Mafanikio ya sekta ya misitu na nyuki katika miaka minne ya Magufuli


Mafanikio ya sekta ya misitu na nyuki katika miaka minne ya Magufuli

Wakala unasimamia misitu ya hifadhi mbalimbali zilizopo nchini. Katika kipindi cha miaka minne, misitu mipya iliyoko kwenye maeneo tofauti hapa nchini ilihifadhiwa. Misitu hiyo inajumuisha hifadhi za Nyuki (Wilaya ya Nyasa, Songea vijijini na Chunya.

Msitu ni mkusanyiko wa uoto wa asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, wanyama pori, wadudu na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. Misitu inaweza kuwa ya asili au ya kupandwa na binadamu (isiyo ya asili).

Misitu ya asili ni misitu ambayo huota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu. Kwa mfano, msitu wa Udzungwa (Mkoa wa Morogoro). Misitu isiyo ya asili ni misitu ambayo hupandwa na mwanadamu.

Katika nchi yetu ya Tanzania utunzaji wa rasilimali misitu ni mdogo, watu wamekuwa wakiharibu rasilimali hii kwa makusudi, miti inakatwa hovyo, matumizi ya mkaa yamekuwa makubwa, watu kuvamia hifadhi za misitu kwa ajili ya kuanzisha makazi ya kuishi n.k.

Changamoto hizi na nyingine nyingi zimekuwa zikirudisha nyuma baadhi ya juhudi za makusudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na wadau kwa ajili ya kulinda rasilimali misitu.

Katika kukabiliana na changamoto hizi, Serikali iliamua kuunda chombo maalum cha kusimamia misitu yote iliyopo chini ya Serikali.

Chombo hicho ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambao umepewa majukumu ya kusimamia na kutunza misitu yote iliyopo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kuadhimisha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Magufuli, TFS inajivunia mafanikio ya sekta ya misitu na nyuki kwa miaka minne (2015/16- 2018/19).

Mafanikio hayo ni pamoja na:

Usimamizi bora wa misitu ya asili

Wakala unasimamia misitu ya hifadhi mbalimbali zilizopo nchini. Katika kipindi cha miaka minne, misitu mipya iliyoko kwenye maeneo tofauti hapa nchini ilihifadhiwa. Misitu hiyo inajumuisha hifadhi za Nyuki (Wilaya ya Nyasa, Songea vijijini na Chunya).

Aidha kumekuwa na upandishwaji hadhi wa hifadhi za Mazingira Asilia (Nature forest reserves). Hifadhi nyingine   ziko mbioni kutangazwa kuwa Nature Reserves. Aidha, misitu katika kipindi hicho misitu mbalimbali iliandaliwa mipango ya usimamizi.

Maendeleo ya rasilimali nyuki

Uzalishaji wa mazao ya nyuki umeongezeka. Uzalishaji asali umeongezeka kwa mwaka 2019 ukilinganisha na  mwaka 2016 huku nta ikiongezeka toka mwaka kwa mwaka 2016 ukilinganisha na zile zilizozalishwa mwaka 2016. Viwanda vipya vimejengwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuchakata mazao hayo. Aidha, idadi ya wafanyabiashara wa mazao ya nyuki imeongezeka kwa asilimia kubwa.

Upandaji miti

Mashamba (forest plantations) mapya kwa lengo la kuhifadhi mazingira, kuongeza ajira na mazao ya misitu (mbao, nguzo n.k) hivyo kuwa na ukuaji wa viwanda.

Miche ya miti ilipandwa katika mashamba huku miche mingine ikitolewa kwa wananchi na taasisi kwa ajili ya kupandwa likiwa ni ongezeko la iliyopandwa kwenye mashamba na maeneo ya wananchi.

Utatuzi wa migogoro

Migogoro katika ya hifadhi na vijiji, taasisi au watu mmoja mmoja imetatuliwa. Migogoro mingine inaendelea kutatuliwa. Katika kutatua migogoro vigingi “beacons” vimewekwa katika mipaka. Mfano wa migogoro iliyotatuliwa ni Geita, Kasulu, Derema (Muheza), Mkulazi (Morogoro), Pagale, Biharamulo, Iyondo Mswima (Ileje).

Ununuzi wa vitendea kazi

Wakala umefanikiwa kununua magari, pikipiki, matrekta, boti na Mitambo (Grader) katika kipindi cha miaka 3 ili kuboresha utendaji kazi.

Ujenzi wa miundombinu

Majengo mapya (ofisi, nyumba za watumishi, ranger out posts) vimejengwa katika maeneo mbalimbali nchini katika kipindi hicho. Aidha, majengo mbalimbali wa Wakala yamekarabatiwa na barabara mpya zimefunguliwa katika misitu.

Makusanyo ya maduhuli ya Serikali

Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Wakala umefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa maduhuli kutokana na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na Serikali ya awamu hii.

Misaada kwa jamii

Mchango wa taasisi kwa jamii ni mkubwa kwa sababhu miradi mingi ya ujenzi wa shule, zahanati, vituo vya polisi na maji imetekelezwa.

Kuimarisha viwanda vya misitu nchini

Mashamba mbalimbali ya miti yanavunwa kwa mwaka na kuhudumia viwanda tofauti tofauti hapa nchini. Viwanda vingine vya samani kote nchini vinahudumiwa na sekta ya misitu na kutoa ajira za moja kwa moja na ‘indirect’ kwa Watanzania. Mashamba ya kuvunwa yameongezeka kwa kiasi kikubwa kuanzia mwaka 2015/16 mpaka sasa.

Utalii

Mwaka 2017 ulikuwa ni mzuri kwa sekta ya utalii hapa nchini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni waliotembelea vivutio mbalimbali, baadhi yao wakiwa watu maarufu duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi aliwahi kusema Utalii unatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi. Utalii unachangia katika Pato la Taifa na fedha za kigeni.