Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnoga alivyoitosa England kisa Taifa Stars

Muktasari:

  • Akiwa katika mahojiano maalum na klabu hiyo, beki huyo alisema licha ya kuishi England lakini alikuwa akitembelea Tanzania mara kwa mara kipindi cha likizo jambo lililomjenga kupenda tamaduni za Bongo.

Beki wa kulia wa Salford City, Haji Mnoga amefunguka kwa nini aliamua kuichagua timu ya Taifa, Taifa Stars badala ya England alikozaliwa.

Akiwa katika mahojiano maalum na klabu hiyo, beki huyo alisema licha ya kuishi England lakini alikuwa akitembelea Tanzania mara kwa mara kipindi cha likizo jambo lililomjenga kupenda tamaduni za Bongo.

“Nilikuwa na nafasi ya kuchezea pande zote mbili, yaani Tanzania na England. Lakini ilipokuja nafasi ya kuitumikia Tanzania, sikuikataa,” alisema Mnoga na kuongeza;

"Tanzania imenijenga kihisia sana ndiyo maana nilipopata barua ya kuhitajika sikusita kwa sababu nilitamani siku moja."

Aliongeza safari zake za mara kwa mara kwenda Tanzania akiwa na baba yake zilimfanya ajione sehemu ya jamii ya Kitanzania, akijifunza mila, desturi na maisha ya kawaida ya Watanzania.

“Ukweli ni Tanzania ni sehemu kubwa ya maisha yangu. Nimekuwa nikija hapa tangu nikiwa mdogo, najua utamaduni na watu wake. Ilikuwa ni heshima kubwa kufanya uamuzi huu na zaidi nimemfurahisha baba yangu."

Mnoga aliitwa Stars kwa mara ya kwanza Machi 22 mwaka 2022 kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Central Africa na beki huyo alicheza dakika 46.

Tangu hapo amekuwa akiitwa kwenye kikosi hicho mara kwa mara.

Kwenye kikosi cha Salford Mnoga amekuwa mchezaji muhimu ukiwa msimu wake wa pili kuitumikia timu hiyo akisajiliwa kutokea Aldershot ya England.