Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yafuzu Kombe la Dunia U-17

SERENGETI Pict

Muktasari:

  • Serengeti Boys iliyopo Kundi C katika AFCON U-17, imefikisha pointi sita ambazo bila ya kusubiri matokeo ya wapinzani wake kwa mechi zilizosalia, tayari imefuzu robo fainali ikiwa na uhakika wa kumaliza nafasi mbili za juu, ambapo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, pia itashiriki Kombe la Dunia U-17, fainali zitakazofanyika Qatar kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 13, 2026 huku Afrika ikiwakilishwa na timu kumi.

USHINDI wa mabao 3-0 ilioupata Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo Mei 17, 2026 dhidi ya Angola, kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U-17) zinazoendelea nchini Morocco, umeifanya ifuzu hatua ya robo fainali sambamba na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia U-17.

Serengeti Boys iliyopo Kundi C katika AFCON U-17, imefikisha pointi sita ambazo bila ya kusubiri matokeo ya wapinzani wake kwa mechi zilizosalia, tayari imefuzu robo fainali ikiwa na uhakika wa kumaliza nafasi mbili za juu, ambapo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, pia itashiriki Kombe la Dunia U-17, fainali zitakazofanyika Qatar kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 13, 2026 huku Afrika ikiwakilishwa na timu kumi.

Ipo hivi; Kanuni za AFCON U-17 mwaka huu, timu nane ambazo zitafuzu moja kwa moja kushiriki Kombe la Dunia U-17, ni zile zitakazomaliza nafasi mbili za juu kutoka makundi manne yaliyopo, kisha zingine mbili ili kukamilisha idadi ya timu kumi zitapatikana kwa kuchezwa mtoano (play-off) utakaowahusu watakaomaliza nafasi ya tatu kila kundi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Serengeti Boys inayonolewa na Kocha Elieneza Nsanganzelu, kufuzu robo fainali ya AFCON U-17 na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia U-17 kwani mara nne zilizopita katika ushiriki wake, iliishia makundi ambapo ni mwaka 2017, 2019, 2021 na 2025.

Katika mchezo wa leo uliofanyika Uwanja wa Mohammed VI Football Academy (pitch 3) uliopo mji wa Salé nchini Morocco, mabao ya Razaki Juma dakika ya 28, Hassan Kizinga (dk 52) na Sadam Hussein (dk 67), yaliifanya Serengeti Boys kutoka uwanjani wababe baada ya kuanza pia na ushindi kama huo dhidi ya Msumbiji, Mei 14, 2026.

Katika kundi hilo, Msumbiji inaburuza mkia ikiwa haina pointi baada ya kupoteza mechi ya kwanza, baadaye itapambana na Mali yenye pointi moja. Angola nayo ina pointi moja, inahitaji kufanya vizuri mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji kuangalia uwezekano wa kufuzu kupitia mtoano.

Kwa sasa Serengeti Boys inasubiri kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya Mali, Mei 20, 2026, kabla ya kuanza 16 bora.