EFTA Ltd inaboresha maisha ya Watanzania kupitia mikopo ya mashine isiyokuwa na dhamana


EFTA Ltd inaboresha maisha ya Watanzania kupitia mikopo ya mashine isiyokuwa na dhamana

EFTA Ltd ni kampuni iliyonzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali na wakulima ambao walionekana kutokuweza kukopesheka na mabenki pamoja na taasisi zingine za kifedha. EFTA Ltd inashughulika na kutoa mikopo ya mashine za kila aina bila dhamana yoyote

Je wewe ni mkulima au mjasiriamali mwenye ndoto ya kuanzisha au kukuza biashara yako? Kama jibu ni ndiyo, ni lazima utakuwa umewaza jinsi utakavyo pata nyenzo za kukuwezsha kutekeleza jambo hilo.

Kwanza, jiulize ili ujue unahitaji nini haswa katika kulitekeleza hilo. Unataka kununua mashine, kukarabati vifaa, kuongeza malighafi au kuongeza uzalishaji? na kufanya hivi utahitaji mkopo kiasi gani na ni muda gani ambao kwa mtazamo wako utatosha kuulipa mkopo huo na pia kulingana na mapato yako unaweza kulipa kiasi gani katika kila awamu?

Majibu ya maswali haya yanapatikana EFTA Ltd. Hii ni kampuni iliyodhamiria kuwanyanyua wakulima na wajasiriamali kwa kuwapatia mikopo ya mashine mbalimbali isiyokuwa na dhamana yoyote.

Meneja Masoko wa EFTA Ltd, Peter Temu anasema, kampuni hiyo imedhamiria kusaidia dhamira ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na katika kulifanikisha hilo wameamua kutoa mikopo ya mashine bila dhamana.

Tuelezee historia ya kampuni ya EFTA Ltdna shughuli zake

“EFTA Ltd ni kampuni iliyonzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali na wakulima ambao walionekana kutokuweza kukopesheka na mabenki pamoja na taasisi zingine za kifedha. EFTA Ltd inashughulika na kutoa mikopo ya mashine za kila aina bila dhamana yoyote,” alisema Temu.

Anaeleza kuwa, “hatukopeshi fedha taslimu bali tunakopesha mashine tu na tunalipia mashine ya mteja kwa muuzaji kisha mteja anapelekewa mashine yake na baada ya hapo mteja atarejesha mkopo wake kwa utaratibu wa rejesho la kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu.”

Soko la biashara ya ukopeshaji wa mashine na vifaa hasa zana za uzalishaji kwa hapa Tanzania likoje? Na kwa namna gani mmejipanga kuwa kinara wa biashara hiyo?

Temu anasema, soko la mikopo ya mashine za kila aina hapa Tanzania liko vizuri japo lilianza na changamoto nyingi haswa ukizingatia kuwa watanzania wengi wana utamaduni wakuogopa kukopa wakiamini kuwa watafilisiwa kwa kushindwa kulipa mkopo jambo ambalo sio kweli. Pia wengine walikuwa hawaamini kuwa wanaweza kukopeshwa mashine bila kuweka dhamana kitu chochote.

“EFTA Ltd kwa sasa tumeanzisha huduma mpya yakuinua sekta ya utalii, ujenzi na usafirishaji kwa kuwakopesha magari ya kusafirisha watalii, mabasi ya kusafirishia abiria ya kila aina, malori ya kusafirishia mizigo, magari na mitambo inayotumika katika shughuli za ujezi. Mikopo yetu yote haina dhamana, kwa kuwa dhamana kwetu ni ile mashine tunayokukopesha.” Alisema Temu

Na kuongeza kuwa, “hivyo kwa kuanzishwa kwa huduma hizi mpya zinafanya EFTA iweze kupanuka zaidi na kuweza kuhudumia wahitaji wengi wa mashine za kila aina na hivyo kuwezesha juhudi za serikali katika kuinua uchumi wa viwanda.”

Mnafanya nini cha tofauti kuhakikisha wateja wenu wanarudi kila wakati?

“EFTA tumejidhatiti sana katika kuboresha huduma zetu ambapo kuanzia mteja anaanza kuulizia huduma zetu iwe ni kwa njia ya simu, kwenye mitandao ya kijamii au kwa kutembelea ofisi mojawapo kati ya ofisi zetu zilizopo katika matawi saba nchini.

Wafanyakazi wa EFTA wamefundishwa huduma kwa mteja na hivyo huwahudumia vyema kuanzia mteja anapoingia hadi anapotoka,” alieleza Temu.

“Pia tuna utaratibu wa kuwatembelea wateja wetu kila baada ya miezi miwili kujua changamoto zinazowakabili na kushauria ili kufanikisha malengo yao waliojiwekea na kuona namna nzuri ya kuzitatua kwa lengo la kuhakikisha kuwa wateja wetu wanafanikisha kile walichokusudia kukifanya,” alieleza Temu.

Kwa namna gani biashara ya ukopeshaji wa mashine inaweza kuwa muhimili wa kunyanyua kampuni ndogo na za kati?

Temu anafafanua kuwa, mikopo ya mashine na hususani ile inayotolewa na kampuni ya EFTA Ltd inawezesha na imewezesha wafanyabiashara wa chini, wa kati na hata wale wakubwa kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa mashine na vifaa vya kuwawezesha kukuza biashara zao, kuongeza uzalishaji, kuanzisha viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa na huduma wanazozizalisha.

“Kabla ya kuanzishwa EFTA wengi walikuwa wanakwama kupata mikopo ya kukuza biashara zao kwa kuwa vigezo na masharti ya mabenki na taasisi zingine za fedha ni ngumu kutekelezwa na walio wengi mfano kuwa na dhamana, kama hati ya nyumba, hiki ni kikwazo kikubwa kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania mali zao hazijarasimishwa hivyo hawawezi kuzitumia kama dhamana,” alisema Temu.

Nini kifanyike ili kuinua sekta hii ya uwezeshaji wajasiriamali na wakulima?

“Elimu kwa wajasiriamali na wakulima kuhusu uanzishaji, uendeshaji wa biashara, usimamizi na faida ya kuzalisha badala yakutegemea bidhaa zinazoingizwa nchini na wazalishaji wa nje na sisi kuwa kama madalali wa bidhaa hizo badala yakuzalisha zetu na kuziuza wenyewe inatakiwa kutolewa kwa wingi,” alisema.

Mnafanya jitihada ili kuufahamisha umma umuhimu wa biashara ya ukoukopeshaji wamashine?

Anasema kuwa, EFTA Ltd inajitahidi sana kufanya jitihada za kujitangaza kuhakikisha kuwa kila mtanzania anafahamu na kunufaika na hii fursa ya mikopo ya mashine bila dhamana.

“Huwa tunahudhuria maonesho ya Sabasaba, Nanenane kila kanda, kuandaa mikutano ya wadau na wafanyabiashara, kutangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mitandao ya kijamii, kuandaa maonesho kwa kushirikiana na washirika na wasambazaji mbalimbali wa mashine na kushirikiana na taasisi mbalimbali kama SIDO, TCCIA, TIC,CTI,TPSF nk,” alisema Temu.

Kilimo ni moja ya sekta tegemezi katika kuinua uchumi wa nchi. Je mmewatazamaje wakulima katika huduma zenu?

“EFTA imewawezesha wakulima wengi katika mikoa zaidi ya 18 kupata zana bora za kilimo kama vile trekta, vifaa vya umwagiliaji, vifaa vya kuchimbia visima, mashine za kusindikia mazao nk. Kuwezesha wakulima hawa kumesaidia kuongeza tija, kuongeza thamani katika kile wanachokizalisha na kuweza kuinuka kiuchumi,” alisema Temu.

Ni hatua gani huchukuliwa kwa mteja atakayekiuka makubaliano ya mkopo?

“Tunakuwa na makubaliano baina ya mteja na kampuni na huwa tunasaini mkataba ambao unabeba taratibu zote za kukopeshwa haswa ukizingatia kuwa mkopaji haweki dhamana kitu chake chochote. Pale anapokua ameshindwa kulipa huwa tunaichukuwa ile mashine tuliyompa kwa kuwa ndiyo dhamana yenyewe na hakuna mali wala kitu chake kingine kitakachochukuliwa,” alisema Temu.

Ni mafanikio gani ambayo mmeyapata tangu kuanza kwa shughuli zenu miaka 16 iliyopita?

Temu anaeleza kuwa, “Mafanikio makubwa tunayojivunia ni kuweza kuwafanya watanzania wengi waliokuwa hawawezi kukopesheka kuweza kupata mkopo na kuweza kuboresha maisha yao na kukuza uchumi wa nchi, mfano wameweza kuongeza mitaji, kusomesha watoto, kupata faida kubwa kwa kulima kilimo cha kisasa, kukuza biashara, kuongeza ajira kwa watanzania, kuongeza uzalishaji, kuongeza thamani ya bidhaa za ndani na kuwezesha uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya kuunga mkono dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.”

Mnajiona wapi baada ya miaka mitano kama kampuni?

“Kwa sasa tumeweza kuwafikia watanzania ndani ya mikoa 23 na tunatarajia kuwa ndani ya miaka mitano tutaweza kuifikia mikoa iliyobaki na hivyo kufanikisha dhamira yetu ya kufikisha fursa hii ya mikopo ya mashine bila dhamana kwa watanzania wote ili wajikomboe, wakuze biashara zao bila kulazimika kuwa na dhamana au masharti magumu pale wanapohitaji kukopa,” alibainisha Temu.

Mnatoa wito gani kwa watanzania?

“Tunapenda kutoa wito kwa watanzania kuwa, hii ni fursa ya kipekee ya kuwawezesha kupata mikopo ya mashine bila dhamana na kwa mkopo wa muda mrefu kimarejesho.

Pia kwa wale ambao bado hawajajua kuwa tumeanza kutoa mikopo katika sekta ya usafirishaji ikihusisha mabasi makubwa ya mikoani, daladala, malori makubwa na magari aina zote ya kufanyia kazi,” alisema Temu.

Anasema, sekta ya utalii tunakopesha magari ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuwasafirisha na kuwahudumia watalii kama njia ya kuinua uchumi kupitia utalii na kwa wale wa sekta ya ujezi hatujawasahau kwani wanaweza kupata magreda, makatapila, na vifaa vya aina vyote vinavyotumika katika ujezi.

Karibuni EFTA Makao Makuu Moshi, Matawi, Moshi, Arusha, Mwanza, Mbeya Bukoba, Morogoro, Dar esa Salaam na Dodoma.