Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo KMC FC mlangoni JKT Tanzania

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Coastal Union na Dodoma Jiji, mkataba wake na KMC unafikia tamati rasmi Juni 30, 2026, ambapo kwa hali ya kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya Championship msimu ujao, kuna uwezekano mdogo wa kuendelea kukichezea.

WAKATI KMC FC ikibakisha hatua chache kucheza Ligi ya Championship msimu ujao wa 2026-2027, nyota wa timu hiyo, Rashid Chambo ameanza kuzivutia klabu mbalimbali ili kuipata saini yake, huku maafande wa JKT Tanzania ikiwa mstari wa mbele.

Nyota huyo wa zamani wa Coastal Union na Dodoma Jiji, mkataba wake na KMC unafikia tamati rasmi Juni 30, 2026, ambapo kwa hali ya kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya Championship msimu ujao, kuna uwezekano mdogo wa kuendelea kukichezea.

Katika Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2025-2026, KMC inaburuza mkiani mwa msimamo ikiwa nafasi ya 16 na pointi zake tisa tu, baada ya kushinda mechi mbili, ikitoka sare tatu na kupoteza 20 kati ya 25 iliyocheza, ikifunga mabao 13 na kuruhusu 43.

Licha ya kiwango kisichoridhisha kwa timu hiyo, ila Chambo amechangia mabao sita ya Ligi Kuu akiwa kikosini humo, baada ya kufunga matatu na kuasisti pia matatu, jambo linalomweka katika nafasi ya kuondoka pindi tu mkataba wake utakapoisha.

KIUN 01

Akizungumza na Mwanaspoti Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC (CEO), Daniel Madenyeka amesema kwa sasa ni ngumu kuzungumzia suala la wachezaji wanaomaliza mikataba yao, kutokana na nafasi mbaya iliyo timu hiyo ya kujinasua na kutoshuka daraja.

“Ni ngumu kuzungumzia hilo kwa sasa kutokana na nafasi tuliyopo, tathimini ya kina kiujumla tutaifanya baada ya msimu kumalizika, ninachowaomba mashabiki zetu waendelee kutuunga mkono licha ya mwenendo usioridhisha,” amesema Madenyeka.

KIUN 02

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua nyota huyo anayeweza kucheza mshambuliaji wa kati na wakati mwingine akitokea pembeni kwa maana ya winga ya kulia na kushoto kwa ufasaha, ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu za kutua JKT Tanzania.