Mgodi wa Geita wapokea tuzo ya mshindi wa jumla wa usalama kimataifa 2019

Muktasari:

Usalama ni kipaumbele chetu cha kwanza na kwa mwaka wote tumeendelea kuboresha usalama katika utendaji wa shughuli zetu kote duniani. Natoa shukrani na pongezi za dhati kwa kila mmoja wetu kwa mchango alioutoa na kuwezesha kufikia kiwango hiki cha ufanisi.

Usalama ni kipaumbele chetu cha kwanza na kwa mwaka wote tumeendelea kuboresha usalama katika utendaji wa shughuli zetu kote duniani. Natoa shukrani na pongezi za dhati kwa kila mmoja wetu kwa mchango alioutoa na kuwezesha kufikia kiwango hiki cha ufanisi.

Tunapofanya kazi ili kufikia lengo letu la 2030 la kufanya kazi kwenye maeneo ambayo hayana kuumia wala madhara, hatuwezi kamwe kujibweteka, lakini kuna mafanikio ambayo tunapaswa kujivunia na kusherehekea.

Hivyo, ninayo fahari kubwa kuwapongeza wafanyakazi, wakandarasi, na menejimenti ya Mgodi wa Geita, kupokea tuzo ya Mshindi wa Jumla wa Usalama Kimataifa kwa mwaka 2019, kwa mfano wa kuziishi kwa vitendo tunu za AngloGold Ashanti. Mafanikio hayo bora ni pamoja na:

• Hakuna vifo vilivyotokea maeneo ya kazi kwa miaka saba iliyopita.

• Hakuna majeraha yaliyotokea na kusababisha mhusika kushindwa kufika kazini kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

• Uboreshaji na utendaji bora mwaka baada ya mwaka kwa asilimia 85 katika kiwango cha majeraha – hii ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na mgodi mwingine.

• Kukidhi vigezo kwa 92% kwa Viwango vya Tathmini ya Mifumo ya Usimamiaji Usalama.

• Kufanikiwa kufunga uchunguzi na utatuzi wa matukio ya usala-ma kazini kwa 93%

• Kutambuliwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA) kuwa kampuni kinara nchini Tanzania kwa usimamizi wa usalama na afya. GGML ilishika nafasi ya kwanza kwa utendaji wa usalama na afya kazini kati ya makampuni 40 yalishindanishwa katika tuzo hiyo kwa mwaka 2019.

• Mgodi wa kwanza unaomilikiwa na AngloGold Ashanti katika Ukanda wa Afrika kuthibitishwa shirkia la kimataifa la ubora ISO 45001: 2018. Tukitambua ugumu uliopo (kutokana na ufanisi wa kip-ekee katika nyanja tofautitofauti), mimi na wenzangu tunatoa pongezi za dhati kwa:

• Kampuni nzima katika kuboresha kiwango cha majeruhi kwa 31% nyingine mwaka baa-da ya mwaka, kufikia kiwango cha chini kabisa katika kumbukumbu zetu na kwa kukamilisha mwaka wa bila ajali iliyosababisha kifo, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza.

• Mgodi wa Mponeng kwa kufanikisha maboresho makubwa ya utendaji kazi kwa usalama ambayo yametoa viwango vyake bora vya kuepusha majeraha (AIFR, LTIFR na SIFR), hatua ya kuzuia kufanya kazi mwaka mzima bila ajali iliyosababisha kifo na mizunguko (shift) milioni mbili bila ajali.

• Mgodi wa Dhahabu wa Tropicana, mshindi wa pili katika Tuzo ya Usalama Kitaifa, kwa maboresho waliyofanya katika kipndi cha mwaka 2019 katika nyanja zifuatazo:

Viwango vya majeruhi (AIFR) na 57% (kiwango bora kabisa kuwahi kufikiwa), Viwango vya majeraha yanayoweza kusababisha mtumishi kushindwa kuhudhuria kazini (LTIFR) kwa 91% (bora kabisa) na Viwango vyote vya Kujeruhiwa (AIFR) kwa 57% (kiwango cha chini kabisa kuwahi kufikiwa), Kiwango cha kutokuwa kwa majeraha (LTIFR) na 91% (kiwango bora kabisa kuwahi kufikiwa).

Pia Tropicana wali-fanikiwa kufika fainali katika Tuzo za Ubora wa Kazi, afya na Usal-ama kwa 2019 katika migodi iliyo Australia ya Magharibi.

Mradi wa Obuasi kwa kurekodi kutimiza masaa milioni moja ya utendaji kazi bila kupata ajali inayoweza kusababisha mfanyakazi kushindwa kuhudhuria kazini.

Kwa kuzingatia ugumu na wingi wa masuala yaliyohitaji kufanyiwa kazi katika mradi huo, ikiwa ni pamoja kuondoa, kukarabati na kufungua upya miundo mbinu ya mgodi wa zamani, ufanisi huu katika usalama kazini unastahili kutambuliwa kwa upekee wake.

Tuzo ya Kuondosha kabi-sa Vihatarishi (Zero HARM) inatambua wale ambao wamechukua hatua ya ubunifu na kuondoa au kudhibiti hatari.

Waliopata tuzo hiyo kwa mwaka wa 2019 ni:

Cuiaba: Kwa Mpango wake wa kudhibiti kiwango cha uchovu kwa kutumia teknolojia inayochambua kupitia sura ya mfanyakazi.

Geita: Kwa mpango kutenganisha mitambo/magari kuepusha muingiliano

Iduapriem kwa mpango wa kudhibiti uchovu kazini ujulikanao kama SmartCap.

Serra Grande kwa mpango wa kutenga na kudhibiti maeneo unakofanyika uchorangaji miamba na kifaa kipya cha kubadilisha mkanda wa kusafirishia kifusi kwenye kinu cha uchenjuliaji dhahabu.

Sun Rise Dam kwa mpango wa uchorong-aji wa miamba unaotumia kamera zilizoko mbali na eneo husika.

Tropicana kwa mpango wa uchorongaji miamba unaojiendesha wenyewe na pia programu ya WWTP inayotambua kiwango cha kilevi au madawa mwilini.

Pongezi kubwa kwa mafanikio hayo na tunatoa changamoto ya kuongezajuhudi ili tuweze kufanikiwa zaidi katika nia yetu ya kuchimba bila kusababisha madhara. Japokuwa ni muhimu kutambua mafanikio na hatua muhimu katika safari yetu ya “kutokuwa na madhara eneo la kazi” ni muhimu pia kuwa na umakini ili tusipoteze umakini kutokana na mafanikio tuliyoyapata.

Ninatoa changamoto kwa kila mmoja wetu kutumia mafanikio haya, kwa kuendelea kuboresha wakati wote, na kuleta tofauti kila siku. Binafsi ninajivunia sana mafanikio ya pamoja ya AngloGold Ashanti na nina uhakika kuwa kwa pamoja tunaweza, na tutafanikiwa kwa juhudi zetu.

Asante kwa kujitoa mlikoonyesha kwa kipindi chote na kwa mara nyingine natoa pongezi kwenu nyote.