Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wolper ajipamba kuficha shida zake

Muktasari:

  • Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Wolper amesema kujipamba na kuonekana nadhifu si lazima kumaanishe mtu ana maisha mazuri kifedha, bali wakati mwingine ni njia ya kuficha changamoto binafsi.

Msanii wa filamu na mfanyabiashara Jackline Wolper, amesema watu wengi hujikuta wakihukumiwa vibaya kwa mwonekano wao wa nje, ilhali ndani wanapitia changamoto mbalimbali za maisha ambazo si rahisi kuzijua kwa haraka.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Wolper amesema kujipamba na kuonekana nadhifu si lazima kumaanishe mtu ana maisha mazuri kifedha, bali wakati mwingine ni njia ya kuficha changamoto binafsi.

“Mimi naweza kupita njiani mtu akadhani nina fedha nyingi maana napenda kujiweka nadhifu kila wakati ili tu heshima yangu ibaki palepale,” amesema Wolper.

Aliongeza kuwa si jambo jema watu kujua kila kinachoendelea katika maisha ya mtu binafsi, hasa pale mtu anapokuwa kwenye kipindi kigumu cha kifedha au kijamii, hivyo kujiremba humsaidia kujiweka imara mbele ya jamii.

Wolper alisisitiza kuwa baadhi ya watu huamua kuendelea kuonekana vizuri mitaani hata wanapopitia changamoto, ili kuepuka huruma au maneno yasiyo ya lazima kutoka kwa jamii na mitandao ya kijamii.

Wolper ambaye ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Movies na pia mfanyabiashara, kwa muda mrefu amekuwa akijulikana kwa mtindo wake wa maisha ya kujituma, urembo na kujitokeza nadhifu katika matukio mbalimbali ya kijamii na burudani.