.4 tu.

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha mwaka huo, watumiaji wa simu walikuwa 90,198 lakini mabadiliko ya teknolojia yamesababisha ongezeko la matumizi ya simu za mkononi.

Mpaka mwaka 2001, matumizi ya simu za mkononi yaliyazidi yale ya simu za mezani. Takwimu zinaonyesha hadi Juni mwaka huu kulikuwa na watumiaji milioni 43.7 wa simu wateja milioni 23.1 wa intaneti, wengi wao wakitumia simu za kisasa.

Ongezeko hilo limetokana na maboresho ya miundombinu ya mawasiliano yaliyofanywa kwa awamu tatu kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania ile ya watu wa China kupitia kampuni ya mawasiliano ya China International Telecommunication and Construction Corporation (CITCC) Tanzania.Suala hili linatokana na maboresho ya miundom-binu yanayofanywa na Wizara ya Mawasiliano kwenye mkongo wa mawasiliano wa Taifa (NICTBB).

Akielezea mafanikio yaliyopo, meneja wa miundombinu ya NICTBB, Adin Mgendi amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia, mkongo umeenezwa karibu nchi nzima kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote.

“Nyaya za mwasiliano zimefikisha huduma maeneo mengi nchini na kuwaunganisha Watanzania wengi hata wa vijijini kwenye intaneti, huduma za fedha, redio na runinga,” amesema.

Kwa upande wake, mkuru-gezi mtendaji wa kampuni CITCC, Haijun Jiang amesema Serikali ya China na Serikali ya Tanzania zinatambua umuhimu wa kurahisisha mawasiliano na kutumia teknolojia mpya kuwanufaisha Watanzania.

Kukamilika kwa awamu ya kwanza na ya pili ya mkongo wa mawasiliano, Jiang amesema kumeshuhudia Tanzania ikiwa kitovu cha mawasiliano ukanda wa Afrika mashariki.

Jambo hilo limeongeza upatikanaji wa mawasilano, kupungua kwa gharama za mawasiliano na faida kubwa kwa Serikali na kampuni za mawasiliano. Kadri mkongo huo unavyoendelea kutumika, gharama za kupiga simu kwa mfano, zinazidi kupungua hivyo kumpa unafuu mteja wa kati idadi ya watumiajiikiongezeka jambo linalokuza mapato ya kampuni za simu.

Takwimu za TCRA zinaonyesha ilikuwa inagharimu kati ya Sh199 na Sh305 kupiga simu kwa dakika moja ndani ya mtandao Disemba 2009 lakini ilishuka mpaka kati ya Sh30 na Sh105 Machi 2013.

Kupiga mitandao mingine kwani gharama zake zilipungua mpaka kati ya Sh150 na Sh230 ukilinganisha na kati ya Sh337 na Sh410 kwa dakika moja ndani ya kipindi hicho huku idadi ya watumiaji ikiongezeka kutoka milioni 17.6 mwaka 2009 hadi milioni 27.6 mwaka 2013.

Mabadiliko hayo yalongeza mchango wa huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwenye pato la Taifa kwa zaidi ya asilimia 2.1 mwaka 2016 na kutoa zaidi ya ajira 8,500 kwa wazawa.

Ujenzi huo pia uliongeza idadi ya watumiaji wa simu za mkononi hadi milioni 42 mwaka 2018 huku wa intaneti wakifika milioni 23.1 kutoka milioni tano walio-kuwapo mwaka 2005.

Mhandisi wa mawasiliano wa CITCC, Mo Chen anas-ema uwiano wa watumiaji wa simu nchini ni mkubwa na unalingana na wa nchi nyingi zilizoendelea.“Tanzania ndio nchi pekee Afrika ambayo Serikali yake inamiliki miundombinu mipya na ya kisasa ya mawasiliano,” amesema.

Kutokana na uwapo wa miundombinu ya uhakika na soko kubwa la mawasiliano, Tanzania inazivutia kampuni nyingi na mpaka sasa zipo saba zinazowaunganisha Watanzania na wageni wanaoingia nchini kwa kupiga simu za kawaida, huduma za fedha au intaneti.

Kati ya hizo, Vodacom ndiyo inayoongoza kwa wateja wengi ikiwa nao milioni 14.3 ikifuatiwa na Tigo yenye milioni 11.6 na Airtel milioni 11.5. Kampuni nyingine zilizopo nchini ni Halotel, TTCL, Smile na Zantel.