Wilaya ya Kongwa inatimiza majukumu chini ya kauli mbiu ya HAPA KAZI TU


Wilaya ya Kongwa inatimiza majukumu chini ya kauli mbiu ya HAPA KAZI TU

Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii inazingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Tawala (CCM) kwa kipindi cha Mwaka 2015 – 2020 kama ilivyoainishwa katika ibara mbalimbali katika sekta saba za Afya, Maji, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Kilimo, Mifugo na barabara ambazo kwa miaka minne zimetumika jumla ya Tshs 27,250,473,988.14 Kati ya fedha hizo Tshs 23,105,732,804.14 zimetumika kugharamia miradi ya maendeleo na Tshs 4,144,741,184/= zimetumika kugharamia Mpango wa Elimu bila Malipo.

Jumapili ya Oktoba 25, 2015 Watanzania walipiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ukiwa ni uchaguzi wa tano tangu chaguzi za vyama vingi kuanza tena.

Chaguzi nyingine za vyama vingi nchini Tanzania zilifanyika mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010, ambapo katika uchaguzi wa 2015, Dk John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi alishinda uchaguzi na Novemba 5, 2015 aliapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara baada ya kuingia madarakani, Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa chini ya Dk Magufuli ilianza kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020 na hivi sasa mafanikio mbalimbali yanaonekana hadi katika ngazi za Wilaya.

Tukiwa katika maadhimisho ya miaka minne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, zipo Wilaya ambazo zimepata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za kimaendeleo. Miongoni mwa Wilaya hizo ni Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.

Mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Wilaya ya Kongwa ni kama ifuatavyo:

Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kwa kipindi cha Novemba, 2015, agosti, 2019

Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii inazingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Tawala (CCM) kwa kipindi cha Mwaka 2015 – 2020 kama ilivyoainishwa katika ibara mbalimbali katika sekta saba za Afya, Maji, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Kilimo, Mifugo na barabara ambazo kwa miaka minne zimetumika jumla ya Tshs 27,250,473,988.14 Kati ya fedha hizo Tshs 23,105,732,804.14 zimetumika kugharamia miradi ya maendeleo na Tshs 4,144,741,184/= zimetumika kugharamia Mpango wa Elimu bila Malipo.

Makusanyo ya Serikali

Maelekezo ya Ilani ya uchaguzi ibara ya 20(c) inalenga kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuongeza vyanzo vya mapato na kupanua wigo wa walipa kodi ili kuongeza uwezo wa Serikali wa kugharamia huduma za kijamii na kiuchumi.

Makusanyo ya ndani ya Halmashauri mwaka 2015/16 na 2018/19

Ukusanyaji wa mapato ya vyanzo vya ndani umekuwa ukiongezeka kila mwaka. Mwaka 2015/2016 makusanyo yalifikia 64%, Mwaka 2016/17 ulifikia 61%, Mwaka 2017/18 ulikuwa 74% na 2018/19 ni 85%. Kuongezeka kwa mapato kumesaidia kutoa huduma kwa jamii kwa ufanisi na tija.

Miradi ya Maendeleo

Maendeleo ya Jamii

Uwezeshaji wananchi kiuchumi

Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ibara ya 60(a)i na 63(a),(d) Halmashauri zote nchini zinaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa Wanawake na vijana kwa mujibu wa sheria ili kuwezesha mikopo yenye masharti nafuu na kutoa elimu ya ujasiriamali na biashara ili kuwawezesha kuongeza ajira, ujuzi wa kujiajiri, fursa za kipato na kujikimu.

Ili kufanikisha azma hii Halmshauri ya Wilaya ya Kongwa imeendelea kutekeleza jambo hilo, ambapo kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano jumla ya shilingi 118,706,420/= zilitengwa na kutolewa kwa vikundi 41 vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.

Sekta ya Afya

Hali halisi ya sekta ya afya

Wilaya ina hospitali ya Wilaya Moja, Vituo vya Afya 4 na Zahanati 56 (47 ni Serikali na 9 ni za binafsi). Aidha, Halmashauri inaendelea na ujenzi wa Zahanati 18 katika vijiji mbalimbali vya Wilaya.

Wilaya imeendelea kutekeleza lengo la kila Kijiji kuwa na Zahanati, Kata kuwa na Kituo cha Afya na Wilaya kuwa na hospitali kwa kutekeleza miradi ifuatayo;

Miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha Novemba, 2015 hadi Agosti, 2019

Maelekezo ya Ilani ibara ya 50 (a) (i) kila Kijiji kuwa na Zahanati, kila kata kuwa na Kituo cha Afya na kila Wilaya kuwa na Hospitali yanaendelea kutekelezwa katika maeneo ambayo huduma hizi hazijakamilika pamoja na kujenga hospitali za Wilaya katika Wilaya zote mpya.

Upanuzi na Ujenzi wa Hospitali

Hospitali ya Wilaya ya Kongwa ilianzishwa kama kituo cha afya hivyo kuwa na majengo yasiyokidhi mahitaji. Serikali ya Awamu ya Tano katika mkakati wa kuboresha huduma za Afya nchini, hospitali ya Wilaya imeendelea kuboresha miundombinu yake kwa kujenga jengo la Maabara, jengo la upasuaji na jengo la kutunzia dawa.

Ujenzi kwa sasa unaendelea na umefikia asilimia 50. Gharama za ujenzi wa majengo haya hadi kukamilika utagharimu Tshs 400,000,000.00. Ununuzi wa Jenerata la kufua umeme umefanyika kwa Tshs 40,000,000.00 na linatumika.

Aidha, ukarabati wa wodi ya watoto wenye utapiamlo mkali katika hospitali ya Wilaya umefanyika sambamba na kuwekewa vifaa kwa gharama ya 14,157,525.00.

Ujenzi na Upanuzi wa vituo vya Afya

Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi Juni 2019 Wilaya imeendelea na kazi za ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya 4 ambavyo ni Mkoka, Kibaigwa, Mlali na Ugogoni.

Katika vituo vya Afya vya Mlali na Ugogoni upanuzi mkubwa umefanyika, ambapo kila Kituo cha Afya kina majengo yafuatayo; nyumba ya mtumishi, ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto, ujenzi wa jengo ya kuhifadhia maiti (Mortuary), ujenzi wa maabara na jengo la upasuaji.

Ujenzi wa majengo hayo umekamilika na umegharimu Tshs 800,000,000.00. Aidha, ujenzi wa vyumba vya upasuaji katika vituo vya Afya Kibaigwa na Mkoka uliogharimu Tshs 60,000,000.00 vimepauliwa na ujenzi unaendelea. Kukamilika vituo kutawezesha utoaji wa huduma bora za dharura za upasuaji.

Ujenzi wa Zahanati

Wilaya inatekeleza Mpango wa Afya ya Msingi (MMAM), ujenzi wa zahanati mpya 18 unafanyika ambapo zahanati 8 katika vijiji vya Msingisa, Mseta Bodeni, Muungano, Sagara A, Ijaka, Manyata, Mautya na Lenjulu ujenzi umekamilika kwa gharama ya Tshs 441,298,890.00.

Aidha, ujenzi wa zahanati 11 katika vijiji vya Manghweta, Chang’ombe, Manungu, Mtanana B, Msunjulile, Mlanje, Tubugwe Juu, Manghweta, Chamae, Ngutoto na Suguta. Gharama za utekelezaji hadi sasa ni Tshs 448,290,000.00. Ujenzi wa miradi ya sekta ya afya upo katika hatua mbalimbali.

Sekta ya maji

Hali ya Huduma ya Maji Vijijini

Maelekezo ya Ilani ibara ya 54 (a)(i) kuongeza upatikanaji wa maji vijijini kutoka 67.7% hadi 85% ifikapo 2020 kwa kuwapatia wananchi waishio vijijini huduma ya maji safi, salama na ya kutosha.

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa kipindi cha miaka 4 katika Wilaya imeboreka ambapo asilimia ya wananchi wanaopata maji kutoka katika vyanzo vilivyoboreshwa imeongezeka kutoka 49.1% mwaka 2015 hadi 57.4% Juni, 2019.

Hii ni kutokana na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 10 mikubwa ya maji katika vijiji vya Chiwe, Kongwa Maji, Machenje, Matongoro, Songambele, Chigwingwili, Mlali Iyegu, Mlali Bondeni, Ibwaga na Pembamoto kwa gharama ya Tshs 6,058,419,656.30.

Aidha, utekelezaji wa miradi minne unaendelea katika vijiji vya Makawa, Mtanana, Vihingo na Kongwa Mjini. Miradi hii hadi kukamilika itagharimu jumla ya Tshs 2,503,697,784.16.

Sekta ya Elimu

Wilaya ina jumla ya shule za elimu ya awali na msingi 117 (Serikali 113, zisizo za Serikali shule 4). Kuna shule za Sekondari 31(26 ni za Serikali na 5 zisizo za Serikali), shule moja ya ufundi stadi Mnyakongo, shule zenye vitengo vya elimu Maalum 3 katika shule za Msingi Mlali, Kongwa na Mkoka na Vituo vya walimu (TRC) 4 katika Kata za Kongwa, Mlali, Kibaigwa na Mkoka.

Elimu ya awali

Maelekezo ya Ilani ibara ya 52 (a)(i) uandikishwaji rika lengwa la watoto wa darasa la elimu ya awali unaongezeka kutoka 45% mwaka 2015 hadi kufikia 100% mwaka 2020.

Uandikishaji Elimu ya Awali

Mwaka 2015 uandikishaji ulifikia watoto 9529 (Wavulana 4,601; Wasichana 4,928) sawa na 95% ya lengo. Mwaka 2016 uandikishaji ulifikia watoto 11,818 (Wavulana 5,519; Wasichana 6,299) sawa na 109% ya maoteo ya 10,857.

Mwaka 2017 uandikishaji ulifikia watoto 11,236 (Wavulana 5,500; Wasichana 5,736) sawa na 57% ya maoteo ya 19,871. Mwaka 2018 uandikishaji ulifikia watoto 11,215 (Wavulana 5507; Wasichana 5708) sawa na 80% ya maoteo ya 14,108 na Mwaka 2019 uandikishaji ulifikia watoto 10,941 (Wavulana 5,373; Wasichana 5,568) sawa na 75% ya maoteo ya watoto 14,608.

Elimu ya msingi

Maelekezo ya Ilani ibara ya 52 (a)(ii) uandikishwaji rika lengwa la watoto wa darasa la kwanza unaongezeka kutoka 95% mwaka 2015 hadi 100% mwaka 2020.

Uandikishaji wa wanafunzi darasa la kwanza

Mwaka 2015 uandikishaji ulifikia wanafunzi 8285 (Wavulana 3949; Wasichana 4336) sawa na 74% ya lengo. Mwaka 2016 uandikishaji ulifikia wanafunzi 11322 (Wavulana 5457; Wasichana 5865) sawa na 104% ya maoteo ya 10857. Mwaka 2017 uandikishaji ulifikia wanafunzi 15717 (Wavulana 7740; Wasichana 7977) sawa na 115% ya maoteo ya 13650. Mwaka 2018 uandikishaji ulifikia wanafunzi 15109 (Wavulana 7652; Wasichana 7457) sawa na 116% ya maoteo ya 13015 na Mwaka 2019 uandikishaji ulifikia wanafunzi 14992 (Wavulana 7218; Wasichana 7774) sawa na 111% ya maoteo ya 13550.

Mwaka 2016 ongezeko lilikuwa ni 30% na mwaka 2017 ongezeko ni 41% Mwaka 2018 ongezeko ni 42% na Mwaka 2019 ongezeko ni 37% ukilinganisha na mwaka 2015.

Ongezeko hili limetokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa elimu bila malipo na kuwafanya wananchi ambao walikuwa wanashindwa kumudu gharama za masomo kuitikia wito wa Serikali ya kuwapeleka wanafunzi wote wanaostahili kujiunga na shule kuandikishwa.

Ufaulu wa elimu ya Msingi

Ufaulu kwa mtihani wa darasa la Nne 2015-2019

Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Nne umekuwa ukiongezeka kila mwaka. Mwaka 2015 ulikuwa 88.70%, 2016 ulikuwa 91.84% na mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 96%. Mwaka 2018 ni 92%.

Ufaulu wa mtihani wa kuhitimu darasa la Saba 2015-2018

Ufaulu wa kuhitimu elimu ya msingi umekuwa ukiongezeka kila mwaka, ambapo mwaka 2015 ulikuwa 54%, 2016 ulikuwa 55% na mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 72. Aidha, ili kuinua taaluma, Serikali ya Awamu ya Tano imeajiri walimu 105 wa shule za msingi. Mwenendo wa ufaulu umekuwa ukiongezeka kila mwaka.

Ujenzi wa miundombinu katika shule za Msingi

Kwa kipindi cha miaka 4 (2015-Juni, 2019, Wilaya imekamilisha ujenzi wa madarasa 106, matundu ya vyoo 244, Nyumba 1 ya walimu, bweni moja, na bwalo moja kwa gharama ya shilingi 1,883,554,236.68 na ujenzi wa madarasa chini ya michango ya wananchi inaendelea. Aidha, shule za Msingi mpya 8 zimesajiriwa katika vijiji vya Mkombozi, Mwidonya, Visumi, Lobilo, Manyusi,Sabasaba, Saigoni na Nhembo.

Aidha, shule za msingi mpya 8 zimesajiriwa katika vijiji vya Mkombozi, Mwidonya, Visumi, Lobilo, Manyusi,Sabasaba, Saigoni na Nhembo. Shule za Msingi za Serikali ziomeongezeka kutoka 105 mwaka 2015 hadi 113 Juni, 2019.

Elimu Sekondari

Udahili wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza

Maelekezo ya Ilani ibara ya 52 (a)(iii) uandikishwaji rika lengwa la wanafunzi wa kidato cha kwanza umeongezeka kutoka 60% mwaka 2015 hadi 100% mwaka 2020.

Wilaya imeendelea kusimamia udahili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, Mwaka 2015, Wilaya ilidahili wanafunzi 1827 (Wavulana 876; Wasichana 951) sawa na 74.94% ya lengo la wanafunzi 2438. Mwaka 2016 walidahiliwa wanafunzi 2479 (Wavulana 1156; Wasichana 1323) sawa na 89.72% ya lengo la wanafunzi 2763.

Mwaka 2017 walidahiliwa wanafunzi 2838 (Wavulana 1329; Wasichana 1509) sawa na 92.08% ya lengo la wanafunzi 3082. Mwaka 2018 walidahiliwa wanafunzi 3602 (Wavulana 1689; Wasichana 1913) sawa na 93.2% ya lengo la wanafunzi 3863 na mwaka 2019 wamedahiliwa wanafunzi 4556 (Wavulana 2107; Wasichana 2449) sawa na 92.4% ya lengo la wanafunzi 4930.

Mafanikio makubwa ya uandikishaji katika elimu ya Msingi na udahili katika elimu ya sekondari unatokana na Mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano wa Elimu bila malipo ambapo Wilaya imepokea jumla ya Shilingi 4,144,741,184/= kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango.

Ufaulu wa mtihani wa kidato cha Pili 2015 – 2019

Ufaulu wa kidato cha Pili umeendelea kuongezeka kila mwaka. Mwaka 2015 ulikuwa asilimia 91.96, mwaka 2016 ulikuwa ni 95.10%, mwaka 2017 ulikuwa ni 93% na mwaka 2018 ni 94%.

Ufaulu wa mtihani wa kidato cha Nne 2015 – 2019

Ufaulu wa kidato cha Nne umeendelea kuongezeka kila mwaka. Mwaka 2015 ulikuwa ni 56%. Mwaka 2016 ulikuwa ni 62.3%. Mwaka 2017 ulikuwa ni 76.74%, na mwaka 2018 ulikuwa ni 79.52%.

Ufaulu wa mtihani wa kidato cha Sita 2015 - 2019

Shule za kidato cha sita katika Wilaya ya Kongwa ni mbili ambazo ni Kongwa Sekondari ambayo ilianzishwa kabla ya mwaka 2015 na ni ya wavulana na Ibwaga imeanzishwa mwaka 2017 na ni ya Wasichana.

Ufaulu wa kidato cha Sita umeendelea kuimarika kila mwaka. Mwaka 2015 ulikuwa 100%, mwaka 2016 ulikuwa ni 98%. Mwaka 2017 ulikuwa 100%, Mwaka 2018 ulikuwa ni 99% na mwaka 2019 ni 97.5%.

Ujenzi wa miundombinu ya shule za Sekondari

Kwa kipindi cha miaka 4 (2015-Juni,2019, ujenzi wa madarasa 49,  matundu ya vyoo 31, maabara vyumba 9, maktaba moja, mabweni 3, jiko 1 na nyumba 12 za walimu zimekamilika, Viti na Meza 629 zimenunuliwa.

Gharama ya miradi iliyokamilika ni Tshs 1,607,458,448.00. Ujenzi wa mabwalo 2 unaenelea kwa gharama ya shilingi 200,000,000.00. Shule za Sekondari mpya 2 zimesajiriwa ambazo ni Banyibanyi na Ndurugumi. Ujenzi wa shule mpya 2 unaendelea katika vijiji vya Lenjulu na Chitego. Hivyo kwa miaka 4 shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 24 hadi 26 Juni, 2019.

Sekta ya Uchumi na Uzalishaji

Kilimo

Maelekezo ya Ilani ibara ya 22 (g) (i) kushirikisha Sekta binafsi kujenga na maghala bora ya kuhifadhia mazao mbalimbali hususan viijini kwa kutoa elimu na kuondoa vikwazo vya utaratibu wa stakabadhi ya Mazao.

Ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara Wilaya imeendelea kuhimiza wakulima kutumia pembejeo na zana bora za kilimo.

Halmashauri inajenga soko katika kijiji cha Mkoka ambalo litatumika kuuzia na kuhifadhi mazao ya wakulima. Majengo yanayojengwa ni pamoja na Ujenzi wa eneo la Kukaushia Mazao, Ujenzi wa Ofisi na Ujenzi wa jengo la Kuhifadhia Mazao. Mradi huu umegharimu Tshs 302,892,100.

Mifugo

Maelekezo ya Ilani ibara ya 25 (j) Kuendeleza na kukuza masoko ya mifugo na mazao yake.

Halmashauri katika kukuza sekta ya mifugo imeweza kubuni miradi mitatu ifuatayo; kiwanda cha kongano la biashara ya Kuku na kiwanda cha kuchakata Maziwa kilichopo eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda lililopo katika kijiji cha Mbande na mnada wa mifugo Mbande.

Miradi hii hadi sasa imegharimu jumla ya Tshs 608,092,900.00.

Sekta ya Miundombinu

Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi Ibara ya 39 kuendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja, vivuko, nyumba na majengo ya Serikali kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii.

Barabara

Wilaya imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya barabara. Kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia 2015 hadi Juni 2019 tumeweza kutengeneza barabara zenye urefu wa kilomita 252.8 kwa kiwango cha changarawe/udongo na kalavati 21  kwa gharama ya Tshs.6,587,871,264.00.

Barabara za lami kilomita 2.89 zenye thamani ya Tshs 1,150,000,000.00.

Hitimisho

Ahadi yetu sisi viongozi na Watendaji wa Wilaya ya Kongwa ni kwamba tutaendelea kutimiza majukumu yetu kwa juhudi na maarifa chini ya kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.