Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mataifa waandaji AFCON 2027 yasaini azimio la pamoja

Muktasari:

  • Nchi hizo ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda zimesaini hati hiyo leo Jumatatu 11 Mei, 2026 kwa lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

Nchi waandaji wa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) wamesaini hati ya makubaliano ya pamoja inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027.

Nchi hizo ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda zimesaini hati hiyo leo Jumatatu 11 Mei, 2026 kwa lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dokta, Patrice Motssepe nchini Kenya ambapo rais huyo yupo kwaajili ya mkutano mkuu wa Africa Forward Summit 2026, lengo kuu la mkutano huo ni kujenga ushirikiano mpya wa kiuchumi, kiubunifu na kimaendeleo unaozingatia usawa na kuanachama na mifumo ya kizamani ya kutegemea misaada.

Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda na viongozi wengine wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais Wallace Karia.