Ushiriki wa CRDB kukuza uchumi, biashara na uwekezaji nchini

Kamishna wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dk Charles Mwamaja (katikati) akiwasili katika hafl a ya kutangaza matokeo ya hatifungani ya kijani ya Benki ya CRDB ‘Kijani Bond” iliyofanyika hoteli ya Johari Rotana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na Ofi sa Mkuu wa Fedha wa benki hio, Fredrick Nshekanabo.


Hesabu za mwaka uliopita (2023) zilionyesha kuwa jumla ya rasilimali za benki ya CRDB zimeongezeka kwa asilimia 14 kutoka Sh11.6 trilioni mwaka 2022 hadi Sh13 trilioni, huku amana za wateja zikiongezeka kwa asilimia 8 hadi Sh8.9 trilioni.

Wakati huohuo, kitabu cha mikopo cha benki hiyo kilishuhudia ukuaji mkubwa wa asilimia 23, kufi kia jumla ya Sh8.5 trilioni.

Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Benki ya CRDB wakipata maelezo juu ya uzalishaji wa sukari wakati walipotembelea Kiwanda cha Mtibwa Sugar.


Wakati wa kutangaza hesabu hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, alisema “matokeo haya yanaonyesha dhamira yao katika kujenga benki imara na kutoa thamani endelevu kwa wadau wetu”.

Nsekela alisema kadiri sekta ya fedha inavyozidi kubadilika, CRDB iko tayari kushikilia dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuimarisha utendaji wake, kuhakikisha thamani ya muda mrefu kwa wadau wake.

“Benki ya CRDB imejipanga vyema kwa siku zijazo, na tunazatiti kutoa thamani endelevu kwa wateja wetu, wanahisa na jamii tunazohudumia. Mtazamo wetu katika ukuaji endelevu utaendelea kuongoza maamuzi yetu ya kimkakati katika miaka ijayo.” Fredrick Nshekanabo, Ofisa Mkuu wa Fedha, yeye alisema:

“Mtazamo wetu katika kuimarisha huduma za mikopo unadhihirika katika uwiano wa mikopo chechefu wa asilimia 2.8”.

Alisema katika mwaka 2023 uwiano wa gharama na mapato ya Benki ya CRDB uliendelea kuwa katika kiwango cha udhibiti pamoja kwa kufi kia asilimia 49.5 pamoja na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji iliyosababishwa na kuzorota kwa mazingira ya uchumi mpana kimataifa.”


Ushiriki wa CRDB katika miradi ya kimkakati

Benki ya CRDB imeweza kushiriki kikamilifu katika kuwawezesha makandarasi wa ujenzi wa miradi ifuatayo ya kimkakati. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Umeme wa Gesi –Kinyerezi (awamu ya I na ya II) – MW 150. Pia usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA.

Vilevile CRDB inashiriki katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere Hydro – MW 2,115, upanuzi wa viwanja vya ndege na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar-Morogoro-Dodoma-Tabora hadi Mwanza.

Kadhalika Benki hiyo inafanikisha ujenzi wa Barabara Kuu zinazounganisha mikoa na wilaya kupitia makandarasi mbalimbali wanaopewa kazi za ujenzi wa miundombinu hiyo, lakini pia ujenzi wa miundombinu ya afya, elimu na usambazaji wa huduma muhimu ya maji mijini na vijijini kupitia mamlaka za maji.

Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kufufua Ushirika kwa kutoa wataalamu wanaosaidia kwenye shughuli za uendeshaji wa taasisi za ushirika na kuongeza mitaji ili kuhuisha na kuujengaUshirika imara na imeweza kutoa mtaji wa Sh3.2 bilioni kwa Tandahimba Community Bank (TACOBA)

Pia Benki ya CRDB imetoa Sh7.0 bilioni kwa Kilimanjaro Cooperative Bank Ltd (KCBL), hivyo kuwezesha Benki hizi za Ushirika kupata mtaji unaofi kia kiasi cha Sh10.2 bilioni na kuweza kujiendesha kwa faida na tija zaidi.


Uchumi wa Buluu

Benki ya CRDB ikishirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaendelea kuwawezesha wajasiriamali wachanga, wa kati na wakubwa walioko Unguja na Pemba kupitia mpango maalumu wa INUKA na UCHUMI WA BULUU kwa kutoa mikopo ili waweze kuongeza mitaji yao kwenye shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na biashara.

Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa CRDB, Maregesi Shaaban anasema katika mpango huu, zaidi ya Sh60 bilioni zinaendelea kutolewa kwa wanufaika wasiopungua elfu hamsini walioko Zanzibar ili waweze kuongeza mitaji kwenye miradi yao na kuongeza tija kwenye uchumi wa nchi.

Vilevile CRDB inashirikiana na Wizara ya Mifugo katika kuendeleza sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Kwa mwaka huu wa 2024, CRDB imetoa mikopo inayofi kia Sh62.4 bilioni kwenye sekta ya mifugo na uvuvi.


Kuhusu Uwekezaji Day

Kangamano la uwekezaji ambalo limekuwa likifanywa na CRDB ni utamaduni wa benki hiyo uliobuniwa ili kuweza kuwa karibu zaidi na wawekezaji kwenye sekta zote za uchumi.

Lengo kuu likiwa ni kuunga juhudi za Serikali kuchagiza maendeleo jumuishi, kufungua fursa zilizopo ndani ya nchi kwa kuuelewesha umma na dunia nzima kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, lakini pia Watanzania kufahamishwa kuhusu fursa zilizopo nje ya nchi.

Benki ya CRDB imekuwa ikitumia jukwaa hilo kuonyesha utayari wake wa kuungana na wawekezaji ili waweze kupata huduma muhimu za kibenki, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mitaji wezeshi kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.