Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker atia neno dili la beki Simba

BEKI Pict


KIWANGO cha beki wa kati, Ismael Toure, kimewakosha mabosi wa klabu ya Simba, huku benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Steve Barker likibariki uamuzi wa Muivory Coast huyo kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja.


Toure ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosaini mikataba ya muda mfupi msimu huu ambapo ni miezi sita wakati anatua dirisha dogo la usajili la Januari 2026, lakini pia anaingia kwenye kundi la mastaa wa klabu hiyo wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu.


Ikumbukwe kuwa, beki huyo alisajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuachana na FC Baniyas ya Umoja wa Falme za Kiarabu, huku akiwa na rekodi ya kuchezea Stellenbosch na Marumo Gallants zote za Afrika Kusini.

Simba ilimleta Toure ili kuimarisha safu ya ulinzi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Wekundu hao walikuwa wakishiriki kabla ya kutolewa hatua ya makundi.

Ujio wake umefuatia mapendekezo ya kocha mkuu Barker, ambaye aliwahi kufanya naye kazi nchini Afrika Kusini katika klabu ya Stellenbosch.

BEK 01

Katika mechi tisa za Ligi Kuu Bara ambazo Simba imecheza tangu beki huyo atue kwenye kikosi hicho, Toure amecheza tano na zote akianza kikosi cha kwanza, huku akiwa na rekodi ya kucheza dakika 450 na kufunga bao moja.

Mmoja kati ya viongozi wa Simba aliliambia Mwanaspoti kuwa, ni wazi kwamba kiwango cha Toure kimekuwa na mchango mzuri kwa kikosi hicho ndio maana uongozi umeamua kumuongeza mkataba.

“Wakati anafika tulitaka kwanza kuona uwezo wake, tukampa mkataba mfupi lakini tumeridhika na kiwango chake, hivyo wakati wowote tutampa mkataba mrefu zaidi,” amesema bosi huyo wa juu wa Simba.

“Tutampa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine, kiukweli ukuta wetu kwasasa umetulia sana na yeye (Toure) ni mmoja wa watu waliorudisha ubora eneo la ulinzi.”

Akizungumza na Mwanaspoti, Barker amesema, Toure ni mmoja wa wachezaji wenye nidhamu na ushirikiano mkubwa na wenzake hasa anapokuwa uwanjani hata nje, lakini wakati anampendekeza alijua ana ubora wa kiwango gani.

BEK 02

“Ni moja ya nguzo zetu kwenye safu ya ulinzi, namfahamu kabla, nilijua tunaleta mchezaji wa ubora gani, ana uzoefu na hesabu nzuri uwanjani,” amesema Barker.

“Ukiangalia ameonyesha kuelewana vizuri na wenzake uwanjani ndio maana imekuwa rahisi kumuona hata ukibadilisha mtu wa kucheza naye sambamba lakini bado timu inakuwa na utulivu.

Kwa sasa, Simba inatumia zaidi pacha ya Rushine De Reuck ambaye alitua tangu mwanzoni mwa msimu akicheza sambamba na Toure, ambapo ndio wanapishana kutokana na ukubwa wa mechi au mipango ya kocha.