Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Allarakhia amfariji Mnoga kuikosa League One

RAKIA Pict

Muktasari:

  • Ingawa safari ya kupanda daraja imeishia Wembley, msimu huu utaendelea kuwa wa kihistoria kwa soka la Tanzania baada ya wachezaji wawili wenye asili ya nchi hiyo, Mnoga na Allarakhia, kucheza katika mechi kubwa za Play-Off kwenye viwanja vikubwa vya England.

LICHA ya ndoto ya beki wa Kitanzania, Haji Mnoga ya kuipandisha Salford City kucheza League One kugonga mwamba, bado ameendelea kupata sapoti kutoka kwa nyota mwenzake wa Tanzania anayekipiga England, Tarryn Allarakhia.

Mnoga na Salford City walijikuta wakimaliza msimu kwa maumivu baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Notts County katika fainali ya Play-Off ya League Two iliyopigwa Uwanja wa Wembley, matokeo yaliyofuta matumaini ya kupanda daraja msimu huu.

Allarakhia ambaye hivi karibuni aliisaidia Rochdale kupanda daraja kutoka National League hadi League Two, alituma ujumbe wa kumpongeza na kumtia moyo Mnoga katika mitandao ya kijamii.

"Wachezaji wawili wa Tanzania kucheza Wembley ndani ya msimu mmoja," aliandika Allarakhia, akionyesha fahari yake kuona nyota wawili wenye asili ya Tanzania wakifika hatua kubwa katika soka la England.

RAKI 02

Kwa Allarakhia, msimu wa 2025/26 umebeba kumbukumbu nzuri baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Rochdale kilichorejea League Two kwa mechi za mtoano Play-Off.

Kwa upande wa Mnoga, licha ya kumaliza msimu bila tiketi ya kupanda daraja, amekuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia Salford City.

Beki huyo aliyewahi kupita akademi ya Portsmouth na kupata nafasi katika timu za vijana za England kabla ya kuamua kuitumikia Tanzania, ameonyesha kiwango kizuri kilichomfanya kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho katika kampeni ya msimu huu.

RAKI 01

Msimu huu Mnoga amecheza mechi 25 kwa dakika 1697 akitoa mchango wake katika safu ya ulinzi ya Salford City iliyokuwa ikisaka kurejea League One kwa mara ya kwanza tangu kushuka daraja.

Ingawa safari ya kupanda daraja imeishia Wembley, msimu huu utaendelea kuwa wa kihistoria kwa soka la Tanzania baada ya wachezaji wawili wenye asili ya nchi hiyo, Mnoga na Allarakhia, kucheza katika mechi kubwa za Play-Off kwenye viwanja vikubwa vya England.