Serikali yaomba Sh16.58 bilioni kununua magari ya Ma-RC

Muktasari:

  • Serikali imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh16.58 bilioni kwa ajili ya magari ya mikoa 81 ya ofisi za wakuu wa mikoa huku 74 yakielekezwa kwa wakuu wa wilaya.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angella Kairuki ameliomba Bunge liwaidhinishie Sh16.58 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 kwa ajili ya ofisi za wakuu wa mikoa.

Kairuki ameliomba Bunge leo Ijumaa Aprili 14,2023 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Tamisemi kwa mwaka 2023/2024.

Amesema katika mwaka huo Ofisi ya Rais -Tamisemi imetengewa Sh16.58 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika ofisi za wakuu wa mikoa.

Amefafanua kuwa kati ya magari hayo, magari matano ni ya wakuu wa mikoa, magari mawili ni ya makatibu tawala wa mikoa na magari 74 ni ya wakuu wa wilaya.