NIC kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo nchini kupitia bima ya mazao


NIC kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo nchini kupitia bima ya mazao

Kwa kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa ni wazi kwamba aina hiyo ya bima itasaidia kujen­ga uchumi kwa kiwango kikubwa. Mbali na ujenzi wa viwanda, aina hiyo ya bima itakuwa pia mkom­bozi kwa wakulima pale majanga yanapotokea.

Wakati taifa likiadhimisha miaka zaidi ya 20 ya huduma za Bima hapa nchini, sekta ya Bima imeendelea kukua na kupata mafanikio makubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima kwa kush­irikiana na wadau wa sekta hiyo, wametoa mchango mkubwa sana katika kuhakikisha sekta ya bima inakuwa na manufaa kwa kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Mchango huo umefanya baa­dhi ya kampuni na mashirika ya bima kuwa wabunifu kwa kuja na bidhaa mbalimbali za bima ambazo zinawapa wananchi uwanja mpana wa kuchagua huduma.

Miongoni mwa bidhaa za bima ambazo zinaonekana kuja kuleta tija katika nyanja ya maendeleo hapa nchini ni bima ya mazaokutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Kwa kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa ni wazi kwamba aina hiyo ya bima itasaidia kujen­ga uchumi kwa kiwango kikubwa. Mbali na ujenzi wa viwanda, aina hiyo ya bima itakuwa pia mkom­bozi kwa wakulima pale majanga yanapotokea.

Bima ya mazao itawasaidia wakulima wa Tanzania, si tu kuepukana na majanga, bali pia kukopesheka katika taasisi za fedha na hivyo kuwa na uhakika wa kulima kisasa.

Afisa Mwandamizi wa Bima kutoka Shirika la Bima la Taifa, Catherine Nangali, anaeleza namna NIC inavyotoa bima hiyo pamoja na faida zake kwa wakulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.

Tueleze kuhusu bima ya mazao inayotolewa na NIC

Bima ya mazao ni kinga inayokinga mazao ya mkulima yanapokuwa shambani dhidi ya changamoto mbalimbali kama ukame, mafu­riko, upepo, mvua zilizozidi, magonjwa na wadudu wasiotibi­ka, moto pori n.k.

Faida za bima hii ni zipi kwa wakulima na sekta ya kilimo kwa ujumla?

Faida za bima ya mazao ni kama zifuatazo;

• kumfanya mkulima awe na amani (peace of mind) kwani hana hofu ya kupoteza mtaji/nguvu zake alizowekeza katika shamba lake pale atakapo­kumbwa na changamoto kama za ukame, magon­jwa na wadudu, moto, upepo n.k.

• Kumfanya mkulima awekeze zaidi katika shu­ghuli za kilimo kwa kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka katika taasisi za kifedha.

• Kumsaidia mkulima kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia pembejeo bora za kilimo kama mbe­gu bora, mbolea, trekta n.k.

• Kumfanya mkulima awekeze zaidi kwenye kilimo kwani ana uhakika wa kuvuna ama kulipwa pale atakapopata majanga shambani.

• Kufanya kilimo kiwe ende­levu kwa kumpatia mkulima elimu kutoka kwa maafisa ugani ambao watatembelea mashambani na kutoa elimu/ushauri wa kilimo cha kisasa.

Utaratibu na vigezo vya kupata bidhaa hii ya bima ya kutoka NIC uko vipi?

Utaratibu wa kupata bidhaa hii ya bima kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) upo kama ifuatavyo;

• Mkulima awe na shamba kuanzia ekari moja

• Mkulima ajisajili katika ofisi zetu zilizo karibu naye, (Tuna matawi katika mikoa karibia yote ya Tan­zania)

• Kwa wakulima wadogo, tutasajili katika AMCOS/ ama vikundi ili kuwafikia kwa urahisi na wingi pia kwa gharama nafuu.

• Mkulima atatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo atatakiwa kuandika taar­ifa zake na mazao anayo­lima.

• Mkulima awe tayari kuli­pia ada ya bima.

Mapokeo ya bidhaa ya bima ya mazao yako vipi?

Wakulima wamepata faraja sana kwa uanzishwaji wa Bima hii ya mazao kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana na changamoto nyingi katika kilimo bila kupata suluhisho. Hivyo kwa uanzishwaji wa bima za hizi wakulima wamepata faraja sana na kuipokea bidhaa hii kwa moyo mmoja.

Ni majanga ya aina gani ambayo yanafidiwa na bidhaa hii ya bima?

Majanga yanayofidiwa na bidhaa hii ni ukame, mafuriko, mvua zilizozidi kiasi, magonjwa na wadudu wasio tibika, upepo mkali, moto pori, uharibifu wa wanyama pori n.k.

Ni hatua gani ambazo mmiliki wa bima hii anatakiwa kuzifuata pindi tu atapakapopata janga ili aweze kufidiwa?

Pindi mkulima anapoona viashiria vinavyopelekea uharibi­fu wa mazao yake anatakiwa kutoa taarifa katika ofisi zetu zilizopo karibu yake ili kuruhusu afisa wa bima/bwana shamba kutembelea shamba lake na kush­auri hatua stahiki.

Pindi mkulima atakapopatwa na majanga shambani kwake atatakiwa kutoa taarifa mapema ili taratibu za fidia zifanyike kwa haraka.

Bidhaa ya bima ya mazao inayotolewa na NIC inato­fautiana vipi na ile inayotolewa na taasisi nyingine za bima?

Bidhaa yetu ni tofauti kabisa kwani sisi tunahudumia mkulima wa chini kabisa kuanzia mkulima anayelima hekari moja tofauti na wengine ambao wana pendelea kutoa huduma hii kwa wakulima wakubwa tu. Sisi hatubagui na tuna lengo la kumfikia kila mku­lima atakayehitaji huduma zetu.

Kilimo biashara ni nguzo muhimu kuelekea uchumi wa viwanda. Kwa namna gani Shirika la Bima la Taifa linasaidia ukuaji wa sekta ndogo ya kilimo biashara nchini?

Shirika la Bima la Taifa tunat­ambua kwamba kilimo bisahara ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi hususani kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda.

Hivyo, uanzishwaji wa bima hii ni hatua muhimu kuelekea kwe­nye mapinduzi ya kilimo biashara kwa sababu kutasaidia sekta ya kilimo kukua kwani mkulima ataweza kuwekeza zaidi katika shughuli za kilimo bila hofu hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao ambayo itachangia pia katika kupatikana kwa bidhaa nyingi zitakazo hamasisha uanzishwaji wa viwanda nchini.

Bidhaa hii ya bima ya mazao ni nguzo katika mnyororo wa thamani wa kilimo kuanzia kwa mkulima mdogo mpaka kwa mku­lima mkubwa kwa sababu bima hii inakinga mtaji wa mkulima aliowekeza shambani usiweze kupotea pale atakapo kutana na changamoto mbalimbali kama nilivyozielezea hapo juu.

Mnatoa wito gani kwa wakulima na taasisi za kilimo kuhusu bid­haa hii ya bima ya kilimo?

Tunawakaribisha wakulima kupata huduma zetu na msimu huu tutatoa huduma za bima ya mazao kwa wakulima wa Pamba katika Mkoa wa Simiyu, ikifuati­wa na Kahawa Mkoa wa Kagera na mikoa mingine kwa mazao mbalimbali. Wakulima waondoe hofu kuwekeza katika kilimo kwani sasa wamepata ulinzi wa uw