Ijue ofisi ya NHIF Zanzibar na huduma za uhakika inazotoa kwa wanachama


Ijue ofisi ya NHIF Zanzibar na huduma za uhakika inazotoa kwa wanachama

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa kuwa na wigo mpana wa ofisi nchini kwa lengo la kuwa karibu na wanachama na kuwapa huduma zilizo bora.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa kuwa na wigo mpana wa ofisi nchini kwa lengo la kuwa karibu na wanachama na kuwapa huduma zilizo bora.

Pamoja na kuwa na ofisi kila Mkoa, NHIF pia imefanikiwa kuwa na ofisi visiwani Zanzibar ambayo inahudumia wanachama walioko huko pamoja na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko.

Ofisi ya Zanzibar ambayo ipo jengo la Makao Makuu ya Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) ghorofa ya nne inasimamia shughuli zake katika mikoa mitano ya Zanzibar, ambayo ni Mjini Magharibi, Kusini & Kaskazini Unguja na Kusini & Kaskazini Pemba.

Ofisi hiyo ilianzishwa Disemba mwaka 2011 iki-wa na lengo la kusimamia huduma za matibabu kwa wafanyakazi wa Muungano na wageni wanaofika Zanzibar kwa shughuli za kikazi au likizo.

Majukumu makubwa ya ofisi Zanzibar ni sawa na ofisi nyingine za Mfuko huu, zikiwa ni pamoja na kusajili wanachama, kukusanya michango, ukaguzi wa waajiri na watoa huduma, elimu kwa umma, watoa huduma na wanachama na malipo kwa watoa huduma wanaohudumia wanachama wake.

Makundi yaliyofikiwa na kujiungaMeneja wa NHIF Zanzibar, Ismail Kangeta anas-ema kuwa hivi sasa ofisi ya NHIF Zanzibar imefanikiwa kuwafikia waajiri 120 kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Taasisi Binafsi, Wanafunzi, Wajasiriamali, Watoto kupitia mpango wa Toto Afya na Viongozi wa Dini.

Ofisi ya Zanzibar ina jumla ya wanachama wachangiaji 22,355 sawa na wanufaika 102,094.Vituo vya kutolea huduma Anasema wanachama wa NHIF Zanzibar wanahudumiwa kwenye vituo 39 vya matibabu ambavyo vipo Unguja na Pemba.

Vituo hivyo vinaanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali za Rufaa na Taifa. “Vituo vya kutolea huduma vya ngazi ya taifa ni pamoja Hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali ya Tasakta na vituo ngazi ya kanda ni Hospitali ya Al Rahma na Tawakal ambazo ziko upande wa Unguja.

Kwa upande wa Pemba kituo kikubwa ni Hospitali ya Abdalah Mzee ambayo ni ngazi ya Mkoa. Huduma zinazotolewa kwa wanachama kupitia vituo hivi ni huduma bora na zinazoridhisha kwa kuwa huduma zote za msingi zinapatikana zikiwemo za kitaalam kama Dialysis, CT Scan, MRI, ICU,” anasema Kangeta.

Elimu kwa ummaAnaeleza ofisi ya Zanzibar imejipanga kuhakikisha wanachama na wadau kwa jumla wanapata elimu na taarifa muhimu kwa wakati. Wadau hupata taarifa kwa kupitia njia mbalimbali zikiwemo za radio, runinga, machapisho na kuwafikia katika maeneo yao.

Aidha, ofisi hii ina utaratibu wa kutoa elimu kwa kutembelea waajiri maeneo yao ya kazi na kupitia mikusanyiko mbalimbali ya wananchi ikiwemo maonesho ya shughuli mbalimbali.

Pamoja na kutoa elimu, NHIF pia huendesha shughuli za upimaji wa afya bure na utoaji wa elimu ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo la damu na saratani.

Kuulinda Uhai wa Mfuko Kangeta katika hili anasema, ofisi ya Zanzibar inashiriki katika kuhakikisha kwamba NHIF inakuwa salama na inadumu kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho. Katika jitihada za kulinda uhai wa Mfuko, ofisi ya Zanzibar hufanya uhakiki wa madai kabla ya kulipa ili kujiridhisha kuwa malipo hayo ni halali.

Ofisi pia hutoa elimu kwa wanachama na watoa huduma kuhusu matumizi salama ya kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kuchukua hatua za kisheria endapo kuna ubad-hilifu wowote juu ya Mfuko unajitokeza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya watoa huduma Visiwani Zanzibar wanasema kuwa Mfuko umekuwa msaada mkubwa katika uboreshaji wa huduma za matibabu kutokana na ongezeko la mapato wanalopata kutokana na kuhudumiwa wanachama wa Mfuko huu.

Victoria Mwankajuki ambaye ni Meneja Uhusiano wa Hospitali ya Tasakta anaeleza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo ni wanachama wa NHIF.“Katakana na ongezeko na wateja ambao ni wanachama wa NHIF imetusukuma kama hospitali kuboresha huduma na kuongeza wataalam ambao wanatoa huduma za kibingwa hivyo kwa sasa mwanachama wa NHIF hana sababu ya kwenda Dar es Salaam kufuata huduma,” alisema.

Naye Dk Hamis Hamis ambaye ni Daktari Bingwa Hospitali ya Mnazi Mmoja, anaupongeza Mfuko kwa kuweka huduma zake visiwani humo ambazo zimekuwa chachu ya maboresho ya huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali.“Mapato yanayotokana na NHIF yanatusaidia kwa kiasi kikubwa sana kubore-sha huduma zetu, pia wanachama wake wanapata huduma bila vikwazo vyovyote hivyo wana uhakika wa matibabu,” alisema Dk Hamisi.

Kwa upande wa wanachama wa NHIF walioko visiwani humo, wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wazi kuwa bila uwepo wa NHIF wasingeweza kumudu gharama za matibabu hivyo wametoa wito kwa wananchi wengine ambao hawajajiunga na Mfuko kuhakikisha wanajiunga mara moja ili wawe na uhakika wa huduma za matibabu.

Akizungumzia uwepo wa Ofisi ya NHIF Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga anasema kuwa, Mfuko umejipanga kuhakikisha unawafikia wananchi katika maeneo yote visiwani humo ili wapate huduma za matibabu zenye uhakika zaidi.

“Tuna mtandao mpana wa huduma za matibabu hivyo wanachama wetu wana uhakika wa kupata huduma hizi bila wasiwasi,” anasema Konga.