Ulipaji bili za maji kwa wakati uliasisiwa na Mwalimu Nyerere


Ulipaji bili za maji kwa wakati uliasisiwa na Mwalimu Nyerere

Tunu ya amani aliyoiasisi Mwalimu Nyerere imesaidia kutupa mwanga wa kuwa wabunifu na kujituma katika kuhudumia wananchi wengi zaidi wa Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha, Bagamoyo, Mlandizi na miji mipya ya Kisarawe na Mkuranga ambayo sasa itaanza kusimamiwa na DAWASA.

Maji ni rasilimali muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai. Kwa Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo, asilimia 75 ya maji yanayotumika huchotwa kutoka Mto Ruvu ulio na chanzo katika milima ya Uluguru iliyopo mkoani Morogoro.

Aidha, upo mtambo mdogo na mkongwe wa maji, ujulikanao kama mtambo wa Mtoni ambao maji yake hutoka katika Mto Kizinga. Vyanzo vingine vya maji ni kutoka katika visima virefu vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Wataalamu wa maji wanabainisha kuwa asilimia 70 ya Dunia ni maji, lakini ni asilimia tatu tu ya maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu na asilimia 97 ni maji ya chumvi na yenye madini mbalimbali yasiyoweza kutumiwa.

Kutokana na umuhimu huo mkubwa wa Maji katika maisha, Watanzania tuna kila sababu ya kuthamini mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika kuhakikisha kuwa rasilimali za maji ikiwemo vyanzo vyake vinatunzwa kwa ajili ya kizazi kilichopo na vizazi vya baadaye.

Aidha kwa namna ya pekee, Baba wa Taifa aliweka sera za kuboresha sekta ya maji nchini wakati tunapokumbuka miaka 20 tangu alipotutoka Oktoba 14, 1999. Jambo moja kubwa lililofanywa na Serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na Mwalimu Nyerere ni kusisitiza umuhimu wa maji katika Dira ya Taifa katika kipindi chake cha uongozi.

Kwa kudhihirisha hili ulipaji wa huduma ya maji katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa ni muhimu.

Masuala ambayo alitilia mkazo ni pamoja na:

• Kushirikisha jamii katika kupanga, kutekeleza na kuendesha miradi ya maji.

• Kuweka mgawanyo wa majukumu kwa kila ngazi kutoka taifa, wilaya na vijiji.

• Kuweka taratibu na sheria zinazotakiwa kutumika katika sekta ya maji kama sheria ya maji Namba 10 ya mwaka 1981.

• Kuwashirikisha wan-awake katika suala la maji kama njia mojawapo ya kuzingatia usawa wa kijinsia.

Aidha alisisitiza suala zima la kulipia huduma za maji na alianza na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Kumbukumbu zilizopo katika Bunge la Tanzania, zinadhihirisha jambo hilo kuwa Januari 6, 1966, Rais, Mwalimu Nyerere alitia saini muswada wa sheria ya shughuli za maji Namba 5 ya mwaka 1966.

Muswada huo ulirekebisha sheria ya zamani iliyosimamia shughuli za maji ya mwaka 1965. Sheria hiyo ilirekebishwa kwa kuongeza kifungu 25(A) ambacho kilikuwa ni kifungu maalumu kwa ajili ya Idara ya Maji ya eneo la Dar es Salaam.

Kifungu hicho 25 (A) kilihusu viwango vya bili ya maji kwa eneo la Dar es Salaam ambapo kilipungua muda wa kulipia bili ya maji kutoka siku 30 hadi siku 15 kifungu kilisema “Vifungu 22, 24 na 25 vya sheria ya shughuli za maji Namba 5 ya 1966 vitahusika na Idara ya Maji ya eneo la Dar es Salaam tu, kwa kufuta maneno siku thelathini, na kuweka maneno siku kumi na tano katika ulipaji wa bili za maji”.

Muswada huo ulipit-ishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Desemba 23, 1965 na kutiwa saini na Mwalimu Nyerere ili kuanza kutumika rasmi Januari 6, mwaka 1966.

Hivyo Serikali ya sasa inapohimiza wananchi kulipia maji ni vyema watambue kuwa jambo hili limeanza tangu enzi za Mwalimu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja anabainisha kuwa kumbukumbu ya miaka ishirini ya Mwalimu Nyerere inapaswa kutoa chachu ya wakazi wa Dar es Salaam kulipa huduma ya maji kama ilivyoasisiwa tangu enzi za Mwalimu.

“Maji ni huduma adhimu na takatifu, tangu maji yanatoka kwenye vyanzo mpaka kumfikia mteja huchukua mchakato mrefu na gharama kubwa, hii inaenda sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kumtua mama ndoo ya maji kichwani inayotekelezwa na DAWASA katika Jiji la Dar es Salaam, Miji ya Kibaha, Kisarawe, Mkuranga na Bagamoyo mkoani Pwani,” alisema Mhandisi Luhemeja.

Luhemeja anabainisha kuwa, Mamlaka imetenga asilimia 40 ya mapato yake katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Majisafi na Majitaka itakayoweza kufikisha lengo la asilimia 95 ya upatikanaji majisafi na asil-imia 30 ya huduma ya Majitaka ifikapo 2020.

“Utekelezaji wa miradi hii ya Majisafi na Majitaka inayofanywa kwa fedha za ndani inatokana na ulipaji wa bili za maji za wateja wetu na mpaka sasa zaidi ya miradi 30 inatekelezwa na DAWASA kutokana na fedha zinazopatikana kutokana na bili za maji zinazolipwa na wananchi tunaowahu-dumia,” alisema

Mhandisi Luhemeja ambaye pia alichukua fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wakubwa na wadogo kwa kuendelea kuiunga mkono DAWASA.

Luhemeja anasema miradi ipatayo 15 imekwisha kamilika ambayo ni Mradi wa Maji Tabata, Bonyokwa, Tabata Kisukuru, Mradi wa Maji Kiwalani awamu ya pili na ya tatu, Mradi wa Maji Saranga, Kiembeni, Kitopeni, Kilimahewa, Lulanzi, Salasala na Zinga Moto.

Alisema miradi 10 inakaribia kuanza kutekelezwa hivi karibuni ambayo ni Mradi wa Maji Minazi Minene, Makurunge awamu ya pili, Mingo awamu ya pili, Mabwepande, Kilindoni, Kidunda, Zegereni, Disulanya, Kibaha TAMCO na kazi ya kuweka mtandao wa maji eneo la Buza.

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya kwanza kutuwekea misingi bora iliyotuwezasha kuboresha huduma ya maji,” alisema na kuongeza kuwa sasa DAWASA inajikita katika kuboresha huduma ikiwemo kutumia teknolojia ya kisasa katika kuingiza ramani na mifumo yote ya maji iliyokuwepo tangu hata kabla ya Uhuru katika ramani za kielektroniki ili kuweza kuwa na usimamizi endelevu wa huduma.

Tunu ya amani ali-yoiasisi Mwalimu Nyerere imesaidia kutupa mwanga wa kuwa wabunifu na kujituma katika kuhudumia wananchi wengi zaidi wa Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha, Bagamoyo, Mlandizi na miji mipya ya Kisarawe na Mkuranga ambayo sasa itaanza kusimamiwa na DAWASA.