Viti 2,000 Kariakoo Derby vyaongezwa Isamuhyo
Muktasari:
- Katika maboresho hayo, JKT inaendelea na ujenzi wa majukwaa mapya kwa muda mfupi uliosalia kwa kuongeza viti 2,000.
- Hatua itakayoongeza uwezo wa uwanja huo kutoka mashabiki 8,000 hadi kufikia mashabiki 10,000.
JESHI la Kujenga Taifa (JKT), linaendelea na maboresho ya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ikiwa ni maandalizi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga inayotarajiwa kupigwa keshokutwa, Jumapili.
Katika maboresho hayo, JKT inaendelea na ujenzi wa majukwaa mapya kwa muda mfupi uliosalia kwa kuongeza viti 2,000.
Hatua itakayoongeza uwezo wa uwanja huo kutoka mashabiki 10000 hadi kufikia mashabiki 12,000.
Ongezeko hilo linalenga kukidhi wingi wa mashabiki wanaotarajiwa kujitokeza kushuhudia mchezo huo watani wa jadi.
Awali, uwanja huo ambao Simba imekuwa ikiutumia kwa michezo yake ya nyumbani ulikuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 10000.
Hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki kuwa na hofu ya kukosa nafasi za kukaa katika michezo mikubwa
Hata hivyo, maboresho yanayoendelea yanatarajiwa kupunguza changamoto hiyo japo ni kwa sehemu ndogo.
Dabi hiyo ya Jumapili inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku viingilio vikitangazwa leo, Ijumaa kuwa ni Sh15,000, VIP B Sh30,000 na VIP A Sh50,000.