Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam, Lupopo zamsaka beki mkongo

AZAM Pict

Muktasari:

  • Azam ipo kwenye harakati za kuendelea kukiboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, huku ikiendeleza mawasiliano na klabu mbalimbali, ikiwemo Union Maniema, kwa lengo la kupata huduma ya beki huyo.

MABOSI wa Azam FC wamehamishia nguvu zao katika kuimarisha safu ya ulinzi baada ya kuanza mazungumzo ya kumsajili beki wa kati wa Union Maniema, Jeancy Mpindi Mukuene, ambaye pia anawaniwa na FC Lupopo.

Azam ipo kwenye harakati za kuendelea kukiboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, huku ikiendeleza mawasiliano na klabu mbalimbali, ikiwemo Union Maniema, kwa lengo la kupata huduma ya beki huyo.

Mukuene ni miongoni mwa mabeki waliovutia benchi la ufundi la Azam, huku kocha Florent Ibenge akitajwa kuwa chanzo cha mapendekezo ya usajili huo kutokana na uzoefu wake mkubwa wa soka la DR Congo na uelewa wake wa wachezaji wa eneo hilo.

Mwanaspoti linafahamu kuwa viongozi wa Azam wanaamini Mukuene anaweza kuwa suluhisho la muda mrefu katika safu yao ya ulinzi kutokana na uwezo wake wa kucheza kwa utulivu, uimara katika mipira ya juu na uzoefu alioupata kwenye Ligi Kuu ya Congo.

“Ni kweli jina lake lipo kwenye orodha ya Azam. Kocha Ibenge amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na anaamini ana sifa zinazoweza kuisaidia timu. Mazungumzo ya awali yameanza, lakini bado kuna hatua kadhaa za kukamilisha,” kimesema chanzo hicho.


AZAM, LUPOPO ZAKABILIANA

Mbali na Azam, FC Lupopo nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya beki huyo, jambo linalotarajiwa kuongeza ushindani katika mazungumzo ya usajili yanayoendelea. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa ushindani kutoka Lupopo unaweza kulifanya dili hilo kuwa gumu zaidi, lakini Azam inaamini inaweza kutumia mahusiano mazuri ya Ibenge ndani ya soka la Congo kumshawishi mchezaji huyo.

“Lupopo nao wanamhitaji, hivyo haitakuwa kazi rahisi. Hata hivyo, Azam inaamini nafasi ya Ibenge na mradi wa timu unaweza kumvutia zaidi mchezaji huyo,” kiliongeza chanzo hicho.


WASIKIE AZAM

Meneja Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema hafahamu chochote kuhusu mchezaji anayesajiliwa kwa sasa, kwani masuala hayo yapo chini ya viongozi wa klabu.

“Kiukweli sifahamu chochote. Kazi yangu ni kupewa jina la mchezaji na kumtangaza tu. Masuala ya usajili na kufuatilia wachezaji wanaosajiliwa ni ya viongozi wangu wa juu,” amesema Zakaria.


NAFASI YAKE AZAM

Iwapo Mukuene atafanikiwa kutua Azam FC, huenda mchezaji mmoja wa kigeni katika safu ya ulinzi akaondoka ili kumpisha Mkongomani huyo.

Katika orodha ya mabeki wa kigeni waliopo kwa sasa Azam, Yoro Diaby ndiye anayetarajiwa kumaliza mkataba wake msimu huu.