Siku kama ya leo Smith alimchapa kofi Chris Rock

Muktasari:

  • Kichapo hicho kilikuja baada ya Chris kumtania aliyekuwa mke wa Will, Jada Smith kuhusiana na kichwa chake kutoota nywele, jambo ambalo Smith hakufurahishwa nalo kutokana na kuwa na ugonjwa ambao unamsumbua

Tarehe na mwezi kama wa leo miaka miwili iliyopita dunia ilishuhudia kile kilichoitwa utovu wa nidhamu baada ya mwigizaji Will Smith kumchapa kofi mchekeshaji ambaye pia ni mwigizaji Chris Rock, mbele ya hadhara katika usiku wa Tuzo za Oscar mwaka 2022.

Kichapo hicho kilikuja baada ya Chris kumtania aliyekuwa mke wa Will, Jada Smith kuhusiana na kichwa chake kutoota nywele, jambo ambalo Smith hakufurahishwa nalo kutokana na kuwa na ugonjwa ambao unamsumbua.

Aliyekuwa mke wa Will Smith, Jada anasumbuliwa na ugonjwa uitwao ‘Alopecia Areata’, ambao hauna tiba husababishwa na mfumo wa kinga kushambulia follicles ya nywele na kupelekea mtu kutoota nywele.

Ikumbukwe kuwa Oktoba mwaka jana Jada Smith alishika vichwa vya habari baada ya kudai kuwa yeye na Will Smith walitengana miaka 7 iliyopita licha ya kuwa wanaishi pamoja.