Scaloni: Sina uamuzi wa mwisho, kila kitu Messi
Muktasari:
- Katika mahojiano na gazeti la Ole kabla ya mchezo wa ufunguzi, kocha wa Argentina, Lionel Scaloni alizungumza kuhusu nafasi na umuhimu wa nahodha wake, Lionel Messi, ndani ya kikosi hicho.
MIAMI, MAREKANI: TIMU ya taifa ya Argentina inajiandaa kutetea taji lake la mabingwa wa dunia zikiwa zimebaki siku sita kabla ya Kombe la Dunia kuanza nchini Mexico, Marekani na Canada, huku wakiwa na matarajio makubwa ya kufanya hivyo.
Katika mahojiano na gazeti la Ole kabla ya mchezo wa ufunguzi, kocha wa Argentina, Lionel Scaloni alizungumza kuhusu nafasi na umuhimu wa nahodha wake, Lionel Messi, ndani ya kikosi hicho.
Scaloni pia alielezea changamoto ya kuiongoza timu ya taifa yenye hadhi kama Argentina katika Kombe la Dunia.
“Hakuna anayependa kutolewa uwanjani, hata Messi,” alikiri kocha huyo.
Kauli yake iliyovutia zaidi ni pale alipodokeza jinsi Messi anavyohusika katika uamuzi ya timu.
“Sifanyi uamuzi wowote bila kushauriana na Messi. Scaloni anaamini ni jambo la kawaida kwa sababu Messi si mchezaji wa kawaida ndani ya kikosi hicho.
“Hakuna maana ya kusema kwamba mimi ndiye mwenye mamlaka yote. Sisi huzungumza na Messi kuhusu uamuzi wote tunayofanya. Aliendelea kusema:”Namwuliza anafikiria nini, anaendeleaje, na tunajaribu kufikia makubaliano.”
Licha ya Messi kuwa na umri wa miaka 38, Scaloni anaamini bado ana mchango mkubwa kwa Argentina.
“Nadhani inapaswa kuwa hivyo, kwa sababu hata akiwa uwanjani na anakutana na ugumu, bado anatupatia mambo mengi.”
Kocha huyo alisisitiza kuwa uwepo wa Messi pekee unaweza kubadilisha mchezo. “Ni bora kuwa naye uwanjani. Ana uwezo wa kutengeneza nafasi na kuunda hatari nyingi.”
‘NGOMA YA MWISHO’
Kombe la Dunia la mwaka huu linaonekana kuwa mashindano ya kuaga kwa baadhi ya magwiji wakubwa wa soka.
Messi na Cristiano Ronaldo wanatarajiwa kushiriki Kombe la Dunia lao la sita, jambo ambalo linaweza kuwa mara yao ya mwisho kucheza katika jukwaa hilo.