Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji kasema... Kuna mtu anapigwa!

GWIJI Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo inakutanisha miamba miwili inayopewa nafasi kubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England na hilo ndilo litakalofanya kipute hicho kiwe cha vuta nikuvute.

LONDON, ENGLAND: MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu England unarudi wikiendi hii, ambapo kivumbi cha maana kitakuwa huko Anfield, wakati Liverpool itakapojimwaga nyumbani kukabiliana na Arsenal.

Mechi hiyo inakutanisha miamba miwili inayopewa nafasi kubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England na hilo ndilo litakalofanya kipute hicho kiwe cha vuta nikuvute.

Lakini, gwiji wa Ligi Kuu England, aliyewahi kukipiga kwenye kikosi cha Manchester United, Gary Neville ametoa utabiri wake katika mechi hiyo ya Anfield, akidai Arsenal itaichapa Liverpool kwao. Hata hivyo, Arsenal haitakuwa na huduma ya mkali wake matata, Bukayo Saka.

Timu hizo zilimaliza nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, licha ya kwamba chama la Arne Slot, Liverpool ilimaliza pointi 10 juu dhidi ya vijana wa Mikel Arteta, Arsenal. Na sasa zinaingia uwanjani kila timu ikiwa imefanya usajili mkubwa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, ambapo Arsenal imewanasa Martin Zubimendi, Eberechi Eze na Viktor Gyokeres kwa kuwataja kwa uchache, wakati Liverpool imewaingiza kikosini Florian Wirtz, Hugo Ekitike, Jeremie Frimpong.

Timu zote zimeanza vizuri, zikiibuka na ushindi kwenye mechi zao za kwanza, lakini Neville alisema: “Nawapa nafasi Arsenal kushinda. Sijui itakuwa ngapi, lakini Arsenal itashinda.”€

Takwimu zinaonyesha timu hizo zimekutana mara 66 kwenye Ligi Kuu England, ambapo mechi 23 zilimalizika kwa sare, huku Liverpool ikishinda 25, mara 16 nyumbani na tisa ugenini, huku Arsenal ikishinda 18, mara 12 nyumbani na sita tu ugenini. Itakuwaje hiyo kesho Jumapili?

Ukiacha kipute hicho cha kibabe, mechi nyingine zitakazopigwa Jumapili, Manchester City itakwenda ugenini kukipiga na Brighton, wakati Nottingham Forest itakuwa na kazi nzito mbele ya West Ham United na Aston Villa ya kocha Unai Emery itajimwaga uwanjani Villa Park kuonyesha ubabe na Crystal Palace.

Lakini, kasheshe la Ligi Kuu England litaanzia leo Jumamosi, ambapo uwanjani Stamford Bridge kutakuwa na kipute cha London derby, wakati Chelsea itakapokipiga na Fulham, wakati Sunderland itakuwa na kazi mbele ya Brentford.

Tottenham Hotspur itakuwa nyumbani kucheza na Bournemouth, wakati Wolves itakuwa na kazi mbele ya Everton na Leeds United iliyotoka kuchapwa mabao 5-0 na Arsenal itakuwa nyumbani kusaka ushindi muhimu dhidi ya Newcastle United.

Masikio na macho ya wengi yatakuwa huko Old Trafford, kuona Manchester United kama itaamka kwenye majanga yanayowakabili kwa sasa itakapokipiga na Burnley. Man United haijashinda mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England msimu huu, hivyo itahitaji kusaka ushindi wa kila aina katika mechi hiyo ili kurudisha matumaini ya kufanya vizuri.

Takwimu zinaonyesha, Man United na Burnley zimekutana mara 18 kwenye mechi za Ligi Kuu England, ambapo sita zilimalizika kwa sare, huko Man United ikishinda 10, nne nyumbani na sita ugenini, wakati Burnley yenyewe imeshinda mbili, moja nyumbani na nyingine ugenini. Itakuwaje safari hii? Ngoja tuone!