Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgosi aipongeza Yanga, akiichapa Dar

MGOSI Pict

Muktasari:

  • Simba ilikuwa mwenyeji kwenye mchezo huo uliopigwa leo katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1.

KAIMU Kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan 'Mgosi' amesema walijidhatiti tangu msimu uliopita na walifanya tathmini wapi wamekosa na wakarekebisha kwenye Ligi Kuu ya Wanawake Bara.

Simba ilikuwa mwenyeji kwenye mchezo huo uliopigwa leo katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendeleza rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja msimu huu kwenye mechi 16 ikiendelea kusalia kileleni na pointi 46.

Akizungumza baada ya mchezo, Mgosi amesema Yanga Princess imeimarika miaka ya karibuni kwani awali walikuwa wakiichapa mabao sita, akiipongeza kwa kuonyesha ushindani mkubwa.

"Niwapongeze Yanga kwa kuonyesha ushindani mzuri ubora wao unakuwa siku hadi siku, lakini ikumbukwe Simba ilianza kujitengeneza muda mrefu tangu wakati huo sasa hivi ni muendelezo tu.

"Yanga pia imebadilika zamani ilikuwa ilikuwa ikikutana na Simba ni vipigo tu mfululizo vya mabao sita hadi saba kwahiyo ndiyo ligi kadri muda unavyokwenda wakawa wanaimarika," amesema.

Leo kocha huyo amepewa tuzo ya kocha bora wa mwezi Aprili baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda mechi tano mfululizo.