Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Curtis Jones: Liverpool tupo kwenye hali mbaya, tujitafakari

JONES Pict

Muktasari:

  • Liverpool imepoteza mechi hiyo ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield, hali ambayo imewanyima furaha mashabiki wa The Reds ambao walitarajia huenda kikosi chao kingewapa kicheko baada ya kupoteza mechi ya Ligi Kuu ya EPL mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Notingham Forest.

Kiungo wa Liverpool, Curtis Jones, ametoa wito kwa wachezaji wenzake baada ya timu hiyo kupokea kichapo kizito kutoka kwa PSV jana Jumatano, Novemba 26, 2025 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Liverpool imepoteza mechi hiyo ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield, hali ambayo imewanyima furaha mashabiki wa The Reds ambao walitarajia huenda kikosi chao kingewapa kicheko baada ya kupoteza mechi ya Ligi Kuu ya EPL mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Notingham Forest.

Jones amesema Liverpool iko katika hali mbaya kwa sasa, hivyo mabadiliko ya haraka kutoka kwa wachezaji wote yanahitajika, hivyo wana jukumu la kuipambania timu hiyo inayonolewa na kocha kutoka Uholanzi, Arne Slot.

Kiungo huyo amekiri kuwa kikosi chao kilionyesha udhaifu mkubwa katika kila idara dhidi ya PSV ambayo ilionekama kuwa na uimara wakati wote, hali ambayo ilisaidia kupata matokeo ya 4-1 ugenini.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Jones imezua mjadala, huku mchezaji wa zamani wa Liverpool na mchambuzi wa soka, Jamie Carragher, akieleza haikuwa sawa kumtuma mchezaji kijana kama huyo kukabiliana na vyombo vya habari baada ya kipigo kikubwa. 

Carragher amedai kuwa nyota mkubwa wa timu, Mohamed Salah, alipaswa kuongoza na kujitokeza mbele ya wanahabari ili kutoa maoni ya klabu badala ya kumwacha Jones kubeba mzigo huo.

Kichapo hicho kutoka kwa PSV kimeongeza shinikizo kwenye klabu ya Liverpool, huku mashabiki na wachambuzi wakihofia mwelekeo wa timu katika mechi zijazo, huku mashabiki wakisubiri kuona iwapo wito wa Jones utaamsha ari mpya ndani ya kikosi hicho.