Prime
Moalin ajitosa ishu ya Depu, atangaza uamuzi
KOCHA wa Yanga Abdihamid Moalin, amesema bado anaamini mshambuliaji wake Laurindo Auralio ‘Depu’, bado ana nafasi ya kuisaidia timu hiyo.
Yanga ilimsajili mshambuliaji huyo katika usajili wa Januari mwaka huu na kupewa nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa kwenye timu hiyo, lakini hadi sasa mambo kwake ni magumu huku akikosa nafasi pia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Mshambuliaji huyo ameshafunga mabao sita pekee hadi sasa katika ligi tangu aliposajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili.
Akizungumzia maendeleo ya mshambuliaji huyo Moalin amesema, bado wana imani naye hata baada ya kupata majeraha bado anajitafuta kurudi kuanza kufunga na wanaona kuwa ana nafasi ya kufanya mambo makubwa kwenye kila nafasi atakayoipata.
“Hakuna tatizo kwa Depu kwa sasa, unafahamu kwamba alipata majeraha akalazimika kuwa nje kwa muda mfupi, ameimarika ndio maana ameanza kucheza taratibu bado ana nafasi ya kufanya mambo makubwa kwenye timu hii kabla msimu haujamalizika.”
“Kila mchezaji hapa ana umuhimu, bahati mbaya kwake (Depu) baada ya kupata majeraha sasa anaanza kutafuta kurudi kwenye kiwango chake.