Mwanasheria  wa Diddy awaka matumizi ya nguvu kumkamata mteja wake

Muktasari:

  • Msako huo ulifanywa baada ya msanii huyo kuhusishwa na madai ya biashara ya ngono yanayomkabili msanii huyo. Hivyo basi kwa mujibu wa tovuti ya Business Insider, imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka kwa  mwanasheria wa Diddy aitwaye Aaron Dyer ikieleza kuwa msanii huyo hakuwa na hatia hivyo msako uliofanywa kwenye makazi yake ulikuwa ni utumiaji mbaya wa nguvu za kijeshi huku akitaja vitendo hivyo kama chuki na uhasama.

Uongozi wa  Diddy, umetoa taarifa juu ya msako uliofanywa Jumatatu, Machi 25 na  Mawakala wa Usalama wa Taifa kwenye nyumba mbili za msanii huyo ikiwemo ya Los Angeles na Miami, kuwa ulikuwa ni matumizi mabaya ya nguvu.

Msako huo ulifanywa baada ya msanii huyo kuhusishwa na madai ya biashara ya ngono yanayomkabili msanii huyo. Hivyo basi kwa mujibu wa tovuti ya Business Insider, imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka kwa  mwanasheria wa Diddy aitwaye Aaron Dyer ikieleza kuwa msanii huyo hakuwa na hatia hivyo msako uliofanywa kwenye makazi yake ulikuwa ni utumiaji mbaya wa nguvu za kijeshi huku akitaja vitendo hivyo kama chuki na uhasama.


                     

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa kilichofanyika ni uhasama kupita kiasi,ulioneshwa na mamlaka hasa jinsi watoto na wafanyakazi wake walivyofanyiwa, hata hivyo taarifa hiyo imeeleza Licha ya uvumi wa vyombo vya habari, si Bw. Combs wala mtu yeyote wa familia yake ambaye amekamatwa na uwezo wao wa kusafiri haujazuiliwa kwa njia yoyote ile.

Mbali  na taarifa hiyo ya mwanasheria  vyombo mbalimbali nchini humo vimeripoti kuwa Diddy ameuza hisa zake zote za kampuni yake ya Revolt TV kwa mtu asiyejulikana.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu mwaka jana 2023, kati ya waliowahi kumtuhumu ni aliyekuwa mpenzi wake Cassie