CCM kupinga matokeo majimbo manne

Wednesday October 28 2015

Msemaji wa Kambi ya Kampeni ya CCM, January

Msemaji wa Kambi ya Kampeni ya CCM, January Makamba . 

By Beatrice Moses

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimelalamikia utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo uliofanywa kwenye baadhi ya majimbo, hivyo kimekusudia kukata rufaa kupinga matokeo yaliyotangazwa kwenye majimbo manne ambayo ni Mikumi, Kawe, Iringa Mjini na Ndanda.

Msemaji wa Kambi ya Kampeni ya CCM, January Makamba akizungumza leo  amesema ingawa kina maeneo mengine walikooteza viti vya ubunge wameshindwa kihalali lakini hayo yalikuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi. 

"Wasimamizi katika majibu haya wamevuruga uchaguzi kutokana na utata uliojitokeza wakati wa zoezi la  kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo IPO kisheria,kwenye baadhi ya majimbo ikiwamo Yamagana wapinzani walipewa fursa hiyo,"

 

Amesema hatua ya kwenda mahakamani inachukuliwa ilin kujiridhisha kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa." Bado tunaendelea kukusanya taarifa ya maeneo mengine walikopoteza viti vya ili kuona kama kulikuwa na ukikwaji uliadilisha matakwa ya wapiga kura wengi,"alisisitiza.

Makamba ametumia nafasi hiyo pia kuwamepongeza wa  ushindi waliopata Freeman  Mbowe na James Mbatia ambapo amekiri kwamba walizidiwa na wananchi wametumia utashi wao katika kupiga kura. 

Advertisement

"Tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza vitivya ubunge tumepoteza kihalali hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi na tunajitathimini kama chama ili tubaini makosa na kujirekebisha," alisema.

Wamelaani pia vitendo vya vurugu ikiwamo kuharibu mali za chama na Serikali uliofanywa na watu wanaotajwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya ukawa, ikiwamo kuchoma moto ofisi za CCM katika Wilaya ya Mbozi na Mahakama.

Amesema kinachoonekana sasa ni baadhi ya wagombea walioshindwa kuacha kufuata sheria badala yake  kuendeleza siasa  za uchaguzi kwenye miutaa kwa kuhamasisha vurugu na maandamano jambo ambapo halifai kwa kuwa a man I ni muhimu zaidi kuliko hitaji la  madaraka ya kulazimisha.

Amemtaka Mgombea wa urais Kupitia Chadema Edward Lowassa kujiandaa kisaikolojia kumpongeza Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli hasa kutokana na matokeo  yanayoendelea kutangazwa kuonyesha anamzidi kwa kura nyingi. 

"Tunaomba ifike pahala sasa katika kujenga demokrasia  na kuimarisha taifa tuanze utamaduni mpya anayeshindwa anyanue siku na kumpongeza aliyeshinda , nafasi ya mwidhjo anayo mgombea  wa Ukawa kuendelea kujijengea heshimakwa kumpongeza Dk Magufuli siku atakapotangazwa mshindi," alisema Makamba.

Makamba pia amesema CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi  ambapo wamefarijika kwamba katibu wrote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi uliuwa wa haki na huru  na umefanyika kwa uwazi na amani , ingawa kulikuwa na changamoto ndogo zilizojitokeza katika baadhibya maeneo kiasi zisingeweza kubadilishga matokeo yanayotangazwa sasa.