Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eriksen aanguka uwanjani, Denmark yatoa taarifa

ERIKSEN Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo ulisimamishwa dakika ya 65 baada ya Eriksen kuanguka bila kuguswa na mchezaji mwingine, huku madaktari na wahudumu wakikimbilia haraka kumhudumia.

ODENSE, DENMARK: HOFU kubwa ilitanda katika ulimwengu wa soka baada ya kiungo mkongwe wa Denmark, Christian Eriksen kuanguka ghafla uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ukraine.

Mchezo huo ulisimamishwa dakika ya 65 baada ya Eriksen kuanguka bila kuguswa na mchezaji mwingine, huku madaktari na wahudumu wakikimbilia haraka kumhudumia.

Kwa bahati nzuri, Shirikisho la Soka la Denmark limethibitisha kuwa nyota huyo mwenye miaka 34 yuko salama na alikuwa na fahamu muda mfupi baada ya tukio hilo.

Daktari wa timu ya taifa ya Denmark, Morten Boesen amesema:

“Christian anaendelea vizuri na alitoka uwanjani akitembea mwenyewe.

ER 02

“Kwa mtazamo wangu kifaa chake cha ICD kilifanya kazi kama ilivyopaswa. Alipoteza fahamu kwa muda mfupi sana lakini alizinduka haraka.”

Boesen aliongeza Eriksen alipelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Tukio hilo limewakumbusha wengi yaliyotokea katika fainali za Euro 2020 wakati Eriksen alipata mshtuko wa moyo akiwa uwanjani dhidi ya Finland.

Baada ya tukio hilo, aliwekewa kifaa maalumu cha moyo kinachoitwa Implantable Cardioverter Defibrillator (ICD) ambacho humsaidia kudhibiti mapigo ya moyo.

Kifaa hicho kilimruhusu kurejea kucheza soka mwaka 2022 akiwa Brentford kabla ya kujiunga na Manchester United na baadaye Wolfsburg ya Ujerumani.

Nahodha wa Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg amesema:

“Nilimwona Christian akianguka chini. Kila mtu alichukua hatua kwa haraka sana.

“Nawapongeza wale wote waliomsaidia kwa sababu walionyesha ujasiri mkubwa.”

Kama ilivyokuwa mwaka 2021, wachezaji wa timu zote mbili waliunda duara kumzunguka Eriksen wakati madaktari wakimhudumia.

ER 01

Baada ya mchezo kusitishwa, wachezaji na benchi la ufundi waliungana katikati ya uwanja kusikiliza maelekezo ya Kocha Brian Riemer.

“Jambo muhimu zaidi ni Christian yuko salama,” amesema Riemer.

“Ametuma salamu kwa wachezaji wote na kusema anaendelea vizuri.”

Eriksen alikuwa akicheza mechi yake ya 151 akiwa na Denmark na hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu lini atarejea uwanjani.