Mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto Tanzania yawe ajenda ya kitaifa


Mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto Tanzania yawe ajenda ya kitaifa

Kiwango cha watu walioathirika na ukatili wa kimwili kipo juu, ambapo kutokana na Utafiti wa Demografia na Afya Tanzania wa mwaka 2015/16 , Mkoa unaoongoza ni Mara kwa asilimia 61 na Shinyanga asilimia 60.

Ukatili dhidi ya wanawake na wato­to umekuwa ni changamoto kubwa sana nchini na duniani kwa ujumla.

Hapa nchini, Serikali yetu ya Jam­huri ya Muungano wa Tanzania imepi­ga hatua katika mwitikio wa kushu­ghulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kusaini na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ya kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, lakini bado mifumo ya ndani ya nchi haiendani na matakwa ya mikataba hiyo.

Katika kusitasita huko kwa jamii katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) limeazimia kupam­bana na tatizo hilo na limekuwa liki­chukua hatua mbalimbali za kuhakik­isha kwamba mfumo wa kitaifa wa ulinzi wa wanawake na watoto tangu kuanzishwa kwake mpaka leo ukoimara.

Gazeti la Mwananchi lilishiriki kati­ka mjadala ulioendeshwa na baadhi ya wafanyakazi wa CDF ofisini kwao, wakiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtend­aji wa CDF, Lennyster Byalugaba, Meneja wa Programu, Wilbert Muc­hunguzi, Meneja wa Uhakiki Ubora, Dorothea Ernest, Afisa Ulinzi wa Mto­to, Sophia Temba, Afisa Mawasiliano, Winfrida Makuru na Afisa Msaidizi Ulinzi wa Mtoto, Irene Massawe, wakielezea kuhusiana na hali ya uka­tili dhidi ya wanawake na watoto na jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na shirika hilo.

Ieleweke kuwa, ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolo­jia, kimwili, kiafya au kiuchumi.

Ukatili wa kijinsia unajumuisha ukatili wa kingono kwa wanawake na watoto, unyanyasaji wa majumbani, ukatili wa kiuchumi kwa wanawake na mila hatarishi ,zenye madhara kamavile ndoa za utotoni na ukeketaji.

Aina za Ukatili

Kuna ukatili wa aina mbalimbali, kutegemea na eneo linaloathirika zaidi baada ya kufanyiwa ukatili huo. Kama ambavyo hapo juu tuligusia kwa uch­ache. Tukianza na ukatili wa kingono, huu huhusisha matendo kama vile ya uba­kaji na kulawitiwa kwa jinsi zote, yaani wasichana kwa wavulana, kushikwa sehemu za mwili bila ya ridhaa, kulazimishwa kushiriki katika ngono bilaya ridhaa, miluzi, shambulio la aibu,kuwaonyesha watoto picha za ngono nk.

Pili, ukatili wa kimwili, huu unahusi­sha vitendo vyote vinavyoweza kuathi­ri mwili kama vile kupigwa, kukeket­wa, kuunguzwa moto, kufinywa n.k.

Ukatili mwingine ni wa kisaikolo­jia ambapo huhusisha vitendo vyote anavyofanyiwa mtoto au mwanamke vinavyomuathiri kiakili kama vile kutukanwa, kufokewa, kutoaminiwa, kudhalilishwa kwa maneno,kusingiziwa vitu, kumfanya mtoto au mwanamke kujiona duni/dhaifu katika kufanya jambo fulani n.k.

Ukatili wa kiuchumi ni vitendo vyote anavyofanyiwa mtoto au mwanamke vyenye lengo la kumnyima fursa yakustawi kiuchumi kama vile kuzuiwa kurithi mali, kusimamia miradi ya kibi­ashara, kutopewa nyadhifa za juu za kazi, kuzuiwa kufanya kazi, n.k.

Ni zipi sababu za ukatili dhidi ya watoto na wanawake na athari zake kwa ustawi wa watoto na wanawake na taifa kwa ujumla?

Wahenga wana msemo wao kuwa“Kila penye kufuka moshi, basi kuna moto;” vivyo hivyo, hata kwenye ukatili dhidi ya wanawake na watoto hautokei tu bali kuna , sababu zilizojificha nyuma yake.

Moja ya sababu kubwa ni umaskini Moja ya sababu kubwa ni umaskini Ni rahisi sana kwafamilia maskini kutengeneza ukaribuna watu watakaowatimizia mahitajiyao mbalimbali pale maji yanapow­afika shingoni. Kutokana na hali hii,mtoto au mwanamkemwenyewe anajikuta katika mazingira ya kufanyiwa ukatili aidha wa kingono,ndoa za utotoni au mwingine ule katika jitihada za kutaka kutimiza mahitaji yake kwa muda fulani.

Tukiachana na umaskini, ipo sababu iliyojichimbia mizizi na imekuwa kilio cha mwanamke wengi. Nazung­umzia mfumo dume ambao umemu­weka mwanamke na mtoto rehani kufanyiwa kila aina ya ukatili na bado utaendelea kama hatutabadilika.

Si jambo la kushangaza kuendelea kushuhudia watoto wa kiume wakien­delea kucheza mpira na wa kike kwen­da kuchota maji visimani majira ya usiku au kuamini kuwa mwanamke hawezi kusimamia biashara hata kama wazo la biashara na mtaji vimetoka kwake.

Nini kinachoendelea Mkoani Mara mpaka leo?

Kiwango cha watu walioathirika na ukatili wa kimwili kipo juu, ambapo kutokana na Utafiti wa Demografia na Afya Tanzania wa mwaka 2015/16 , Mkoa unaoongoza ni Mara kwa asilimia 61 na Shinyanga asilimia 60.

Miaka ya nyuma hali ilikuwa mba­ya zaidi kutokana na mila hatarishi ambazo kwenye jamii ya leo zina­onekana kupitwa na wakati, lakini bado zinaaminiwa na kutekelezwa na jamii ya Wakurya ambapo ukeketaji umeonekana kuwa ni fahari kwa mwa­namke na mtoto wa kike. Ukatili huu ni mbaya sana kufanyiwa mwanamke kutokana na kuathiri sehemu kubwa ya maisha yake.

Jambo jingine ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wanaharakati wa masuala ya kijinsia na haki za bin­adamu ni Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ambayo wanadai kuwa ni moja ya 1971 ambayo wanadai kuwa ni moja ya vikubwa vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Sheria hiyo inawaruhusu wavulana kuoa wakiwa na umri wa miaka 18 na wasichana kuolewa wakiwa na mia­ka 15 kwa ridhaa ya wazazi na miaka 14 kwa kibali cha Mahakama. Hivyo kuwanyima wasichana haki yao ya kusoma na kuchagua nani na wakati gani wa kuolewa,” Afisa Mawasiliano wa CDF, Winfrida Makuru anaeleza.

Hali ya ukatili kwa wanawake na watoto ipo vipi nchini?

Ukirejea ripoti ya UNICEF ya mwaka 2009 inaonyesha kuwa, watoto 6 kati ya 10 wanafanyiwa ukatili wa kimwili na ndugu wa karibu. Mtoto mmojakati ya wawili wamefanyiwa ukatili wa kimwili na mwalimu kabla ya miaka 18. Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kwamba ukatili wa kingono kwa watoto wa kike ni asilimia 27.9na watoto wa kiume ni asilimia13.4;ambapo wasichana 3 kati ya 10 na mvulana 1 kati ya 7 wamefanyiwa ukatili wa kingono. Pia, kutokana na utafiti wa Demografia na Afya Tanzania mwaka 2015/16, asimilia 40 ya wanawake wenye umri wa kuan­zia miaka 15 hadi 49 wanafanyiwa uka­tili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Utafiti huo unaenda mbali zaidi na kuainisha kuwa, asilimia 10ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa uke­ketaji, ambapo kati ya hao asilimia 35 wamefanyiwa ukeketaji kabla ya kufikisha mwaka mmoja.

Inaweza kushangaza lakini ni ukwe­li mtupu kuwa Manyara ndio Mkoa unaoongoza kwa ukeketaji kwa asilim­ia 58, ukifuatiwa na Dodoma (47%), Arusha ( 41%) na Mara ( 32%).

Takwimu hizi ni uthibitisho tosha wa namna vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nawatoto vimekuwa vikiongezeka Tanzania. Yapo baadhi ya maeneo ambayo ukatili umekuwa ukifanyika sana. Asilimia kubwa ya maeneo hayo yakiwa ni yale tunayoyaamini kuwa ni salama kwa watoto wetu, maeneo kama vile shuleni, sehemu za ibada, mitaani, kwenye daladala, majumbani n.k.

Nini mchango wa CDF katika kup­inga ukatili dhidi ya wanawake na watoto? Mmefanikiwa kwa kiasi gani mpaka sasa?

Kutokana na kwamba jukumu la ulinzi wa mtoto ni la kila mtu, Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) limekuwa liki­tekeleza programu kuu tatu zenye lengola kuwalinda watoto na wanawake dhi­di ya ukatili hapa nchini.

Afisa Msaidizi Ulinzi wa Mtoto kuto­ka CDF, Irene Massawe anaelezea jiti­hada hizo: “Programu ya Ulinzi wa Mtoto inahusika katikakuhakikisha mfumo wa kitaifa waulinzi wa mtoto ni imara. Hivyo, CDFinafanya kazi kwa karibu sana na Jeshi la Polisi,Idara ya ustawi wa jamii, vyombo vya sheria,vyombo vya habari na wananchi wote kulinda ustawi wa watoto nchini ili kutokomeza ukatili dhidi ya wan­awake na watoto. Tukumbuke kwamba ulinzi wa mtoto ni jukumu letu sote.”

Kutokana na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/18- 2021/22 na kwa ushirikiano wa karibu na Serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CDF imewezesha uanzishwaji wa kamati 3 za ulinzi wa wanawake na watoto(moja ya Mkoa na mbili za Wilaya), kituo cha mkono kwa mkono(One-stop centre) katika Hospitali ya Mwananya­mala, kuwajengea uwezo Afisa wa Jeshi laPolisi, kwenye namna ya kushughulikia kesiza ukatili pamoja na kutoa vitendea kazi kwa madawati 22 ya Polisi ya Jinsia na Watoto katika maeneo tunayofanyia kazi na kutoa mafunzo mbalimbali ili kuweza kuimarisha mfumo waulinzi wa mtoto.

Pia, kwa kushirikiana na Polisi dawati la Jinsia na Watoto makao makuu na shirika la UNFPA, ukarabati wa ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto umefanyika na ni endelevu kwenye baadhi ya mikoa ya Mara, Manyara na Kigoma.

“Programu nyingine ni uwezeshaji wa wasichana ambayo ina lengo la kujenga uwezo wa watoto wa kike kati­ka kutokomeza changamoto za ndoa za utotoni, mimba za utotoni na uke­ketaji, kukuza uelewa wa jamii katika uongozi na afya ya uzazi. Pia, kuhakiki­sha watoto wa kike na kiume wanajit­ambua katika mambo yanayowahusu sambamba na utoaji wa taarifa pale wanapoona haki zao za msingi zinaki­ukwa. Haya yote yanafanywa kupitia klabu za watoto wa ndani ya shule na wasichana wa nje ya shule.”

Irene anamalizia: “Ushiriki wa wanaume na wavulana katika kuku­za na kutetea haki za wanawake na wasichana ni programu nyingine inayotekelezwa na CDF. Lengo kuu ni wanaume na wavulana kukuza, kulinda na kutetea haki za wanawake kulinda na kutetea haki za wanawake asilimia kubwa ya wanaohusikakatika vitendo vya ukatili dhidi ya wan­awake na wasichana ni wanaume . CDF iliona kuna umuhimu wa kuhakikisha wanaume na wavulana wanashiriki kikamilifu katika jitihada na mikakati ya kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji.”

Afisa Mawasiliano wa CDF, Winfrida Makuru anaeleza namna programu ilivyofanikiwa: “Mwanzoni haikuwa rahisi kuwashirikisha wanaume, lakini kwa sasa hali imebadilika na kutia moyo kwa kuwa mwitikio ni mzuri sana. Kwa kiasi kikubwa, hali hii imechagizwa na uanzishwaji wa vikundi vya akina baba ambavyo vimekuwa vikipatiwa mafunzo juu yausawa wa kijinsia, majukumu ya akina baba na namna ya kuwalinda watoto na wanawake Kwa kuamini mwanaume ni mtu anayesikilizwa,tumewashirikisha viongozi wa kimila na wa kidini katika kuchagiza mabadiliko katika jamii kwa ura­hisi.”

Programu ya mwisho, ni utetezi na ushawishi ambapo ni katika kuhakiki­sha sera, sheria, mipango na programu mbalimbali za kiserikali zinazingatia utu na ustawi wa mtoto na mwa­namke. Hapa tunafanya kazi moja kwa moja na kamati mbalimbali za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan Kamati ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Ofisi ya Spika na Makamu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza­nia na vyombo vya habari; na hasa kupendekeza marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayosababi­sha watoto wa kike wafanyiwe vitendo vya ukatili.

Mnadhani kwa nini jambo hili lina­takiwa kuwa ajenda ya kitaifa?

Zipo sababu zinazoweza kuelezwa kwa nini jambo hili liwe ajenda ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na takwimu za ripoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mwaka 2018 zinaonyesha kuwa asilimia 91 ya ukatili unaofanywa dhidi ya watoto ni ukatili wa kingono huku asilimia 9 zilizobaki ni za aina nyingine za ukatili. Takwimu hizi zitumike kutufungua macho ili tufanye kazi kwa ukaribu sana na serikali kushughulikia suala la ukatili kama ajenda ya kitaifa ili kasi ya vitendo hivyo viweze kupungua hapo baadaye.

Pia, Serikali imekuwa ikitumia gharama nyingi sana katika kulishu­ghulikia suala la ukatili dhidi ya wato­to na wanawake, ambapo waathirika hutibiwa bure mpaka pale wanapokaa sawa. Fedha hizi za Serikali zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za kimaendeleo endapo ingelibeba jambo hili katika mabega yake kama ajenda ya taifa.

Mngepewa fursa ya kupendekeza nini kifanyike ili kukomesha viten­do hivi vya ukatili nchini, mnge­pendekeza nini?

Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF)limeandaa mapendekezo yanayo­takiwa kufanyiwa kazi ili kutokomeza au kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake nchini.

Afisa Ulinzi wa Mtoto wa CDF, Sophia Temba anaeleza mapendekezo hayo: “Tunatoa rai kwa Bunge litunge sheria na kupitisha sera zenye tija kwa ulinzi wa watoto na wanawake na ambazo hazitakuwa zikikinzana na sheria nyingine. Tukisalia hapo hapo, ni muhimu kuwepo na mabadiliko ya vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971. Sambamba na hilo, tunaviomba vyombo vya habari kutumia majukwaa yao kueleza zaidi kuhusiana na ukatili dhidi ya watoto na wanawake na mwendelezo wake ili jamii ishtuke kutoka usingizini na kuona kuwa yanayofanyika hayafai na kuona kuwa yanayofanyika hayafai na ,” anaeleza Sophia.

Sophia amesisitiza kuwa, taasisi zote zenye malengo yanayofanana yakupambana na ukatili dhidi ya wan­awake na watoto kufanya kazi kwa umoja ili kufanikisha jukumu hilo ambalo ni wajibu wa kila mmoja wetu. Kwa ufupi, Jeshi la Polisi, idara ya jamii, hospitali na jamii, wote inabidi wafanye kazi kwa karibu. Amewataka viongozi wa kidini kupaza sauti kutumia maandiko matakatifu ili wanajamii wawe hofu ya Mungu kwa kile wanachofanya dhidi ya wanawake na watoto.

Changamoto mnazokabiliana nazo(CDF) katika harakati za kupinga ukatili wa watoto na wan­awake ni zipi? Na mnazitatuaje?

Meneja wa Uhakiki Ubora, Dorothea Ernest anaeleza changa­moto hizo: “Changamoto ni sehemu ya ukuaji kama taasisi, na CDF haijayumbishwa na hali hiyo badala yake inaendelea kuwa imara zaidi. Changamoto mojawapo ni utayari wa jamii yenyewe kutaka kulizungumzia suala hilo. Imekuwa vigumu kwa familia nyingi kueleza uwepo wa matukio haya katika maeneo yao, kutaja wahusika na kuripoti kituoni na badala yake watu kienyeji, jambo hili linaleta ugumu kwa CDF na taasisi kama hii kuweza kutoa msaada.

Huwezi kuacha kuzungumzia mila na desturi zenye mizizi katika jamii zinazofanya ukeketaji kama changamoto nyingine kubwa. Hali imebadilika kwa kuwa viongozi wengi wa kimila wameelimika na wameanza kuona ath­ari za ukeketaji baada ya kupata mafunzo mbalimbali kutoka CDF juu ya madhara ya ukatili. Changamoto nyingine ni CDF kutokusambaa sehemu kubwa ya Tanzania, kwani inafanya kazi katika mikoa mitatu tu: Dares Salaam, Dodoma na Mara. Hivyo, inakuwa ngumu kufahamu na kufuatilia kesi zinazohusu ukatili unaofanywa dhidi ya wanawake na watoto katika mikoa mingine.’’

Mna ujumbe gani kwa Watanza­nia?

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Lennyster Byalugaba anasema kuwa, “Suala la ulinzi wa watoto na wanawake ni mtambuka na ni la kila mtu, hivyo kila mtu anatakiwa kuwa­jibika kwa nafasi yake na kuhakiki­sha kuwa utu na ustawi wa watoto na wanawake unakua, unalindwa na unaboreshwa."