Mbaroni akidaiwa kumwingilia  kuku hadi kufa

New Content Item (1)

Rogers Sunday (wapili kulia) anayedaiwa kubaka kuku akitolewa ndani ya nyumba ya dada yake kwaajili ya kupelekwa kituo cha polisi.

Muktasari:

  • Chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na kumchunguza mtuhumiwa afya yake ya akili.

Mwanza. Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni ndivyo unavyoweza kusema baada ya Rogers Sunday (41) mkazi wa Kitongoji cha Misungwi Kata ya Usagara mkoani Mwanza kutuhumiwa kumwingilia kuku hadi kufa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Aprili 15, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amedai kuwa Sunday alifanya tukio hilo Aprili 12, mwaka huu kwa lengo la kujiridhisha kimwili.

New Content Item (1)

Kuku anayedaiwa kubaka

“Tukio hilo limetendeka sebuleni nyumba kwa  dada wa mtuhumiwa na kushuhudiwa na mtoto wa kike wa dada yake huyo.

Chanzo cha tukio bado kinachunguzwa ikiwa ni pamoja na kumchunguza mtuhumiwa huyo afya yake ya akili,” amesema Mutafungwa.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Misungwi, Samson Madirisha amedai kuwa walipomuuliza mtuhumiwa huyo ambaye ni mpiga debe stendi ya mabasi Usagara sababu za kafanya kitendo hicho, alidai alizidiwa na hamu ya tendo la ndoa.

 “Kama kiongozi nilichukua jukumu la kutoa taarifa kituo cha Polisi ambao nao walifika na kuondoka na mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi," amesema mwenyekiti huyo.

Kamanda wa Sungusungu kata ya Usagara, Buhili Makubilo amesema kitendo hicho cha Sunday kinahatarisha usalama wa watoto katika eneo hilo, akiwataka wazazi wawe makini.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai  mtuhumiwa alimkamata kuku huyo ambaye alikuwa anataga, kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake na kuanza kumwingilia, alipomaliza haja zake alimtupa nje akiwa amekufa, huku sehemu zake za nyuma zikitoa damu.

Mmiliki wa kuku huyo, Doris Boazi amedai  taarifa za kuku wake aliyekuwa akitaga  kuingiliwa alizipata juzi saa sita mchana, baada ya kuuliza alipomuona katupwa.

Amesema kuku wake huyo ameacha mayai manne.