Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe akabidhiwa ufaransa Kombe la Dunia 2026

MBAPPE Pict (1)

Muktasari:

  • Mbappe, ambaye ana mabao 56 akiwa na jezi ya Ufaransa, atakuwa na kibarua cha kufunga mabao mawili tu ili kuvunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo, Olivier Giroud (57).

PARIS, UFARANSA: STRAIKA wa Real Madrid, Kylian Mbappe na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or Ousmane Dembele wataongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kuelekea Kombe la Dunia baada ya kocha Didier Deschamps kutangaza majina 26 yatakayoiwakilisha nchi hiyo kwenye mashindano ya mwaka huu.

Mbappe, ambaye ana mabao 56 akiwa na jezi ya Ufaransa, atakuwa na kibarua cha kufunga mabao mawili tu ili kuvunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo, Olivier Giroud (57).

Nyota huyo wa Real Madrid anatarajiwa kuendelea kuwa nahodha wa kikosi hicho licha ya hivi karibuni kusumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja. Kwa upande mwingine, Dembele anatua kwenye Kombe la Dunia akiwa katika kiwango bora baada ya kufunga mabao 35 na kusaidia Paris Saint-Germain kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Mafanikio hayo yalimwezesha kuwa mchezaji wa pili kutoka Ufaransa kushinda Ballon d’Or katika karne hii huku akiwa bado hajafunga bao lolote katika michuano ya Kombe la Dunia licha ya kushiriki mara mbili.

MBAPP 01

Kocha Deschamps ameunda safu ya ushambuliaji inayowajumuisha nyota wa Bayern Munich Michael Olise na chipukizi wa PSG Desire Doue huku kiungo mshambuliaji wa Manchester City Rayan Cherki na beki wa Arsenal William Saliba wakitajwa miongoni mwa wachezaji saba wanaocheza Ligi Kuu England walioitwa kwenye kikosi hicho.

Katika kikosi hicho pia wamo Lucas Hernandez, N'Golo Kante, Mbappe na Dembele ambao ndio pekee waliosalia kutoka kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Hata hivyo, Deschamps amefanya maamuzi yaliyozua mjadala kwa kuwaacha nje baadhi ya nyota waliokuwepo katika Kombe la Dunia 2022 akiwemo kiungo wa Real Madrid Eduardo Camavinga pamoja na mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Randal Kolo Muani.

MBAPP 02

Kipa wa PSG Lucas Chevalier naye ameachwa nje, huku kipa ambaye hajawahi kuitwa timu ya taifa, Robin Risser wa Lens akiitwa kuwa chaguo la akiba pamoja na Brice Samba nyuma ya kipa namba moja Mike Maignan.

Straika wa Liverpool Hugo Ekitike, ambaye alipata majeraha makubwa ya kisigino mwezi Aprili ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri waliokosekana kwenye kikosi hicho kama ilivyotarajiwa.

Akizungumza baada ya kutangaza kikosi hicho, Deschamps alisema uteuzi wake haukulenga kuchukua majina makubwa pekee bali kuunda timu yenye uwiano mzuri.

“Si lazima hawa wawe wachezaji 26 bora zaidi mmoja mmoja, lakini ni suala la uwiano na namna timu itakavyoungana,” alisema Deschamps.

Ufaransa itaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo dhidi ya Senegal utakaochezwa mjini New Jersey Juni 16 kabla ya kuvaana na Iraq Juni 22 na Norway Juni 26, katika hatua ya makundi.

MBAPP 03

Kikosi kizima:

Makipa: Mike Maignan (AC Milan), Robin Risser (Lens), Brice Samba (Rennes)

Mabeki: Lucas Digne (Aston Villa), Malo Gusto (Chelsea), Lucas Hernandez (Paris St-Germain), Theo Hernandez (Al Hilal), Ibrahima Konate (Liverpool), Maxence Lacroix (Crystal Palace), Jules Kounde (Barcelona), William Saliba (Arsenal), Dayot Upamenaco (Bayern Munich)

Viungo: N'Golo Kante (Fenerbache), Manu Kone (Roma), Adrien Rabiot (AC Milan), Aurelien Tchouameni (Real Madrid), Warren Zaire-Emery (Paris St-Germain)

Washambuliaji: Maghnes Akliouche (Monaco), Bradley Barcola (Paris St-Germain), Rayan Cherki (Man City), Ousmane Dembele (Paris St-Germain), Desire Doue (Paris St-Germain), Michael Olise (Bayern Munich), Kylian Mbappe (Real Madrid), Jean-Phillipe Mateta (Crystal Palace), Marcus Thuram (Inter Milan)