Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo afichua kibano kipya kwa mastaa Yanga

KIBANO Pict


YANGA imewatoa kwa mkopo wachezaji wake watatu wa kigeni waliowasajili msimu huu, ambao ni Moussa Bala Conte, Celestine Ecua na Mohamed Doumbia, ilioamini ujio wao ungeweza kuipa nguvu kikosi hicho.


Kitendo cha mastaa hao kutolewa kwa mkopo, kimetajwa kinaweza kuwatibulia wale wapya ambao watasajiliwa msimu ujao kwani kuna kibano kipya kinakuja kudhibiti mienendo yao.


Yanga ilimsajili Moussa Bala Conte akitokea CS Sfaxien ya Tunisia akibeba matumaini angeziba pengo la Khalid Aucho ambaye alimaliza mkataba wake na kutimkia Singida Black Stars.

Conte kwa sasa yuko Morocco, akiitumkia Raja Athletic kwa mkopo, timu hiyo inafundishwa na kocha Fadlu Davids ambaye aliwahi kumhitaji kiungo huyo wakati anainoa Simba.

MBI 02

Ecua anayeichezea JS Kabylie ya Algeria kwa mkopo naye alisajiliwa na Yanga akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast huku akiwa anaichezea Zoman kwa mkopo akimaliza akiwa mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast.

Ecua hadi anaondoka Yanga alifunga bao moja pekee kwenye ligi alipowatungua Mtibwa Sugar wakati timu hiyo ikishinda 3-0.

Doumbia alitua Yanga akitarajiwa kuwa namba 10 kuziba nafasi ya Stephanie Aziz KI aliyeuzwa mwisho wa msimu uliopita Wydad, lakini wote wakashindwa kufikia matarajio ya klabu hiyo na kutolewa kwa mkopo.

TSHABA 02

Bosi mmoja wa juu wa Yanga ambaye anahusika kwenye usajili, amesema baadhi ya mastaa wa kigeni ambao waliwasajili msimu huu waliangushwa na kuwa na mambo mengi ya nje ya uwanja hatua ambayo ilizorotesha viwango vyao.

“Kuna maeneo mikataba ya wachezaji wetu hatukuwabana vizuri, unajua hao wachezaji wa kigeni ambao unawataja wote walikuwa na viwango vikubwa kwenye timu walizotoka, unamtaja Conte nani hakumwona alivyokuwa na CS Sfaxien,” amesema bosi huyo.

“Nenda kwa Ecua alikuwa mchezaji bora pale ASEC na Ligi Kuu ya Ivory Coast lakini bahati mbaya sana hawa wote wakajiunga hapa na wakashindwa kufanya vizuri na hata huko waliko bado viwango vyao haviko sawasawa.

“Kuna mambo mengi lakini kubwa ni maisha yao nje ya uwanja, walishindwa kujitunza ili wafanye vizuri, hapa Yanga tunalipa vizuri, niliwahi kusema hapa kwetu mchezaji anaweza kuishi kwa bonasi tu, tulianza kusikia taarifa nyingi kuhusu wao wakati walipokuwa hapa kuna mambo huko nje hayapo sawa.”

KIBA 01

Bosi huyo amesema wachezaji ambao watasajiliwa msimu ujao watakutana na vifungu vigumu kwenye mikataba yao itakayowafanya kujitunza na kuitumikia klabu kwa kupambana na kinyume na hapo hawatavumiliwa.

“Hatutaki kuingilia sana maisha ya nje ya uwanja lakini pale inapohitajika, itabidi tufanye hivyo, tumeshakubaliana huku ndani kwamba mikataba yetu yote ipitiwe upya, iwe na ubora wa kumfanya mchezaji kuwa kwenye presha ya kujituma na kuishi kwa nidhamu, tukikutana na kesi za ajabu huko nje hatutavumilia.

“Msimu huu moja ya jambo ambalo limechangia kupunguza nguvu ya kikosi chetu ni hawa wachezaji kushindwa kufanya yale ambayo tuliyatarajia tumejikuta tuna kikosi chembamba tukitegemea wachezaji wachache.”