Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SMZ kuweka usawa miundombinu ya michezo

SMZ Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Wete, Shafi Mohammed Shafi kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Riziki Juma Pembe, katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea na mpango wake wa kuimarisha na kukamilisha mtandao wa viwanja vya mpira ili kuhakikisha Pemba inapata miundombinu ya michezo yenye hadhi sawa na Unguja.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Wete, Shafi Mohammed Shafi kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Riziki Juma Pembe, katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Mwakilishi huyo alitaka kufahamu kuhusu Serikali kujenga viwanja vya mpira wa miguu kisiwani Pemba kama ilivyovijenga Unguja.

Gulam amesema, Serikali kwa sasa inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa viwanja vya Wilaya na Mikoa, ambapo kiwanja cha Wilaya ya Wete tayari kimejengwa katika eneo la Pandani ndani ya Wilaya hiyo.

Amesema, Serikali inafanya hivyo kwa lengo la kukuza vipaji, kuongeza fursa za michezo na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

"Mbali na uwanja wa Gombani uliopo Pemba, tayari Serikali imejenga viwanja vya Wilaya na Mkoa katika maeneo mbalimbali ya visiwa hivyo," amesema.
 
Ametaja viwanja ambavyo vimejengwa ni vile vya Mkoa vilivyopo Skuli ya Kangani (Kangani) na Kinyikani (Mchangamdogo) na viwanja vya Wilaya vya Gombani (Chake Chake), Ukutini (Mkoani), Gongoni (Micheweni) na Pandani (Wete).