Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wa zamani wameheshimishwa

WAKONGWE Pict

Muktasari:

  • Siku anatua, pale katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, alikuwepo nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay ambaye pia miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kuwa kaimu Mkurugenzi wa Michezo.

KIJIWE kimeona idadi kubwa ya wachezaji wa zamani wakishiriki katika mapokezi ya nyota wa zamani wa England, Rio Ferdinand.

Siku anatua, pale katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, alikuwepo nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay ambaye pia miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kuwa kaimu Mkurugenzi wa Michezo.

Kesho wake wakati Ferdinand anaelekea Bungeni, Dodoma kulikuwa na kundi kubwa la wachezaji wa zamani ambao waliungana naye kumsindikiza na kushirikiana naye katika shughuli tofauti alizofanya.

Walikuwepo kina Bakari Malima, Edibily Lunyamila, Mayay, Mrisho Ngassa, Iddi Moshi, Mwinyi Kazimoto, George Masatu, Mohammed Mwameja na Mustafa Hozza.

Ni jambo jema kuona wizara inawathamini na kukumbuka mchango wa wachezaji wa zamani na kuwajumuisha katika matukio na hafla kubwa kama ilivyokuwa katika ziara ya Rio Ferdinand.

Kujumuishwa kwao kunaweza kuwa chachu ya kukihamasisha kizazi cha sasa kujituma na kujitolea zaidi katika soka ili kiweze ama kufikia au kuvuka zaidi ya pale walipofikia wenzao wa nyuma katika klabu na timu yetu ya taifa.

Mfano tukio kama la Mrisho Ngassa kumwonyesha Rio Ferdinand tukio la miaka mingi nyuma baina yao ni kumbukumbu nzuri ambayo ni chachu kubwa ya kuhamasisha wachezaji wa kisasa.

Tukio hilo ni lile la Ngassa kucheza dhidi ya Rio Fedinand katika mchezo wa kirafiki wakati wa maandalizi ya msimu mwaka 2011 uliozikutanisha Manchester United na Seattle Sounders.

Ngassa alienda Seattle Sounders kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na timu hiyo ndipo ikakutana na Manchester United.