Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta kawa mbogo, awajibu Gary Neville, Jamie Carragher

Muktasari:

  • Wachambuzi wa Sky Sports, Gary Neville na Jamie Carragher, walidai Arsenal ilicheza kwa tahadhari kubwa walipokutana na Manchester City, jambo ambalo Arteta amefunguka kuwa sio kweli.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amepuuza madai ya wachambuzi waliosema kuwa Arsenal inacheza kwa kusita sita na kusisitiza kwamba falsafa yake ndiyo inayozalisha mashambulizi zaidi katika soka la England.

Wachambuzi wa Sky Sports, Gary Neville na Jamie Carragher, walidai Arsenal ilicheza kwa tahadhari kubwa walipokutana na Manchester City, jambo ambalo Arteta amefunguka kuwa sio kweli.

Arteta alitoa majibu wakati wa mahojiano kabla ya mechi yao ya Carabao Cup dhidi ya Port Vale jana, ambapo kwa hasira alisema kikosi chake kimejaa vipaji vya wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kushambulia na hata makipa wake ni sehemu ya mashambulizi.

Kocha huyo Mhispania aliwataja David Raya (kipa), Gabriel (beki) na Mikel Merino (kiungo) kama mifano ya wachezaji wenye mtazamo wa kushambulia.

“Ukiangalia wachezaji tulionao, kuanzia kwa kipa, ni kipa mwenye takwimu za kushambulia zaidi katika ligi. Mabeki wa kati, pia ndio mabeki wa kati wanaoshambulia zaidi. Mabeki wa pembeni pia  ukiangalia takwimu zao utaelewa. Huwa tunacheza na kiungo mshambuliaji upande wa kulia ambaye msimu uliopita alicheza kama namba tisa. Hiyo ni dalili ya kuwa ana uwezo mkubwa wa kushambulia, sijawahi kuona kwenye ligi kiungo akaenda kuwa namba tisa. Hivyo tuna aina mbalimbali za wachezaji wa kushambulia, kila mmoja akiwa na kipaji cha kipekee,” alisema.

“Ukiangalia rekodi yetu ya ushindi, idadi ya mabao tuliyofunga, idadi ya mechi tulizomaliza bila ya kuruhusu bao na namna tulivyocheza dhidi ya Man City inaonyesha wazi, sasa sujui mtu anaposema tunashambulia kwa kuvizia au kusita sita huwa simuelewi.”

Arteta alisema amepokea jumbe nyingi kutoka kwa makocha, viongozi na marais wa klabu wakimsifu kwa jinsi Arsenal ilivyocheza dhidi ya Manchester City, jambo analoliona kama ishara ya kwamba walikuwa bora tofauti na kile ambacho wachambuzi hao wamekisema.