Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzimu wa kocha mzawa unavyoitesa Brazil

PUMZI Pict


KWA mara ya kwanza kwenye historia yao, Brazil itaongozwa na kocha wa kigeni kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu.


Mabingwa hao mara tano wa Dunia waliweka pembeni utamaduni wao wa kuajiri makocha wazawa tu, pale walipomtangaza Carlo Ancelotti, raia wa Italia, kuwa kocha wao. Ancelotti ambaye ni kocha mwenye uzoefu akifundisha timu kubwa za Ulaya na kushinda mataji yote makubwa, amepewa kibarua cha kuhakikisha heshima ya Brazil inarudi.


Tangu wachukue ubingwa 2002, Brazil wamekuwa wakipitia wakati mgumu ikiwemo aibu waliyopata nyumbani ya kipigo cha kihistoria cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani. Matarajio ni kwamba safari hii watabeba ubingwa, lakini hata hivyo kuna kizingiti kikubwa mbele yao.

Katika historia ya mashindano haya, hakuna timu iliyowahi kuwa bingwa ikiwa na kocha wa kigeni... na huu ndio mzimu unaoitesa Brazil.

Wanaamini wana kikosi kinachostahili kuwa bingwa. Wanaamini wana kocha anayetosha kuwapa ubingwa wa Dunia. Kinachowapa hofu ni hicho tu...mzimu wa kigeni! Ancelotti ni mmoja wa makocha 28 wa kigeni watakaokuwepo kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu huko Marekani, Canada na Mexico. Mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa yote yana makocha wazawa kasoro Brazil ambayo ni Argentina (Lionel Scaloni), Ufaransa (Didier Deschamps), Ujerumani (Julian Nagelsmann), Uholanzi (Ronald Koeman) na Hispania (Luis de la Fuente).

PUM 03

Hapa ndipo kichwa kinapowauma Brazil, je Don Carlo ataweza kuuvunja mwiko huu uliodumu kwa miaka yote? Katika historia ya mashindano hayo ni nchi nane tu ambazo zimewahi kuwa bingwa ambazo ni Brazil (mara tano), Italia (nne), Ujerumani (nne), Argentina (tatu), Uruguay (mbili),

Ufaransa (mbili), England na Hispania mara moja moja. Nchi zote hizo zilikuwa na makocha wazawa wakati zinachukua ubingwa.

Nchi tano katika hizo zimekuja na makocha wazawa, kasoro tatu. Brazil ina Mtaliano Carlo Ancelotti, Uruguay Muargentina Marcelo Bielsa na England inaye Mjerumani Thomas Tuchel. Mzimu wa kocha mzawa pia unawaandama wenyeji wawili kati ya watatu wa mashindano hayo, Marekani na Canada. Hawa wote wana makocha wa kigeni, kasoro Mexico pekee, ambapo Canada ina Mmarekani Jesse Marsch, Mexico ina Javier Aguirre (mzawa) na Marekani ina Muargetina Mauricio Pochettino

PUM 02

Katika orodha ya mabingwa wanane wa mashindano hayo, watano walibeba ubingwa walipoandaa. Ni wawili tu ambao hawakuwahi kuchukua ubingwa walipoandaa, wakachukua wakiwa nje ya ardhi yao. Brazil mara zote tano na Hispania. Kwa hiyo Canada na Marekani wanapewa nafasi angalau kidogo kutokana na uenyeji, lakini papo hapo inawakataa kutokana makocha wao wa kigeni.

Mataifa mengine yenye sifa ya kuwa mabingwa lakini yanahukumiwa na kukosa kocha mzawa ni Ureno linalofudishwa na Roberto Martinez (mgeni - Hispania), Ubelgiji — Rudi Garcia na Uturuki — Vincenzo Montella.

PUM 04

VIPI AFRIKA

Kombe la Dunia Qatar 2022 lilikuwa la mafanikio makubwa kwa Afrika. Japo hakuna timu iliyofika angalau robo fainali, lakini kwa mara ya kwanza kila timu ilionja ushindi angalau mmoja. Kwa kiasi kikubwa hiyo ilihisishwa na timu zote kuwa na makocha wazawa ambao ni

Walid Regragui (Morocco), Aliou Cisse (Senegal), Otto Addo (Ghana), Rigobert Song (Cameroon) na Jalel Kadri (Tunisia).

Safari hii Afrika imetoa timu 10 kwenye mashindano hayo, huku nne zikiwa na makocha wa kigeni ilhali sita zikiwa na makocha wazawa.

Zenye makocha wazawa ni Misri (Hossam Hassan), Morocco (Mohamed Ouahbi), Senegal (Pape Thiaw), Tunisia (Sabri Lamouchi), Ivory Coast (Emerse Fae) na Cape Verde (Bubista).

Nchi zenye makocha wa kigeni ni Afrika Kusini (Hugo Broos), Algeria (Vladimir Petkovic), DR Congo (Sebastien Desabre) na Ghana ina Carlos Queiroz. Acha tuone nini kitatokea. Mzimu wa makocha wa kigeni utaisha au utaendelea?