MUWSA inatimiza kwa vitendo ndoto ya Rais Magufuli ya kufikisha huduma bora za maji kwa wananchi


MUWSA inatimiza kwa vitendo ndoto ya Rais Magufuli ya kufikisha huduma bora za maji kwa wananchi

Historia ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi inaanzia mwaka 1994 ilipoanzishwa kama idara ya Serikali inayojitegemea (Urban Water Department). Mabadiliko haya yalifuatia utekelezaji wa Sera ya Maji ya mwaka 1991 iliyotilia mkazo wa uanzishaji wa miradi na Taasisi za Majisafi na Majitaka zinazojitegemea kiuendeshaji. Mwaka 1998 MUWSA ilianzishwa rasmi kama Mamlaka inayojitegemea.

Historia ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi inaanzia mwaka 1994 ilipoanzishwa kama idara ya Serikali inayojitegemea (Urban Water Department). Mabadiliko haya yalifuatia utekelezaji wa Sera ya Maji ya mwaka 1991 iliyotilia mkazo wa uanzishaji wa miradi na Taasisi za Majisafi na Majitaka zinazojitegemea kiuendeshaji. Mwaka 1998 MUWSA ilianzishwa rasmi kama Mamlaka inayojitegemea.

 Hali ya Utoaji Huduma ya Majisafi

Mamlaka inatoa huduma kisheria kwenye Manispaa ya Moshi kwa asilimia 100 na wastani wa saa 23.5. eneo la Manispaa lina wakazi takribani 205,113 kulingana na ukokotozi toka kwenye Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

 MUWSA pia inahudumia kwa asilimia 100 eneo la Mji Mdogo wa Himo katika Kata ya Makuyuni ambayo inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 22,400.  Aidha, katika Mji Mdogo wa Himo eneo la Kata ya Njiapanda Mamlaka haijaanza kulihudumia kutokana na kuwepo Jumuiya za Watumia Maji ambazo hazijakabidhi eneo hilo.

Aidha, kutokana na mahitaji makubwa ya huduma ya maji safi katika maeneo yaliyoko nje ya Manispaa ya Moshi, Mamlaka imeendelea kutafuta vyanzo vya maji vinavyoweza kuhudumia maeneo husika na kubuni miradi ya maji inayowezesha kutoa huduma bora ya maji safi katika maeneo hayo ya Vijijini.

Kutokana na kuhudumia maeneo ya nje ya Manispaa, Mamlaka imeongezewa eneo la huduma lenye Kata 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kisheria kwa tangazo la Serikali namba 573 la tarehe 05/10/2018 ambapo tayari Mamlaka ilishapokea maombi ya kutoa huduma maeneo hayo na kuanza kujenga na kuboresha miundombinu ya maji. Kata hizo ni Pamoja na Mabogini, Kimochi, Old Moshi Mashariki, Mamba Kusini, Mwika Kusini, Marangu Mashariki, Kibosho Mashariki, Uru Kusini, Uru Kaskazini, Uru Mashariki, Old Moshi Mgharibi na Mbokomu,

Ufanisi katika kutekeleza majumu yake, kumeiwezesha MUWSA kuaminiwa na Wizara ya Maji na kupewa majukumu ya kutekeleza miradi kwa niaba ya Wizara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Same na Rombo.

Katika kipindi cha Mnne, MUWSA imekuwa miongoni mwa  Mamlaka bora katika utoaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa mazingira kati ya Mamlaka 25 za Miji mikuu ya Mikoa na kutunukiwa tuzo na Mamlaka ya udhibiti wa wa nishati na Maji nchini (EWURA).

Mafanikio ya mamlaka katika kipindi cha miaka minne  (2015-2019).

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi imefanikiwa kutoa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa asilimia zaidi ya 95. Mafanikio hayo yanaweza kutazamwa katika mambo yafuatayo

Jedwali namba 1: mafanikio ya Mamlaka kwa miaka minne 2015-2019

1

Wastani wa uwezo wa  uzalishaji maji kwa siku

34,736 m3

43,431 m3

47,015 m3

51,899 m3

2

Wastani wa masaa ya kutoa huduma ya majisafi kwa wakazi

23

23.5

23.5

23.5

3

Uwezo wa matanki ya kuhifadhi maji

9,086 m3

9,302 m3

9,527 m3

9,977 m3

4

Idadi ya wateja wa maji safi

27,459

30,392

33,744

38,196

5

Idadi ya wateja wa maji taka

2,733

2,801

2,866

2,952

6

Wastani wa asilimia ya upotevu wa maji kwa mwaka

22%

23%

21.7%

20.3

7

Mtandao wa usambazaji wa majisafi

421km

495.6km

573.32km

690.06km

8

Urefu wa mtandao wa majitaka

59.3km

62.11km

66.4km

67km

9

Ufanisi wa kukusanya mapato

89%

89.85%

92%

94%

10

Makusanyo

6,196,510,162

7,297,426,133

7,910,702,781

8,296,686,976

11

Hesabu za Mamlaka za kila mwaka kaguliwa na kupatiwa hati safi.

Hati Safi

Hati Safi

Hati Safi

Ukaguzi unaendelea

12

Tathimini ya utendaji inayofanya na EWURA

Mwaka wa Fedha

Kigezo

Nafasi

 

 

2015/2016

Maji taka

2

 

 

Maji safi

1

 

 

2016/2017

Majitaka

1

 

 

Majisafi

1

 

 

2017/2018

Majisafi

3

 

 

Majitaka

2

 

 

2018/2019

Tathmini bado inaendelea

 

Miradi ya kuongeza kiasi cha majisafi iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka minne

Mamlaka imetekeleza jumla ya miradi kumi na mbili (12) ya Majisafi na kuongeza uwezo wa kuzalisha Maji  kutoka mita za ujazo 34,736 mwaka 2015 hadi kufika mita za ujazo 51,899 mwaka  2019.  Miradi hiyo ni kama vile ujenzi wa mradi wa usambazaji maji eneo la Shabaha na Sanya line B, Ujenzi wa Chemichemi ya Kisimeni, Visima virefu vya KCMC, Chemichemi ya Mkashilingi, Kaloleni, Mradi wa usambazaji Maji eneo la Newland, Ujenzi wa Chemichemi ya Mang’ana, Chemichemi ya Kyaronga, Mradi wa Kipure, Mradi wa Nikodemo pamoja na mradi wa Maji Musa Toroka. Miradi yote hii imetekelezwa kwa fedha na wataalamu wa ndani na kugharimu jumla ya Shilingi  6,968,806,238.

Kutekelezwa kwa miradi hii kumewezesha wananchi wa Kata za Mabogini, Uru Kusini, Rau, Mbokomu, Kiboriloni, Soweto, Uru Kaskazini, Mwika Kusini, Old Moshi Masharikik, Kimochi na Kata ya Masama Rundugai Wilaya ya Hai kupata huduma ya Maji ya uhakika.

Aidha Mamlaka imetekeleza jumla ya miradi minne kwa kutumia fedha kutoka Wizara ya Maji yenye lengo la kuondoa kero ya Maji katika maeneo ambayo yalikuwa na changamoto. Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Maji Mweka Sungu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Vijiji vya Mweka na Sungu pamoja na Chuo cha Wanyama pori Mweka, Mradi wa Mamba Kusini kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Mamba Kusini, Mradi wa Maji Mrusunga kwa ajili ya kuhudumia Kata ya Mbokomu pamoja na mradi wa wa Ntenga Wilayani Same ambao unahudumia Kata ya Vuje. Miradi yote hii imegharimu jumla ya Shilingi 2,728,015,635.

Sambamba na miradi ya uzalishaji Maji, Mamlaka pia imeweza kutekeleza miaradi mikubwa miwili ya upanuzi wa mtandao wa Majitaka katika maeneo ya Rau, Pasua, Ushirika wa Neema, Chuo Kikuu cha Mwenge na maeneo ya Kcmc. Miradi hii imegharimu kiasi cha Shilingi 862,917,500.

Miradi hii itasaidia upatikanaji wa huduma za majisafi kwa masaa 24 katika maeneo ya; Shabaha na Sanya line B (wakazi 4,030), Kariwa na Longuo A (wakazi wapatao 5,180), Rau, Korini kusini na Kiboriloni (wakazi wapatao 18,578), Karanga na Soweto (wakazi wapatao 34,000), Manosa, Sanya line A, Msufini na Chekereni (wakazi wapatao 10,507), Mabogini na Harusini (wakazi wapatao 7,236), Newland

(wakazi wapatao 8,204), Uru Kaskazini na Uru Kusini (wakazi wapatao 33,985), Vijiji vya Matala, Kondeni na Mawanjeni

(wakazi wapatao 12,304), wakazi wa Kata ya Old Moshi na Kimochi, wakazi wa Kata ya Old Moshi Mashariki na maeneo ya Jirani na wakazi wa Kata ya Masama Rundugai Wilayani Hai.

Ubora wa maji yanayosambazwa

Maji yanayozalishwa na MUWSA yanakidhi ubora wa Shirika la Viwango Nchini yaani TBS pamoja na Shirika la Afya Duniani WHO. Moshi ndio mahali pekee ambapo mtumiaji anaweza kuchota maji moja kwa moja toka kwenye bomba na kunywa bila kupata madhara. Vyanzo vya maji vimetunzwa vyema kutokuruhusu uchafunzi wowote.

Maji yanayopotea (non revenue water)

Kama ilivyo kwa Mamlaka nyingine za maji nchini, MUWSA imekuwa na changamoto ya upotevu wa maji kwa kiasi cha wastani wa asilimia 20.3 ambao ni juu ya kiwango kinachokubalika cha chini ya asilimia 20.

Hata hivyo muwsa imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha kiwango hicho kinateremka hadi kufikia chini ya kiwango kinachokubalika. Katika kuhakikisha hilo, imejiwekea mikakati ya kupambana na kiasi cha maji yanayopotea ikiwa ni pamoja na:

  1. Kubainisha mita zote zisizohesabu matumizi ya Maji kwa usahihi na kuzibadilisha
  2. Kubainisha mabomba chakavu na kuyabadilisha
  3. Kuhakikisha mita zinasomwa kwa usahihi na kwa wakati uliopangwa kuzingatia mzunguko wa usomaji (Reading cycle)
  4. Kuhakikisha taarifa zote za uvujaji zinafanyiwa kazi kwa wakati kwa kadri zinavyotolewa taarifa
  5. Kufunga dira za Maji kwenye “fire hydrants” zote
  6. Kutoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa kila atakayetoa taarifa ya wizi wa maji na kuthibitika kuwa ni kweli.

Kupambana na wizi wa maji           

Kutumia maji bila kuyalipia ni ni kosa kisheria. Mamlaka imejiwekea utaratibu wa kupambana na wizi wa Maji katika maeneo inayoyahudumia ikiwa ni pamoja na kuwa na kampeni inayoitwa “Tajirika na Mamlaka”. Hii humpatia mwananchi fursa ya kupata kiasi cha shilingi 100,000 akitoa taarifa ya wizi au hujuma ya miundombinu ya maji na ikathibitika kuwa kweli. Vilevile Mamlaka imekuwa ikishirikiana na Viongozi kuanzia kwenye ngazi ya mtaa au kitongoji katika kuhakikisha wanatoa taarifa ya hujuma pale inapotokea.

Uhusiano na umma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi inadumisha uhusiano na umma tunaohudumia kwa kuwapatia taarifa mbalimbali zinazohusiana na huduma kwa njia mbalimbali kama vile Mikutano ya wananchi kuanzia ngazi ya mitaa, matangazo kwa kutumia vyomba mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na Redio, Luninga, Magazeti na mitandao ya jamii.

Vile vile Mamlaka imekuwa ikichangia shughuli mbalimbali za maendeleo kuunga mkono juhudi za Serikali. Imechangia katika sekta ya Elimu, afya pamoja na makundi yenye mahitaji Maalumu.

Mazingira

Mamlaka inashirikiana na wadau mbalimbali katika shughuli za utunzaji wa Mazingira. Upandaji wa miti rafiki wa maji katika maeneo yote ya vyanzo vya Maji, kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa vikundi mbalimbali vya jamii pamoja na kushiriki kampeni za Kitaifa na Kimkoa za kimazingira. Mamlaka imetunukiwa tunzo ya utunzaji wa Mazingira kwa mwaka 2017 katika kutambua mchango wa Mamlaka katika Mazingira.

Juhudi za Mamlaka za kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa saa 24 na Uondoaji wa Majitaka zimepelekea Manispaa ya Moshi kuwa ya kwanza kwa usafi wa Mazingira nchini Tanzania.

Mita za malipo ya kabla (Prepaid Water Meters)

Mamlaka imeanza utaratibu wa kutumia mita za malipo ya kabla kwa baadhi ya wateja wake. Zoezi hili limeanzia kwa wateja  wa kundi la Taasisi. Zoezi hili ni moja ya mpango wa kupunguza madeni kwa kumuwezesha mteja kulipia huduma kwa kadri anavyotumia. Hadi sasa takriban wateja 16  tayari wana mita za malipo ya kabla. Mpango wa MUWSA ni kuhakikisha wateja wengi zaidi wanafungiwa mita hizi kulingana na bajeti ya kila mwaka. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Mamlaka imejiwekea malengo ya kufunga mita za malipo ya kabla 97.

Rasilimali watu

Mamlaka imejiwekea utaratibu wa kuboresha hali za wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na

            I.            Kuboresha mishahara

          II.            Kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu

        III.            Ushirikishwaji wa watumishi kupitia baraza la wafanyakazi na mkataba wa hali bora kazini

       IV.            “Promotion” kwa wafanyakazi

Utaratibu huu umekuwa chachu kwa wafanyakazi wa MUWSA kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuweza kuleta tija kwa Mamlaka na mtu mmoja mmoja.

Mipango ya mamlaka hadi mwaka 2025

Mamlaka imejiwekea mipango mbalimbali hadi kufikia 2025 ambayo ni pamoja na;

ü  Kuongeza uwezo wa uzalishaji wa Maji kwa mita za ujazo 42,939

ü  Kuongeza maunganisho mapya ya wateja 12,000

ü  Kupanua mtandao wa Majisafi kwa kilometa  95.45

ü  Kupanua mtandao wa Majitaka kwa kilometa 21

Changamoto 

Pamoja na mafaniko iliyoyapata MUWSA, bado kuna changamoto ambazo zinaifanya Mamlaka kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 100. Changamoto hizo nia kama zifutazo.

Na.

Changamoto

Athari/Utatuzi

1

Gharama kubwa za ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka.

Uchakavu wa miundo mbinu ya Majitaka kwa baadhi ya maeneo hasa katikati ya Mji.

Hata hivyo Menejimenti imechukua hatua kwa kuchukua Mkopo benki ili kutekeleza baadhi ya kaziza ujenzi wa miradi na ukarabati wa miundombinu.

3

Taasisi za Serikali kutolipa anakara zake kwa wakati.

Kutokulipwa madeni haya kumeifanya Mamlaka kushindwa kulipa baadhi gharama za uendeshaji pamoja na kutekeleza miradi kwa wakati.

Aidha, Menejimenti inaendelea kufuatilia kwenye Tasissi na Wizara husika ili walipe madeni yao.

 Matarajio ya Mamlaka

MUWSA imejipanga kuhakikisha inaendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi tu kwa kuhakikisha inaendelea kutoa huduma kwa asilimia 100 na kwa saa 24 katika eneo zima la huduma.

Wito wa Mkurugenzi Mtendaji

Mkurugenzi Mtendaji MUWSA anatoa wito kwa wadau wote kushirikiana na MUWSA katika kuhakikisha huduma ya Maji inakuwa endelevu katika maeneo yote ambayo MUWSA inahudumia. Hii ni pamoja

ü  Kulipa ankara ya huduma kwa wakati

ü  Kutoa taarifa ya hujuma dhidi ya miundombinu ya MUWSA

ü  Kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti

ü  Kutokuvamia na kuharibu vyanzo vya Maji

KAULI MBIU:

MUWSA: UWAJIBIKAJI NA HUDUMA BORA