Kwa nini uwekezaji sekta ya kilimo ni muhimu

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO, Revocatus Kimario wakisaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitatu kuwawezesha zaidi ya wahitimu 2,500 wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo

“Kama kilimo kikienda kombo, hakuna jambo lingine litapata nafasi ya kwenda vizuri,” alisema raia wa India, Mankombu Sambasivan Swaminathan, aliyekuwa mbobevu wa masuala ya kilimo.

Kwa namna nyingi unaweza kuhusisha nukuu hiyo na mambo mengi. Tanzania ina eneo lenye ukubwa wa hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo, ambapo hekta milioni 10.8, sawa na asilimia 24.5 ndizo zinazolimwa mazao mbalimbali.

Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa umwagiliaji wakati zinazotumika kwa umwagiliaji ni hekta 727,280.6, sawa na asilimia 2.5. Takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa asilimia 65.6, sawa na zaidi ya Watanzania milioni 40 maisha yao ya kila siku yanategemea sekta ya kilimo moja kwa moja.

(SUA) kushiriki mafunzo nje ya nchi. Wakishuhudia, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya SUGECO, Dk Anna Temu, Mwanasheria kutoka Benki ya CRDB, Gerald Mosha na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Changa CRDB Bank Foundation, Fadhil Bushagama.

Uzalishaji wa mazao ya chakula katika mwaka 2021/2022 ni tani milioni 17.14 ambapo mahitaji ya chakula kwa mwaka 2022/2023 ni tani milioni 15.05.

Hapa nchini sekta ya Kilimo huchangia karibu asilimia 30 ya Pato la Taifa; imetoa ajira kwa wananchi kwa wastani wa asilimia 65.6 na kuchangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda na asilimia 100 ya chakula nchini.

Ifikapo mwaka 2030, Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 79 na milioni 135 ifi kapo mwaka 2050, hata hivyo, kasi ya ongezeko la watu ni asilimia 3, huku wastani wa ukuaji wa sekta ya kilimo ukiwa ni asilimia 3.5.

Makadirio ya mahitaji ya chakula ifikapo mwaka 2030 yatakuwa tani milioni 20 na mwaka 2050 yatakuwa tani milioni 33.7.

Hali hii inaleta changamoto kwa nchi kuwa na mikakati ya uwekezaji ya muda mrefu kwenye Sekta ya Kilimo ili kuhakikisha utoshelevu wa chakula kwa miaka hiyo na ziada kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.

Taarifa ya Jukwa la Pili la Dakar 2 la mwaka 2023 inaonesha kuwa idadi ya watu duniani wanaokabiliwa na njaa ni milioni 828 na Bara la Afrika ni milioni 249.

Takwimu hizo zinaonyesha umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya kilimo hapa nchini sanjari na kutumia fursa ya biashara ya mazao ya chakula katika soko la Afrika ambayo inakadiriwa kufi kia Dola za Marekani Trilioni 1 ifi kapo mwaka 2030.

Hatua hiyo pia itafungua fursa zaidi za masoko na ajira katika mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula na kuondoa watu waliopo kwenye umasikini.

Kwa Tanzania, sekta ya Kilimo ni mwajiri mkuu wa nguvukazi ya taifa na mchangiaji mkuu wa kipato cha wananchi na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, miongoni mwa changamoto kubwa ambazo hutatiza ukuaji wa sekta ya kilimo, ukiachilia mbali utaalamu ni upatikanaji wa mtaji wa kuwekeza katika kilimo biashara.

Serikali imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ya kuunganisha sekta ya kilimo na sekta ya fedha na kupitia majukwaa mbalimbali imekuwa ikitoa hamasa kwa wakopeshaji kuelekeza fedha zao kwa wakulima ili kuongeza tija mashambani.

Benki ya CRDB ni miongoni mwa Taasisi zilizoitikia wito kwa Serikali kwa kufanya ukopeshaji mkubwa kwa wakulima katika miaka ya hivi karibuni.

Msimu wa kilimo unaoendelea wa 2023/2024 hadi kufi kia Februari mwaka huu, Benki ya CRDB imetoa jumla ya mikopo ya kilimo inayofi kia Sh1.41 trilioni.

Kiwango hicho cha mikopo ni sawa na asilimia 43 ya mikopo yote ya kilimo inayotolewa na mabenki hapa nchini, hatua inayoonyesha dhamira yao ya dhati kwa shughuli za kilimo.

Kinachofanywa na Benki ya CRDB ni kuunga mkono mpango wa Serikali na viongozi wa juu ambao matamanio yao ni kujenga Sekta ya Kilimo endelevu itakayowapa fursa vijana na wanawake kushiriki kwenye kilimo biashara.

Katika hotuba Wizara ya Kilimo, Serikali iliweka wazi shauku yake ya kuinua sekta ya kilimo, lengo ni kutoa fursa za ajira zenye staha na kipato cha uhakika ili kufi kia lengo la ukuaji wa Sekta ya Kilimo kwa asilimia 10 ifi kapo mwaka 2030.

“Tunataka kuondoa watu kwenye umasikini na kubaki endelevu kwa kuwekeza kwenye miradi ya muda mrefu, kwani uwekezaji kwenye kilimo siyo wa muda mfupi, bali matokeo yake ni ya muda mrefu,” alisema Waziri Hussein Bashe, wakati akiwasilisha hotuba yake Bungeni.

Kinachofanywa na Serikali sasa ni matokeo ya dhamira aliyoionyesha Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuingia madarakani. Katika hotuba yake ya kwanza Bungeni kama Rais wa Awamu ya sita, Rais Samia alitangaza kuwa atafanya mabadiliko katika sekta ya kilimo.

“Tutafanya mabadiliko katika sekta ya kilimo kwa lengo la kuongeza tija, kuwekeza katika kilimo cha biashara, mbegu bora na uwekezaji kwa taasisi za Serikali ili kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima,” alisema Rais Samia katika hotuba yake ya Aprili 22, 2021.

Rais Samia alisema Serikali anayoiongoza itazipa mtaji taasisi zinazojihusisha na kilimo na itahamasisha kuzalisha kwa tija, upatikanaji wa mbolea, masoko imara, ugani, uuzaji mazao nje ya nchi na upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima.

Benki ya CRDB imefanya nini kukuza uwekezaji katika kilimo

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka huu Bungeni, Waziri Bashe alizishukuru taasisi za kifedha ambazo kwa namna moja au nyingine zinaunga mkono maendeleo ya kilimo.

Miongoni mwake ni Benki ya CRDB ambayo alisema katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 imetoa mikopo ya kilimo yenye thamani ya Sh801 bilioni.

Bashe alisema kati ya mikopo hiyo, Sh494 bilioni zilipatiwa AMCOS 472 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kilimo, mifugo, misitu na uvuvi.

Katika mahojiano na gazeti hili, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara- Benki ya CRDB, Maregesi Shaaban anasema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, CRDB imetoa mikopo kwenye sekta ya kilimo inayofi kia jumla ya kiasi cha Sh3.92 trilioni.

Kati ya mikopo hiyo, Sh944.6 bilioni imeelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati yanayozalishwa na wakulima wadogowadogo waliojiunga kwenye vikundi vya uzalishaji, ikiwemo vyama vya ushirika (AMCOS) vinavyofi kia 541.

Anaeleza kuwa lengo la mikopo kwa vyama hivyo lilikuwa ni kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo (mikopo ya pembejeo, maghala, ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao, mikopo kwa ajili ya miradi ya ufugaji, uwekezaji kwenye misitu, uvuvi na biashara).

Maregesi anasema uwekezaji huo, umechagizwa zaidi na jitihada za Serikaliya awamu ya sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kusaidia upatikanaji wa mitaji nafuu kwa mabenki.

Anasema Benki ya CRDB ni miongoni mwa taasisi za fedha zinazonufaika na mitaji nafuu inayofi kia kiasi cha Sh37 bilioni kutoka Serikali Kuu kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Fedha ambazo hadi sasa zinaendelea kukopeshwa kwa wakulima wadogowadogo kwa riba isiyozidi asilimia tisa (9%) kwa mwaka. Uwezeshaji huu umesaidia kuwafi kia wakulima wengi zaidi, hivyo kuongeza tija ya uzalishaji kwenye sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na biashara,” anasema.

Anasema wakulima wadogowadogo kupitia kwenye vyama vya ushirika wanaunganishwa na mfumo madhubuti ya kifedha kupitia mtandao imara wa Benki ya CRDB.

“Mkulima anaweza kupata huduma za kifedha kupitia CRDB Wakala na simu za mkononi. Hivyo, kujijengea tabia za kujiwekea akiba kupitia huduma rahisi zinazopatikana hadi vijijini,” anasema Shaaban.

Anasema Benki hiyo inaendelea kuwawezesha vijana na wanawake ili kuongeza kasi ya uzalishaji kwenye sekta zote za kiuchumi, ikiwemo kilimo, misitu, biashara, viwanda, mifugo na uvuvi.

“Kupitia kampuni yetu tanzu ya CRDB Bank Foundation, tunaendelea kutoa mafunzo kwa vijana na wanawake ili waweze kusimamia miradi yao vema. Hadi sasa, Benki ya CRDB imekwishatoa mafunzo kwa vijana na wanawake zaidi ya 3, 000,000,” anasema.

Benki ya CRDB pia inatoa mitaji (start-up capital) ili kuyawezesha makundi haya muhimu kuendeleza miradi yao kupitia programu ya IMBEJU (seed capital).

Margesi anasema pamoja na utoaji wa mikopo, Benki ya CRDB inashirikiana na Wizara ya Kilimo, pia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa mafunzo yanayohusu elimu ya fedha (financial literacy) kwa vijana na wanawake waliopo kwenye programu maalumu ya mafunzo kwenye vituo atamizi vilivyopo kote nchini.

“Vijana hawa ni miongoni mwa Watanzania wachache waliopata bahati ya kujumuishwa kwenye sera ya uwezeshaji jumuishi kupitia mashamba nundu yenye lengo la kuwaandalia mazingira bora ya kuijenga kesho yao yenye tija zaidi (BBT),” anasema

Anaeleza kuwa kupitia ushirika huo jumla ya vijana wasiopungua 300 walipata mafunzo kupitia Benki ya CRDB kwenye vituo atamizi vilivyoko nchini kote.

“Huu ni mpango endelevu ya utoaji mafunzo kwa vijana, mafunzo haya yatatolewa miaka yote kwa vijana BBT ili kuwajengea uwezo wa kusimamia miradi yao”.

Maregesi anasema CRDB Bank Foundation imesaini mkataba wa Makubaliano (MoU) na Sokoine University Graduate Entrepreneurship Cooperative (SUGECO) ili kuwawezesha wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kufanikisha mafunzo kwa vitendo nje ya nchi.

Kupitia mkataba huo, CRDB Bank Foundation imetenga kiasi cha Sh67 bilioni kwa ajili ya programu hiyo na fedha hizo zitatolewa ndani ya miaka mitatu ya ushirikiano huu na SUGECO.

Mtaji wezeshi unatarajiwa kuwa kati ya Sh8.7 milioni 8.7 hadi Sh11.29 milioni.

Pamoja na uwezeshaji huo, CRDB Bank Foundation, SUGECO na USAID wameandaa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wahitimu hao pindi wanaporejea nchini ambapo eneo maalumu limeandaliwa kwa ajili ya kuwawezesha kuwekeza katika kilimo cha kisasa na chenye tija.

Kadhalika Maregesi anasema Benki ya CRDB inashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kupitia uwekezaji wa pamoja (joint fi nancing) na upatikanaji wa dhamana za kilimo kwa wateja wetu ili kuchagiza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

“Benki ya CRDB pia inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuongeza kasi ya uwezeshaji jumuishi kwenye sekta muhimu za kiuchumi,” anasema.

Anasema benki hiyo ina mpango wa utoaji mikopo maalumu ya zana bora za kilimo kwa kushirikiana wa wadau wa usambazaji wa ndani na nje.

“Uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Benki ya CRDB kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ni matokeo ya sera nzuri zinazowavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika kukuza fursa za uwekezaji nchini,” amesema


Mfumo wa usambazaji wa mbolea za ruzuku

Maregesi anasema Benki ya CRDB ikishirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imefanikiwa kubuni mfumo madhubuti wa kidijitali ili kurahisisha usambazaji wa mbolea za ruzuku.

“Wadau wote wanasajiliwa kupitia mfumo wa kidijitali (wanunuzi wakubwa, wasambazaji na wakulima ambao ndio wanufaika wa mwisho wa mbolea za ruzuku) na taarifa zao zinahifadhiwa kwenye mfumo kulingana na maeneo wanapotoka, ukubwa wa mashamba yao, aina ya mazao wanayolima na vyama au vikundi ambavyo wakulima wamejisajili,” anasema.

Mfumo huo unarahisisha upatikanaji wa mbolea zenye ubora kwa wakati na umepunguza na kuondoa tatizo la uingizaji wa mbolea zisizo na ubora.

Kadhalika mfumo huo unamtambua mtumiaji wa mwisho wa mbolea za ruzuku kwa alama za vidole na namba maalumu za usajili, hivyo kuiwezesha Serikali kufi kisha ruzuku ya pembejeo kwa wanufaika waliokusudiwa.