Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onana apokewa kwa shangwe Uturuki

ONANA Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo raia wa Cameroon alisafiri kwenda Uturuki akiwa na mkewe mrembo Melanie, Alhamisi iliyopita kwenda kukamilisha uhamisho wa kujiunga kwenye Turkish Super Lig akiwa ameichezea mechi moja tu Man United msimu huu, ile ya kipigo kutoka kwa timu ya daraja la chini ya Grimsby Town kwenye Kombe la Ligi.

INSTABUL, UTURUKI: Kipa, Andre Onana ataongeza mshahara wake mara mbili huko Trabzonspor baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo wa msimu mzima na kuyapa kisogo maisha magumu Manchester United.

Kipa huyo raia wa Cameroon alisafiri kwenda Uturuki akiwa na mkewe mrembo Melanie, Alhamisi iliyopita kwenda kukamilisha uhamisho wa kujiunga kwenye Turkish Super Lig akiwa ameichezea mechi moja tu Man United msimu huu, ile ya kipigo kutoka kwa timu ya daraja la chini ya Grimsby Town kwenye Kombe la Ligi.

Akiwa amepata maumivu ya misuli ya paja kwenye kipindi cha majira ya kiangazi na kushindwa kutumika kwenye mechi za pre-season za Man United, kipa Mturuki Altay Bayindir alipewa nafasi na kocha Ruben Amorim kucheza kwenye mechi tatu za Ligi Kuu England ilizocheza timu hiyo hadi sasa msimu huu.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, kocha Amorim alisajili kipa mpya, Mbelgiji Senne Lammens kutoka klabu ya Royal Antwerp kuja kuokoa jahazi baada ya Onana, aliyenaswa kwa Pauni 47.2 milioni akitokea Inter Milan miaka miwili iliyopita kushindwa kufanya vizuri.

Hata hivyo, kwenye mkataba wa Onana na Trabzonspor hakuna kipengele kinachowalazimisha kumsajili jumla wakati mkopo wake utakapofika tamati mwisho wa msimu na klabu hiyo ya Uturuki haijalipa ada yoyote ya mkopo badala yake itamlipa tu mshahara wote kipa huyo.

Kinachoelezwa ni kwamba Onana atakwenda kuongeza mshahara wake karibu mara mbili huko Trabzonspor, ambapo kama angebaki Man United mshahara wake ungeshuka kutoka Pauni 170,000 kwa wiki hadi Pauni 120,000 na Pauni 67,000 kwa wiki baada ya kodi baada ya wachezaji wote kupunguziwa kwa asilimia 25 kutokana na kushindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man United ilimtakia kila heri Onana kwenye taarifa yake iliyosema: "Katika msimu wake wa kwanza United, Andre alikuwa sehemu ya kikosi kilichobeba Kombe la FA baada ya kuifunga 2-1 Manchester City uwanjani Wembley. Onana alicheza mechi 50 katika msimu wa pili na sasa amekubali kujiunga kwa mkopo Trabzonspor. Uhamisho umekamilika kabla ya dirisha kufungwa Ijumaa. Tunamtakia kila la heri."

Baada ya kufanya makosa mengi kwenye kikosi cha Man United, mashabiki wengi wa kikosi hicho wamefurahia uhamisho huo.
Shabiki mmoja aliandika kwenye Instagram: "Punguzo zuri, heri kuchelewa kuliko kutofanya kabisa!"

Mwingine aliongeza: "Tafadhali mwaacheni aondoke bure endapo kama watamrudisha, sisi hatujali", wakati shabiki wa tatu alisema: "Mwisho wa zama za makosa."