Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

El Clasico: Barca ikitafuta ubingwa, Madrid ikipanga kuvuruga sherehe Camp Nou

Muktasari:

  • Kinachofahamika ni kwamba, huenda vikosi vya timu hizo vikawakosa baadhi ya mastaa, upande wa Real Madrid akithibitika kuukosa mchezo Federico Valverde aliyeumia katika tukio la ugomvi baina yake na kiungo mwenzake, Aurelien Tchouameni katikati ya wiki hii kwenye chumba cha kubadilishia nguo klabuni kwao, huku supastaa wa Barcelona, Lamine Yamal akikosekana kutokana na kuwa majeruhi.

BARCELONA, HISPANIA: MAMBO ni moto! Wakati Barcelona wanapojiandaa kuwakaribisha Real Madrid katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania (LaLiga) unaotarajiwa kupigwa leo, Jumapili, kuanzia saa 4:00 usiku, kuna vitu vya kufurahisha kuelekea mchezo huo wa Dabi ya Hispania (El Clasico) ambavyo kwa mashabiki huenda vikawaacha na maswali kibao.

Kinachofahamika ni kwamba, huenda vikosi vya timu hizo vikawakosa baadhi ya mastaa, upande wa Real Madrid akithibitika kuukosa mchezo Federico Valverde aliyeumia katika tukio la ugomvi baina yake na kiungo mwenzake, Aurelien Tchouameni katikati ya wiki hii kwenye chumba cha kubadilishia nguo klabuni kwao, huku supastaa wa Barcelona, Lamine Yamal akikosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Lakini, wakati hali ikiwa hivyo, Barcelona wanahitaji sare tu ili kutangazwa mabingwa wapya wa Hispania huku Real Madrid wakijipanga kuchelewesha ubingwa huo iwapo watawafunga wapinzani wao hao, na kompyuta ya utabiri ya Opta inaipa Barcelona inayoongoza La Liga nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo kwa asilimia 49.8, huku Real Madrid ikipewa asilimia 27.2 na uwezekano wa asilimia 23 wa sare.

Iwapo Barca, ambao wanaongoza La Liga kwa tofauti ya pointi 11 huku zikiwa zimebaki mechi nne wataepuka kufungwa, basi watatwaa ubingwa. Huko nyuma kumekuwapo na tukio moja ambapo ubingwa wa La Liga uliamuliwa moja kwa moja kupitia matokeo ya El Clasico. Hata hivyo, Real Madrid wameshinda mechi nane kati ya 12 zilizopita za La Liga dhidi ya Barcelona.

Ikipoteza linaweza kuwa tukio baya zaidi kwa Real Madrid dhidi ya wapinzani wao wakubwa kuwakabidhi ubingwa. Lakini hiyo ndiyo hali inayoikabili Real Madrid, Jumapili hii, inapokwenda Camp Nou kuivaa Barcelona.

Kwa kocha wa Barcelona kubeba ubingwa atakuwa ameshinda katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Blaugrana, na kuwa kocha wa nne kufanya hivyo katika karne ya 21 baada ya Pep Guardiola, Luis Enrique na Ernesto Valverde.

Ingawa sare inatosha kwa Barca, Blaugrana watataka kutwaa ubingwa kwa staili ya aina yake mbele ya mpinzani mkubwa - tena mtani wa jadi. Baada ya ushindi wa mabao 4-3 msimu uliopita, Flick anaweza kuwa kocha wa pili wa Barca kushinda mechi zake mbili za kwanza za nyumbani za La Liga dhidi ya Real Madrid katika karne ya 21 baada ya Guardiola ambaye alishinda tatu za kwanza.

Barca pia wako kwenye kiwango bora wakiwa wameshinda mechi 10 zilizopita za La Liga, ikiwa ni mfululizo bora chini ya Flick. Makocha wanne pekee katika historia ya klabu hiyo wamewahi kufikisha ushindi mara 11 mfululizo wa ligi ambao ni Guardiola (16), Frank Rijkaard (14), Luis Enrique (12) na Tito Vilanova (11). Blaugrana pia wamefunga mabao katika michezo 54 mfululizo La Liga tangu walipofungwa bao 1-0 na Leganes Desemba 2024, ikiwa ndiyo rekodi ndefu zaidi inayoendelea katika ligi tano bora za Ulaya.

Tangu tarehe ya El Clasico ya pili ya msimu ilipopangwa, ilionekana wazi inaweza kuamua ubingwa, ingawa huenda hakuna aliyedhani tofauti ya viwango kati ya vigogo hao wa soka la Hispania ingekuwa kubwa kiasi hiki msimu huu. Hata kama Barca watateleza, bado utahitajika muujiza mkubwa kwa Los Blancos kubadili hali na kutwaa ubingwa na huenda ikiwa hivyo itakuwa 'comeback' ya aina yake.

Real Madrid wamepoteza mechi mbili kati ya tano za mwisho za ugenini La Liga (ushindi mara mbili, sare moja), idadi sawa ya vipigo walivyopata katika mechi 17 zilizopita za ugenini kwenye mashindano hayo (ushindi 12, sare tatu, vipigo viwili), na kompyuta ya Opta haiwapi nafasi kubwa ya kubeba ubingwa, ikiwapa asilimia 0.08.

Ni mara moja tu katika historia ambapo ubingwa wa La Liga uliamuliwa moja kwa moja kupitia matokeo ya El Clasico. Hilo lilitokea msimu wa 1931-32, ambapo Real Madrid chini ya kocha raia wa Hungary, Lippo Hertzka walipata sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa mwisho wa msimu na kuwazidi Athletic Club kutwaa ubingwa.

Bila shaka, kumekuwa na mifano mingi ya wapinzani hawa kukutana katika fainali huku mataji yakiwa mezani. Ukijumlisha mechi za mikondo miwili kumekuwa na matukio 28 kama hayo katika Copa del Rey (mara nane), Copa de la Liga (mara mbili) ambayo ilichezwa kwa miaka minne katika miaka ya 1980, na Supercopa de Espana (mara 18). Real Madrid wametwaa mataji 11 kutoka katika mechi hizo huku Barca wakitwaa tisa.

Na ingawa Madrid watakuwa na hamu ya kuchelewesha sherehe za Barca, ukweli unabaki kuwa huu umekuwa msimu mgumu kwa Los Blancos ambao watamaliza bila taji lolote.

Kocha Alvaro Arbeloa atasimamia El Clasico yake ya kwanza na ni makocha wanne pekee wa Real Madrid wameanza kwa ushindi katika mchezo huo ugenini dhidi ya Barcelona ambao ni Jose Quirante 1929 (1-2), Carlos Queiroz 2003 (1-2), Bernd Schuster 2007 (0-1) na Zinedine Zidane 2016 (1-2). Arbeloa huenda anaelekea kwenye mechi zake za mwisho kama kocha wa Madrid huku Mourinho akitajwa kuwa chaguo la Florentino Perez, hivyo kuivuruga Barca inaweza kuwa nafasi yake bora ya kubaki kazini.

Kutokana na Kylian Mbappe kuwa shakani kucheza kutokana na majeraha huku kukiwa na mgogoro kati yake na viongozi wa klabu, Arbeloa anaweza kumtegemea Vinicius Junior ambaye amefunga mabao manane katika mechi 23 dhidi ya Barca kwenye mashindano yote. Ni dhidi ya Valencia na Osasuna pekee (mabao tisa) ambapo Mbrazili huyo amefunga zaidi.

Upande mwingine, Robert Lewandowski yupo kwenye kiwango bora akiwa amehusika kwenye bao katika kila mechi tatu zake zilizopita za La Liga (mabao mawili, asisti moja) na anaweza kuhusika kwenye bao katika mechi nne mfululizo au zaidi kwa mara ya nane kwenye mashindano hayo.

Lewandowski hatakuwa na msaada wa mfungaji bora wa Barcelona, Yamal ambaye amefunga mabao 16 La Liga na kutoa asisti 11 msimu huu, lakini Ferran Torres ambaye alifunga bao la ushindi dhidi ya Osasuna wiki iliyopita amechangia mabao 15 ya ligi huku Marcus Rashford akiwa na mchango wa mabao 14 La Liga. Raphinha ambaye hakutumika dhidi ya Osasuna alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Real Madrid kwenye Supercopa mapema msimu huu.


BARCELONA VS REAL MADRID

Real Madrid wameshinda mechi nane kati ya 12 za mwisho za La Liga dhidi ya Barca (vipigo vinne), idadi sawa ya ushindi waliopata katika El Clásico 32 zilizotangulia kwenye mashindano hayo (ushindi mara nane, sare saba, vipigo 17).

Hiyo inajumuisha ushindi wa mabao 2-1 wa Los Blancos katika mchezo wa kwanza msimu huu, ambapo Mbappe na Jude Bellingham walifunga mabao. Hakuna kati ya mechi 12 zilizopita za La Liga kati ya Real Madrid (ushindi mara nane) na Barca (mara nne) uliomalizika kwa sare, ikiwa ndiyo mfululizo mrefu zaidi bila sare katika El Clásico ya ligi tangu michezo 18 kati ya 1977 na 1986 (ushindi mara 10 kwa Real Madrid na mara nane Barcelona).

Nyumbani, Barcelona wameshinda mechi mbili kati ya tatu za mwisho za La Liga dhidi ya Real Madrid (kipigo kimoja), mara mbili ya ushindi waliopata katika mechi saba zilizotangulia nyumbani dhidi yao kwenye mashindano hayo (ushindi mmoja, sare tatu, vipigo vitatu).

VIKOSI VINAVYOTARAJIWA

BARCELONA: Joan García, Eric Garcia, Pau Cubarsi, Gerard Martin, Joao Cancelo, Pedri, Gavi, Roony Bardghji, Dani Olmo, Fermin Lopez, Robert Lewandowski.

Kocha mkuu: Hansi Flick


RELA MADRID: Andriy Lunin, Trent Alexander-Arnold, Antonio Rudiger, Dean Huijsen, Alvaro Carreras, Franco Mastantunonto, Thiago Pitarch, Aurelien Tchouameni, Vinicius Junior, Jude Bellingham, Brahim Diaz.

Kocha mkuu: Alvaro Arbeloa