Mafanikio ya TAWA katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli


Mafanikio ya TAWA katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli

Katika miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) imetekeleza majukumu yake makuu matatu katika kuimarisha na kuendeleza uhifadhi.

Katika miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) imetekeleza majukumu yake makuu matatu katika kuimarisha na kuendeleza uhifadhi.

TAWA imeweza kutekeleza majukumu hayo kwa mafanikio makubwa kutokana na utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Gazeti hili, Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Dk James Wakibara anasema mafanikio hayo yametokana na sababu mbalimbali.

Kuimarisha ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na mazingira yake

Dk Wakibara anasema katika kipindi cha miaka minne ya Rais John Magufuli, ulinzi wa rasilimali za wanyamapori ndani na nje ya mapori ya akiba na tengefu uliimarishwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali. Anasema, TAWA kupitia Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kukabiliana na ujangili hasa wa tembo na faru kwa nguvu zote kwa njia mbalimbali.

Anasema katika kipindi cha miaka minne, ujangili umedhibitiwa kwa mfano uonekanaji wa mizoga ya tembo inayotokana na ujangili umepungua kutoka mizoga 17 mwaka 2015/16 hadi 0 kwa mwaka 2018/19. Dk Wakibara anasema katika kudhibiti ujangili Mamlaka imejenga maghala ya kuhifadhia silaha yapatayo 18 ambayo yamekuwa na ufanisi mkubwa.

Anasema TAWA imefanikiwa kuthibiti mifugo inayoingia ndani ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu kinyume na Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009. Anasema Uvamizi wa mifugo katika maeneo ya Uhifadhi yanayosimamiwa na TAWA umepungua kwa asilimia 51% kutoka mifugo 56,708 mwaka 2016/17 hadi mifugo 27,699 mwaka 2018/2019.

Anasema, Shirika lime-fanikiwa kutatua migogoro ya mipaka kati ya maeneo ya vijiji na hifadhi katika Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu, vilevile imejenga jumla ya vigingi (beacons) 3,806 katika umbali wa mita 500 kati ya kigingi kimoja na kingine kwa kipindi cha mwaka 2017 hadi 2019.

Uanzishwaji wa jeshi usu Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) imeingia katika mfumo wa jeshi usu (paramilitary) kutoka katika mfumo wa kiraia, ambao ulizinduliwa rasmi mwezi Novemba mwaka 2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Dk Wakibara anasema Idadi ya watumishi 690 wamehitimu mafunzo ya jeshi Usu na wameongeza weledi, nidhamu na uzalendo katika utendaji kazi wao.

Kuimarika kwa utalii

Katika miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya utalii katika Mapori ya akiba imeongezeka kutoka watalii 35,479 kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 na kufikia watalii 129,428 kwa kipindi cha mwaka 2018/ 2019 sawa asilimia 234.7%.

Dk Wakibara anasema shughuli za utalii zimesababisha kuongezeka kwa pato la Shirika. Kutokana na ongezeko hilo, kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 Shirika limechangia gawio la Serikali na wananchi waliopo jirani na maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (Wildlife Management Areas-WMAs).

Mnada wa vitalu vya uwindaji

Dk Wakibarana anasema katika uongozi wa awamu ya tano, TAWA ilianzisha mfumo wa kuuza vitalu kwa njia ya kieletroniki ili kuondoa migogoro lakini pia kuongeza mapato ya Serikali. Anasema, TAWA imeuza vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada wa kieletroniki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni, 2019.

Utaratibu huu unazingatia misingi ya utawala bora, kuongeza uwazi katika tasnia ya uwindaji na kuruhusu nguvu ya soko kutoa bei ya vitalu.

Kuboresha ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi Anasema TAWA imefanikiwa kuendesha shughuli zake kwa ufanisi chini ya usimamizi bora wa Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Meja Generali (Mstaafu), Hamisi Semfuko.

Anasema, Shirika limenunua vitendea kazi vikiwepo Magari ya doria na utawala 73, visoma dira 217’GPS’, mahema 531, pikipiki 15, boti za doria 4, sha-jala (stationary) pamoja na sare za askari wa doria 6,425.

Dk Wakibara anasema sambamba na vitendea kazi shiri-ka pia limewapatia mafunzo watumishi wake wapatao 1,641, mafunzo ya muda mrefu na mfupi ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji.

Mikakati ya TAWA na maeneo mapya iliyokabidhiwa na Serikali

Licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka minne ya Rais Magufuli, TAWA imejipanga kuendeleza uhifadhi, kupambana na ujangili na kuvutia watalii zaidi katika maeneo mapya ambayo imekabidhiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Miongoni mwa maeneo hayo TAWA iliyokabidhiwa ni eneo kitalii la Kilwa ili kulihifadhi na kuvutia watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kutembe-lea eneo hilo. Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Generali mstaafu, Hamis Semfuko anasema baada ya kutembelea Kilwa wamejionea utamaduni wa malikali zilizopo na sasa TAWA inakusudia kuufanya mji wa Kilwa kama kitovu cha utalii katika Ukanda wa Kusini.

“Tunajipanga kuhakikisha tunakuza utalii katika mji huu wenye vivutio vingi vya mali kale na kitamaduni, lakini pia hapa kuna msikiti wa kihistoria uliojengwa karne ya 13, Kasri ya kifalme na fukwe nyeupe ambavyo vyote ni vivutio vya utalii,”anasema.

Anasema katika hatua za awali TAWA inatarajia kununua boti ya kisasa ya kitalii katika maeneo ya Kilwa ambayo watalii wataweza kutembea baharini na kuona viumbe mbalimbali ndani ya maji.

Anasema boti hiyo ya kisasa ya kitalii itakuwa ni ya vioo chini ambayo inawezesha watalii kuona kirahisi samaki na viumbe hao lukuki waliopo baharini Ukanda wa Kilwa. Meja Generali Mstaafu, Semfuko anasema pia katika mji huo wa Kilwa TAWA itaanzisha utalii wa Baiskeri kwa watalii kuzitumia kutembelea maeneo ya vivutio kwa kuzikodi.

Dk Wakibara anasema mji wa Kilwa una fursa nzuri za kuwekeza katika utalii kwani una maeneo mazuri ya mali kale yenye vivutio vya asili. Dk Wakibara anasema hivi sasa kuna usafiri mzuri ulioboreshwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais John Magufuli wa barabara ya lami kutoka Dar es Salaam hadi Kilwa na hivyo watalii ambao watakwenda kutembelea maeneo ya Selous wataweza kupitia Kilwa na kufanya utalii wa mali kale na fukwe.

“Tunataka kongeza radha ya utalii katika eneo la Kilwa kwa kuboresha utalii wa uta-maduni, kuongeza vionjo kwa watalii kupata historia ya mji wa Kilwa ambao karne ya 13 ulikuwa na sarafu yake na kitovu cha biashara katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki,”

anasema. Naibu Kamishna wa TAWA ambaye anahusika na masoko, Imani Nkuwi anasema TAWA itaboresha miundombinu katika maeneo ya Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko ili kutoa hamasa kwa watalii wa ndani na nje kutembelea.

Nkuwi Anasema pia TAWA inakusudia kuongeza mazao ya utalii katika maeneo hayo kwa kuongeza siku za watalii kukaa nchini, hasa wale ambao watapenda kutembelea Kilwa na baadaye kuelekea hifadhi ya Selous na nyingine za Kusini.

“Tunatengeneza mkakati wa kupata wawekezaji wa mahoteli na shughuli za kitalii kwa kuwa sasa Ukanda wa Kusini umeanza kufunguka kutokana na Serikali kujenga barabara za lami na kujengwa kiwanja cha ndege cha Kilwa,”anasema Nkuwi. Haya ndio mafanikio ya TAWA katika miaka minne ya Rais John Magufuli na mikakati yake kuendeleza mafanikio haya.

TAWA inajihusisha na shughuli za usimamizi wa rasilimali za wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa za Tanzania na Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutekeleza kazi zifuatazo:-

a) Kusimamia mapori ya akiba na tengefu

b) Kusimamia na kulinda shoroba za wanyamapori maeneo ya mtawanyiko, ardhi oevu na maeneo ya wazi yenye wanyamapori

c) Uangalizi wa wanyamapori katika maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMA).

d) Kuendeleza utalii na uwekezaji katika utalii wa uwindaji, utalii wa picha, ufugaji wa wanyamapori katika shamba (Wildlife ranches