Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunha, Sesko ngoma ngumu

Muktasari:

  • Washambuliaji hao wawili hawakucheza kwenye mechi ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Everton, Jumatatu iliyopita na wamewekwa kando katika msafara wa kuelekea Selhurst Park.

MUNICH, UJERUMANI: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim hatakuwa na huduma za washambuliaji wake Matheus Cunha na Benjamin Sesko katika mechi ngumu ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace, Jumapili.

Washambuliaji hao wawili hawakucheza kwenye mechi ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Everton, Jumatatu iliyopita na wamewekwa kando katika msafara wa kuelekea Selhurst Park.

Cunha aliumia mazoezini wikiendi iliyopita, akiongeza idadi ya wachezaji wagonjwa kwenye eneo la kushambulia sambamba na Sesko, ambaye aliumia katika mechi ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Kutokana na hilo, kocha Amorim alilazimika kumtumia Joshua Zirkzee akimwaandisha kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu England msimu huu alipokabiliana na Everton.

Mambo hayakuwa mazuri, Man United ilishindwa kupitisha mpira kwenye goli la kipa Jordan Pickford, licha ya kucheza dhidi ya timu iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kufuatia Idrissa Gueye kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kupigana na mchezaji mwenzake Michael Keane.

Mashabiki walikuwa na matumaini Cunha angerejea uwanjani kwenye mechi dhidi ya Palace, baada ya kocha Amorim kuelezea maumivu yake hayakuwa siriazi sana, lakini mambo ni tofauti.

“Sesko ataendelea kuwa nje kwa muda,” alisema Amorim.

“Itachukua muda na tunampatia matibabu ya kutosha. Harry (Maguire), ni hivyo pia. Nilimtarajia Matheus kwenye mechi ijayo (West Ham, Alhamisi), si kwenye hii mechi.”

Kocha wa kati, Maguire hakucheza pia dhidi ya Everton kutokana na kusumbuliwa na misuli na Cunha aliumia mazoezini.

Man United ilicheza mechi tano bila ya kupoteza kwenye Ligi Kuu England kabla ya Kieran Dewsbury-Hall kuifungia bao pekee Everton, Jumatatu iliyopita, huku kikosi cha Amorim, kilipiga mashuti 25 na kumiliki mpira kwa asilimia 69 bila ya kufunga bao uwanjani Old Trafford.