Mwili wa Gardner wawasili Rombo kwa maziko
Muktasari:
- Gardner alifariki dunia Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Rombo. Mamia ya waombolezaji wakiwemo waandishi wa habari, watangazaji, wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini wameungana na wananchi wa wilaya ya Rombo kumuaga aliyekuwa mtangazaji wa Clouds, Gardner Habash ambaye atazikwa leo kijijini kwao Kikelelwa, kata ya Tarakea Motamburu, wilayani hapa.
Mwili wa Gardner umewasili nyumbani kwao leo, Aprili 23, 2024 kwa ajili ya taratibu za maziko ambazo zitafanyika katika Kijiji Cha Kikelewa.
Gardner alifariki dunia Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Viongozi mbalimbali Serikali wanahudhuria mazishi hayo, akiwemo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.
Mwili baada ya kufikishwa nyumbani kwao na kuagwa na wanafamilia utapelekwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Kikelelwa kwa taratibu za kuaga na kisha kurudishwa nyumbani kwa ajili ya maziko.