Megan atuhumiwa kwa unyanyasaji wa kihisia 

Muktasari:

  • Emilio kwenye shitaka hilo amedai kuwa Juni mwaka 2020 Megan alimlazimisha amtazame akiwa anafanya ngono katika gari kisha baada ya tukio hilo alimuonya kuwa asiseme chochote alichoshuhudia ili kulinda heshima ya rapa huyo.

Mwanamuziki wa Marekani, Megan Thee amefunguliwa mashitaka na aliyekuwa mpiga picha wake Emilio Garcia kwa unyanyasaji wa kihisia na mazingira magumu ya kazi.

Emilio kwenye shitaka hilo amedai kuwa Juni mwaka 2020 Megan alimlazimisha amtazame akiwa anafanya ngono katika gari kisha baada ya tukio hilo alimuonya kuwa asiseme chochote alichoshuhudia ili kulinda heshima ya rapa huyo.

Kwa upande wa Megan mwenye umri wa miaka 29 bado hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo zinazo mkabili.

Hata hivyo mwaka huu Megan aliuanza kwa kutikisa vichwa vya habari baada ya kuingia kwenye bifu na Nicki Minaj, alipoachia wimbo wake ‘Hiss’ uliodaiwa kumchana mume wa Nicki, Kenneth Petty, na kupelekea Nicki kujibu kupitia wimbo wake wa ‘Big Fotty’.

Mbali na hayo mwanamuziki huyo wa kimataifa amewahi kufanya ngoma kama vile Sweetest Pie, Hiss, Sg, Not My Faulit, Cognac Queen.

Ikimbukwe kuwa mwaka jana mwanamuziki huyo alimshitaki Tory Lanez kwa kumpiga risasi mguuni mwaka 2020 ambapo mpaka sasa rapa huyo anatumikia kigungo cha miaka 10 gerezani.