Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtego wa Morocco unavyobeba neema ya Yanga

FADLU Pict


KOCHA Fadlu Davids anapitia presha kubwa ndani ya timu yake ya Raja Athletic ya Morocco, wakati wowote lolote linaweza kutokea akapoteza ajira hiyo, baada ya kuonekana kukosa matokeo mazuri, lakini Yanga wanachekelea hatua hiyo huku wakimtumia mahitaji yao.


Yanga kwa sasa inafundishwa na Abdlhalim Moalim ambaye walikubaliana na vigogo hao kuwa atakuwa kwenye kikosi hicho kama kocha mkuu hadi mwisho wa msimu huu ambapo Yanga itatafuta kocha mwingine wa kukiongoza kikosi hicho.


Mashabiki wa Raja wanatoa shinikizo kubwa kwa Fadlu aondolewe kwenye nafasi hiyo, wakiona kama ameshindwa kuwapa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo maarufu kwa jina la Botola Pro, ambapo mabosi wa timu hiyo wamekuwa na vikao vingi kuhusu ishu hiyo.

FADL 01

Hata hivyo, kuna mambo mawili yanayochochelewesha hatua hiyo ambayo ni kiasi cha fedha ambacho Raja itakitumia kumnlipa kocha huyo kwa kumsitishia mkataba lakini pia wachezaji wa timu hiyo ambao wanaona bado wanataka kumpigania kocha huyo.

Wakati presha ikiwa hivyo kwa Fadlu, Yanga inachekelea hatua hiyo ikiona kama hesabu zao zinakwenda kuwa sawa kwa kupatikana nafasi ya kumchukua kocha huyo wa zamani wa Simba ambaye ilishazungumza naye raia huyo wa Afrika Kusini.

Furaha ya Yanga ni kwamba endapo Raja itamtimua Fadlu basi mabingwa hao wa soka Tanzania itakwepa ugumu wa kuvunja mkataba wa kocha huyo na Waarabu hao ambapo, Fadlu atatakiwa kulipa kiasi cha Dola 600,000( Tsh 1.5 Bilioni).

FADL 04

“Ndio tunajua kwamba mambo sio mazuri pale Raja hata yeye (Fadlu) wakati tunaongea naye alituambia kwamba mashabiki wa timu ile ni vichaa, kama wakivunja mkataba wake itakuwa habari njema kwetu kwani tutaepuka gharama kubwa ya kuvunja mkataba wake,’ amesema bosi huyo wa juu wa Yanga.

Raja wakivunja mkataba wake watalazimika wao kumlipa kiasi kama hicho na kwa presha ya wale mashabiki wanaweza kukubaliana na kulipa kiasi hicho, hili litatupunguzia mzigo kwenye mazungumzo ya mkataba wake na sisi.

“Nilikwambia kwamba hapa Tanzania ni sisi Yanga ambao tulimfanya Fadlu asichukue ubingwa kutokana na kumfunga mechi zote mbili lakini hata ubora wa kikosi chetu ulikuwa mkubwa kushinda ule wa Simba lakini kiujumla alifanya kazi bora sana na alistahili kupata tuzo ya kocha bora wa msimu ule kama zingefanyika sherehe.”

FADL 01

Aidha bosi huyo wa Yanga amethibitisha kwamba wameshamtumia mradi kwa kocha huyo ambao amekubaliana nao ambapo kinachosubiriwa sasa ni hatua ya uamuzi wa kocha huyo pamoja na klabu yake ya Raja. Baadhi ya mambo ambayo Yanga wanataka kwa kocha huyo msimu ujao ni ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho la CRDB, nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na makombe mengine ya ndani.

“Tumeshamtumia mradi wetu kwa msimu ujao aliupitia na akaridhika lakini alituomba kwanza amalize msimu, tunachokiona sasa ni kwamba uamuzi huo unaweza kufanyika kwa haraka kutokana na hali inavyoendelea sasa.”

Fadlu ameiongoza Raja kwenye mechi 20 akichukua nafasi ya kocha mzawa Lassaad Chabbi, ambapo ndani ya mechi hizo ameshinda 11 akitoa sare sita na kupoteza michezo minne.

FADL 05

Mfupa mgumu kwa Fadlu ni hatua ya kutopata ushindi dhidi ya timu kubwa ambapo amepoteza dhidi ya RS Berkane (0-1) matokeo ambayo yalitibua hasira za mashabiki,Wydad Athletic (0-1), FAR Rabat (2-1) huku timu ndogo pekee ambayo ilimfunga kocha huyo ni COD Maknes (1-0), ambapo pia imetoa sare bila mabao dhidi ya Berknane na Wydad kwenye mechi za mzunguko wa kwanza.

Raja inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 42 juu yake ikiwa Berkane yenye pointi 43, Maghreb Fez inayofundishwa na kocha wa zamani mwingine wa Simba Pablo Martin iko nafasi ya pili na pointi 44 huku FAR Rabat ikiongoza msimamo na pointi 44 ikiwa haijapoteza mchezo wowote msimu huu.