Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) kinavyokidhi ubora wa ubunifu wa majengo nchini


Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) kinavyokidhi ubora wa ubunifu wa majengo nchini

AAT ni familia kubwa ya Wabunifu nchini Tanzania inayohakikisha inasaidia maendeleo ya wanataaluma hiyo kwa kufanya na kuwezesha uendeshaji na uhudhuriaji mafunzo endelevu kazini (CPD); na kwa kutanua wigo wake kwa kushirikina na Mashirika ya Kimataifa ya Wabunifu.

Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) kilianzishwa mnamo 1982 na kinajivunia jumla ya wanachama 566 kote nchini. Hii ni pamoja na wanachama 328 waliosajiliwa, wahitimu 40, wanafunzi 191 na wataalam wa ufundi 7.

AAT ni familia kubwa ya Wabunifu nchini Tanzania inayohakikisha inasaidia maendeleo ya wanataaluma hiyo kwa kufanya na kuwezesha uendeshaji na uhudhuriaji mafunzo endelevu kazini (CPD); na kwa kutanua wigo wake kwa kushirikina na Mashirika ya Kimataifa ya Wabunifu.

AAT inafanya kazi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha mazingira yaliyojengwa na uimara wake kwa kutoa msaada wa ushauri kupitia semina na makongamano mbalimbali.

AAT imekuwa ikitoa msaada wa kiufundi kwa Bodi ya Usajili ya Wabunifu na Wakadiriaji Majengo (AQRB) kwa miaka kadhaa. Hii inaanzia kwa  wanachama wake kutumika kama watu rasilimali katika  utoaji wa mafunzo  ya kujitayarisha kwa ajili  ya mitihani ya kitaaluma ya kati na wa mwisho, pamoja na kutoa  watu wa rasilimali katika semina kadhaa.

AAT kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Technische Berlin (TU - Berlin), Taasisi ya Goethe, na Jumuiya ya Ulaya ilirudisha jengo hilo (Old Boma) na kuanzisha Kituo jijini Dar es Salaam cha Urithi wa Ubunifu Majengo Tanzania (DARCH). Inakusudia kuokoa na kukuza Urithi wa Ubunifu Majengo nchini Tanzania, ikianzia jijini Dar es Salaam, ikifuatia nchini kote na hatimaye kanda ya Afrika Mashariki.

AAT kwa kila mwaka hutoa tuzo ya mwanafunzi bora wa mwaka wa mwisho wa Ubunifu Majengo katika Chuo Kikuu Ardhi. Lengo ni kuwapa motisha wanafunzi kufanya vyema kwenye masomo yao.

AAT ina uhusiano na mashirika kadhaa ya kimataifa ambayo ni pamoja na Taasisi ya Wabunifu Majengo Afrika Mashariki.(EAIA) , Jumuiya ya Wabunifu Majengo ya Afrika (AUA), Jumuiya ya Kimataifa ya Wabunifu Majengo (UIA) na Chama cha Ubunifu Majengo cha Taasisi ya Wabunifu Majengo ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CAA).

Dhima

Kukuza ubora katika Ubunifu na kutoa huduma kwa umma na kuhakikisha kuwa jamii inapata faida nyingi kutokana na huduma zinazotolewa na Wabunifu Majenzi.

Dira

Kuwa kundi kubwa nchini linaloshinikiza ulindaji maslahi ya Wabunifu katika kiwango bora na pia kuhakikisha huduma ya Mbunifu Majengo inamfikia mwanachi wa hali ya chini.

Mikakati

  • Kuongeza uelewa wa umma juu ya umuhimu wa    kuwashirikisha Wabunifu wa majengo katika miradi  na mipango ya uendelezaji ardhi kwa majenzi na ujenzi wenyewe.
  • Kupanua uwakilishi wa AAT katika vyombo vya kitaifa vya kutengeneza sera na katika vyombo vya kimataifa ikiwa ni pamoja na EAIA, AUA, UIA na CAA,
  • Kuboresha hali ya kifedha ya AAT ili iweze kufanya shughuli mbalimbali zinazolenga kuinua ustawi wa taaluma ili kuboresha utoaji huduma kwa jamii .
  • Kuandikisha wanachama wapya ambao ni wanafunzi; kuwaandaa kama kundi fulani la wanachama wa makampuni wanachama wa baadaye ili kuongeza wigo wa Wabunifu wanataaluma wenye weledi.
  • Kuendeleza na kudumisha imani ya umma katika uwezo na uadilifu wa Wabunifu kwa kuwataka wanachama hao kukidhi kiwango cha juu zaidi cha maadili na weledi; kulinda masilahi ya umma kwa kukuza na kutekeleza kanuni za kitaalam na Maadili kwa wabunifu wote wanaofanya shughuli zao nchini Tanzania.
  • Kuangalia daima na kulinda maslahi na matarajio ya Tanzania katika juhudi zote za maendeleo ambazo zina athari za kiuchumi, kijamii na kimazingira katika uhai wa taifa.

Muundo

Muundo wa Jumuiya ya Wabunifu Majenzi Tanzania unajumuisha Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) na Baraza.

Mkutano Mkuu wa Mwaka

Mkutano Mkuu wa Mwaka ndiyo chombo cha juu cha AAT. Unafanyika mara moja kila mwaka. Kila baada ya miaka miwili Mkutano Mkuu hufanyika pamoja na uchaguzi wakati ambao viongozi wapya huchaguliwa na kuhudumu kwa muda wa miaka hiyo miwili.

Baraza

Baraza ni chombo cha kutekeleza majukumu ya kila siku. Inajumuisha Rais, Makamu wa Rais, Katibu, Mweka Hazina, Rais Mstaafu na wajumbe sita wa Baraza watakaochaguliwa. Mwanachama wa kumi na mbili ni Mkuu wa Idara ya Usanifu wa Chuo Kikuu cha Ardhi. Baraza linakutana mara moja kila mwezi.

Nini unahitaji kuwa mwanachama wa AAT?

Hatua nyepesi:

  1. Unapaswa kuwa na Shahada ya kwanza / stashahada / Mwanafunzi wa Masomo ya Ubunifu / Ubunifu wa ndani/ Usanifu Mazingira/ Teknolojia ya ubunifu.

Fomu za maombi zinapatikana katika Ofisi za AAT au upakue kupitia tovuti ya AAT www.aat.archi

Rudisha fomu ya maombi iliyojazwa na kusainiwa.

Maombi yako yatapitia katika mchakato wa AAT unaozingatia Taratibu na Kanuni

Utajulishwa kupitia taarifa zako katika fomu ya maombi

 

Wasiliana nasi:

Honorary Secretary,

Architectural Association of Tanzania,

Old Boma, Sokoine Drive/ Morogoro Road,

P.O Box 8275 Dar es Salaam, Tanzania

Phone: +255 22 2113194

Mobile: +255 768 373897