Kampuni ya Topcom Printers inakidhi mahitaji ya huduma za uchapaji nchini


Kampuni ya Topcom Printers inakidhi mahitaji ya huduma za uchapaji nchini

Topcom Printers (TPC) ni kampuni inayofanya kazi kwenye teknolojia ya uchapaji wa dijitali. Kampuni hii ilianzishwa na kusajiliwa mnamo tarehe 5, 2001 chini ya Sheria ya Makampuni, CAP 213 ikiwa na namba ya usajili 127709 kama kampuni ya uchapaji. Kampuni hii ipo katika barabara ya Shaurimoyo /Mtaa wa Paa, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Mwanasaikolojia wa Kimarekani Abraham Maslow aliwahi kueleza sababu za kisaikolojia ambazo zinamuwezesha mtu kufanya jitahada na kutumia kile alichonacho ili kufikia malengo yake.

Moja ya sababu ambazo alizitaja katika andiko lake hilo ni motisha. Maslow alieleza kuwa motisha ni vichocheo vya ndani na nje ambavyo vinamfanya mtu kujituma zaidi na kuongeza juhudi ili aweze kufikia malengo yake ya kimaisha.

Maslow alivitaja baadhi ya vichocheo hivyo kuwa ni kuthaminiwa kwa anachokifanya, usalama mahali anapofanya shughuli zake na kutambulika mchango wake katika eneo alilopo.

Motisha ya kufanya vizuri ili kufikia malengo haipo tu kwa mtu mmoja mmoja pekee bali hata kampuni zinahitaji motisha ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Kampeni ya kutafuta kampuni bora 100 za kati nchini inayoandaliwa kila mwaka na kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia bidhaa yake ya The Citizen kwa kushirikiana na KPMG ni miongoni mwa kampeni bora zenye lengo la kuongeza motisha kwenye kampuni za kati ili ziweze kufikia malengo ya kuwa kampuni kubwa.

Kampeni hii ambayo hufanyika kila mwaka, huzitambua kampuni bora za kati 100 na kuzitunuku tuzo ili kuongeza hamasa katika shughuli wanazofanya, lengo likiwa ni kuzisaidia kufikia malengo yao ambayo kwa namna moja au nyingine huchangia kuongeza pato la taifa kwa sababu kampuni hizo zinalipa kodi na kutengeneza ajira nyingi.

Kampeni ya kampuni 100 bora za kati kwa mwaka 2019 ime-shuhudia kampuni mbalimbali zikishiriki kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kushika nafasi za juu. Kampuni ya Topcom Printers ni miongoni mwa kampuni zilizofanya vizuri kwenye kam-peni ya mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa kampu-ni ya Topcom Printers, Willy Urio anaeleza namna kampuni hiyo ilivyofanikiwa kupenya katika kundi kubwa la kampuni bora za kati kwa mwaka 2019.

Historia ya Topcom Printers

Topcom Printers (TPC) ni kampuni inayofanya kazi kwenye teknolojia ya uchapaji wa dijitali. Kampuni hii ilianzishwa na kusajiliwa mnamo tarehe 5, 2001 chini ya Sheria ya Makampuni, CAP 213 ikiwa na namba ya usajili 127709 kama kampuni ya uchapaji. Kampuni hii ipo katika barabara ya Shaurimoyo /Mtaa wa Paa, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Kampuni ya Topcom Printers ilianza kama kampuni ndogo ya uchapaji ikiwa inafanya shughuli zake ndani ya chumba kimoja lakini baadaye ilikuwa mpaka kufikia kiwango cha kuwa kam-puni ya kati.

Urio anasema wamejidhatiti katika matumizi ya teknolo-jia mpya na wafanyakazi bora wenye weledi na utaalam wa hali ya juu unaondeana na mahitaji ya soko la uchapaji ndani na nje ya nchi.

Anaeleza kuwa mashine wanazotumia katika shughuli zao ni za kisasa na za kidijitali. Aidha, wana uhusiano mzuri wa kufanya kazi na washirika na washauri katika taaluma zingine kwa utoaji wa huduma kamili za kitaalam. Topcom Printers wanalenga kuendana na mahitaji yote ya wateja wao.

Kupitia Topcom Printers kazi yako itafuatiliwa katika eneo la masoko kupitia michakato ya utunzaji wa siri za mteja kutokana na mahitaji yake na mchakato huu utaendelea hadi mteja atakapopokea mradi uliokamilika kwenye mlango wake.

Wafanyakazi wa Topcom ni watu wenye uzoefu na wanaotoa huduma bora kwa wateja, wanahakikisha ubora wa kazi ya mteja bila kujali pesa, thamani au ukubwa wa kazi, vyote hufuatiliwa kwa kiwango cha juu.

Huduma zinazotolewa na Top-com Printers

Topcom Printers wanajivunia sifa na mafanikio ambayo wamepata katika tasnia ya kuchapa zaidi ya miaka kumi na sita iliyopita. Sifa thabiti ya Topcom inatokana na utoaji wa huduma bora kwa wateja wake, kufanya kazi kwa ushirikiano na wafanyakazi wenye mwelekeo wa kuwajali wateja.

Topcom Printers wanajihusi-sha na shughuli mbalimbali ikiwemo;

Uchapaji wa kidijitali

Topcom Printers wamejidhatiti katika matumizi ya teknolojia na ndiyo maana wanafanya shughuli za uchapaji kwa kutumia njia za kidijitali. Topcom Printers wanachapa; Vitabu, vijarida, vipeperushi na lebo, Single & Multipart Forms, kadi za Mialiko na Matangazo, Alama na Mabango, Kalenda na vibebeo vya nyaraka na vifaa vya mao-fisini, vitabu vya kumbukumbu (Diary) n.k.

Usanifu wa kibunifu (Creative Graphic Design) Wafanyakazi wa Topcom Printers ni watu wenye ubunifu wa kisanifu, wanafanya kazi na mteja wakati wote mpaka kazi itakapokamilika. Kutoka wazo hadi kukamilika kwa bidhaa ya mteja wanakuwa na mteja kwa kila hatua.

Katika eneo hili la usanifu wa kibubnifu, Topcom Printers wanafanya shughuli zifuatazo; Profession Designers, Document scanning, Digital Printing, Photocopying pamoja na Proof Out.Huduma za ujarida (Bindery Services) Kulingana na kile mteja ana-chochapisha, anaweza kuhitaji huduma mbalimbali kama vile kufunga na kukata baada ya kazi yako kumalizika kuchapishwa.

Topcom Printers wanakupa huduma nyingi katika umaliziaji wa kazi yako ya uchapaji zikiwemo; Kukunja (Folding), kuweka namba (Numbering), Collating, (Binding), Stitching, Ukataji wa karatasi (Paper Cutting) pamoja na kuweka majalada (Lamination).

Huduma nyingine

Mbali na huduma zilizotajwa, Topcom Printers pia wanatoa huduma mbalimbali katika tasnia ya uchapaji wa kidijitali hapa nchini, huduma hizo zinajumuisha; utengenezaji wa business card, uchapaji wa fulana, (T-shirt Printing), utengenezaji wa risiti za kielektroniki (Point of sell rolls), fomu zilizo kwenye mfumo wa rola (computer forms), kazi za rangi (Color jobs) ambazo zinahusisha; majarida, ripoti, vyeti, kalenda, mabango ya matangazo (Posters) vipeperushi, kava za tairi (Tires Covers), mabango makubwa ya matangazo (Large Format Printing) n.k.

Pia, wanachapa nyaraka za siri kutoka taasisi mbalimbali. Matumizi ya teknolojia na ubunifu Teknolojia kwa kawaida huendelea kukua duniani hivyo bila kuendana na mabadiliko haya biashara inakuwa ngumu.

Topcom kama kampuni ya uchapaji, wanakwenda sambamba na mabadiliko haya kwa kufanya shughuli zao kwa kutumia teknolojia mbalimbali. Katika eneo hili, Topcom wanatumia mfumo wa kompyuta (Software) unaofahamika kama Ease Print Solutions ambao kazi yake ni kukadiria thamani ya bidhaa ambayo mteja anaitaka.

Mbali na makadirio ya gharama za huduma ama bidhaa, mteja anayohitaji, mfumo huu pia unafuatilia utendaji wa kazi kwenye kampuni, kufuatilia oda za wateja mbalimbali pamoja na kuhakikisha kwamba kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa.

Kwa kutumia mfumo huu, wanapata mrejesho mzuri wa kupanga bei zinazoendana na hali za wateja wao, kuandaa Proforma Invoice, hati ya kufikisha bidhaa (delivery note), Tax invoice, nyaraka za kodi pamoja na kuhifadhi kumbukumbu za wateja wetu.

Aidha, Topcom Printers wanafahamu kwamba ili kuendelea kufanya vyema sokoni ni lazima wawe wabunifu, hivyo suala la ubunifu ni moja ya vitu wanavyovipa kipaumbele sana. Katika kulitekeleza hili wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali ili kufahamu mahitaji mapya ya soko na namna soko linavyokwenda.

Tafiti hizi zinawasaidia kutambua ni kitu gani kimekosekana sokoni na vitu gani ambavyo wateja wanavihitaji kwa wakati husika, hivyo baada ya hapo wanakuja na bidhaa na huduma za kibunifu kwa bei inayoendana na hali za wateja wao.

Uwepo wa vifaa na mashine mbalimbali za kisasa za kufanyia kazi kama; Main Top Machine, Konica Press Machine, Speed Master Machine, Binding and Folding Machine, Lamination Machine, Stitching Machine, Cat-ting Machine n.k, kunawaweze-sha kuendelea kuwa wabunifu na kuwapatia wateja wao huduma wanazohitaji.

Mafanikio ya Topcom Printers

Wakiwa na miaka 18 katika soko la uchapaji, Topcom Printers wanajivunia mafanikio mbalimbali. Moja ya mafanikio hayo ni kutengeneza ajira mbalimbali kwa Watanzania. Mafanikio mengine ni kutoa huduma bora ambazo zimewafanya kuaminika na kupewa zabuni na taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na za binafsi.

Kwa sasa Topcom Printers wana-toa huduma kwenye taasisi zote za Serikali, Halmashauri za miji, Wilaya na Majiji, Mashirika ya umma na binafsi n.k. Mafanikio mengine ni pamoja na kushika nafasi ya 24 katika kampuni bora za kati hapa nchini.

Haya ni mafanikio makubwa kwa Topcom Printers kwa sababu wameona kwamba na wao mchango wao unatambulika na jamii. Kingine ni kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika azma ya kufikia uchumi wa viwanda kwa sababu ili wafike huko wanahitaji viwanda na kampuni ndogo na za kati ambazo ni za wazawa kama ilivyo kwa Topcom Printers.

Mambo ambayo wamejifunza kutoka kwenye kampeni ya Top 100Kwanza kabisa Topcom Printers wanaipongeza kampuni ya Mwananchi kupitia gazeti lake la The Citizen pamoja na KPMG kwa kuandaa kampeni hii kwa sababu ni jambo zuri ambalo linakutanisha kampuni hizi za kati mahali pamoja na kuweza kujif-unza na kubadilishana mawazo ambayo yanaweza kusaidia kampuni kupiga hatua moja mbele.

Kwenye kampeni hii Topcom Printers wamejifunza vitu vingi sana, kwanza ni kutambua mapungufu yako wapi na nini wanatakiwa kuboresha ili mwakani washike namba za juu zaidi. Kingine wamekutana na watu mbalimbali ambao wamechangia nao mawazo ya kibunifu yatakayowasaidia kusonga mbele kama kampuni.

Pia, Topcom Printers wanapenda kuwashauri waandaji waongeze nguvu katika kuitan-gaza kampeni hii ili watu wengi waweze kushiriki kwa sababu wanaposhiriki wengi ni rahisi kwa kampuni kujifunza vitu vingi zaidi. Pia, watakapokuwa na sample size kubwa katika utafiti matokeo yao yatakuwa dhahiri au ya uhakika.

Changamoto

Topcom Printers wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao. Changamoto hizo ni; ucheleweshwaji wa malipo kutoka kwenye taasisi wanazofanya nazo kazi hususani za Serikali, kukosekana kwa uwazi katika uchukuaji wa kodi kwa baadhi ya taasisi, kukosekana kwa viwanda vya kuzalisha malighafi, Topcom kama kampuni kuwa na mtaji na eneo dogo la kufanyia kazi n.k.Uwepo wa tozo nyingi zikiwemo za OSHA, Fire, huduma za Halmashauri (city service levy), Afya, TMDA, WCF, NSSF nk.

Changamoto nyingine ni TRA kutokuamini hesabu wanazowapelekewa na Topcom Printers kwa ajili ya kukotoa kodi hasa zuio la kodi (withholding tax deductions), unakuta mteja anawakata Topcom Printers kodi hii, lakini haiwasilishwi TRA au inawasilishwa lakini mawasiliano jinsi ya kupata cheti cha kuonyesha imewasilishwa ni ngumu sana kuipata.

Hivyo TRA wanashindwa kusaidia kuwasukuma hawa wateja kuziwasilisha kwa Topcom Printers.

Mikakati ya Topcom Printers

Moja ya mkakati walionao Topcom Printers ni kuongeza uwezo wa ufanyaji wa shughuli zao. Mfano kwa sasa wameagiza mashine ya kisasa ya kuten-genezea mabango makubwa ya matangazo (Large Format Printing) ambayo yataongeza ufanisi kwao zaidi.Aidha wanaboresha bidhaa zao mbalimbali za matangazo (Promotions Materials) kwa ajili ya kuuza, kama vile; fulana, kalamu, vikombe, kofia, vitabu vya kumbukumbu, kava za tairi n.k ambavyo vyote vitakuwa na nembo yao.

Kuongeza ubunifu katika ufanyaji wa shughuli zao ili waendelee kupata wateja wapya. Kuendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia, kutafuta eneo kubwa, kuongeza mtaji na vifaa, kuon-geza bidhaa na huduma n.k.

Wito kwa wateja na Watanzania

Topcom Printers inawashukuru wateja wao na Watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kuwaamini na kuwaunga mkono. Wanaomba waendelee kuwaamini kwa sababu kwa sasa wana mambo mazuri zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao.

Topcom Printers bado wana-fanya kazi nzuri na za uhakika, wanafuata maadili ya kazi zao, wanatunza siri za wateja kwa sababu wao wanachapa mpaka nyaraka mbalimbali.

Kama mtu anahitaji huduma zao mahali popote alipo hapa nchini wanaweza kuwasiliana na Topcom Printers kwa anuani ifuatayo;

Topcom Printers

Mtaa wa Shaurimoro, Ilala

S.L.P 61026,

Dar es Salaam, Tanzania

Simu ya mezani: +255 22 2861887

Simu ya mkononi: +255 715 200940 na +255 200940, +255 754200940

Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.topcomprinters.com