Sumu kuvu ni hatari kwa afya, uchumi

Muktasari:
- Kutokana na uhama-sishaji unaotolewa na wadau wa afya, kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kupen-da kula ugali wa nafaka. Waandaaji wa nafaka hizi wana-paswa kuwa makini wakati wa usagaji ili kuondoa uwezekano wa kuwamo kwa fangasi wa sumuku-vu.
Utunzaji salama wa nafaka baada ya mavuno ni muhimu kwa usala-ma wa chakula kwani hupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya bakteria au fangasi wanaosababisha magonjwa tofauti ikiwamo sumukuvu.
Sumukuvu ni aina ya sumu inayoten-genezwa na kuvu au fangasi wanaoota kwenye mazao mbalimbali hasa nafaka kama vile mahindi, mtama, ngano, mchele na ulezi. Kuvu hao wanapoota huonekana kama ukungu. Mahindi ndiyo nafaka inayo-shambuliwa zaidi na uchafuzi wa sumuku-vu ikilinganishwa na nafaka nyingine.
Mazao mengine yanayoweza kusham-buliwa na fangasi hawa licha ya nafaka ni pamoja mbegu za mafuta mfano kara-nga, pamba, alizeti na korosho; makopa au mihogo mikavu, viungo vya chakula mfanov iliki na mdalasini; mboga za maja-ni na matunda yaliyokaushwa. Wanyama wanaokula sukumuvu huwa na uwezekano wa kuathiri mazao yao mfano maziwa au nyama.
Uchafuzi wa sumukuvu kwenye nafaka huweza kutokea kabla na baada ya mavu-no na haiwezi kuondolewa kwa njia za kawaida kwa kupika kwa muda mrefu.
Yapo madhara ya kiafya ya kula chaku-la kilichochafuliwa ambayo ni pamoja na kifo kwa mlaji wa chakula hicho. Kwa kawaida athari hutegemea kiwango cha sumu katika chakula kilicholiwa, muda uliopita tangu kitumike, umri na afya ya mlaji kwa ujumla.
Agosti, watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha mkoani Dodoma baada ya kula chakula kinachoaminika kilikuwa na maambukizi ya sumukuvu huku wen-gine wakilazwa.Madhara ya muda mfupi ni pamoja na maumivu ya tumbo, kutapika, homa, dege-dege, kutokwa damu nyingi, manjano ya macho na sehemu za mwili mfano viganja. Mtu akionesha dalili hizi apelekwe kituo cha afya kilichopo karibu haraka.
Kwa muda mrefu, sumukuvu yaweza kusababisha saratani ya ini, figo na koo, kuathiri mfumo wa kinga ya mwili na uzazi, kuathiri ukuaji wa watoto hasa wenye umri chini ya miaka mitano.
Madhara kwa uchumi
Watu wanapougua kutokana na maambukizi ya sumukuvu husababisha kudorora kwa shughuli za uzalishaji mali. Mzigo wa gharama za matibabu pia huathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.
Aidha, biashara ya mazao nje ya nchi ambayo ni muhimu katika kukuza Pato la Taifa huweza kupoteza soko endapo itafahamika kuwa yana kiwango kikubwa cha sumukuvu. Mfano mzuri ni hasara ambayo Tanzania iliipata mwaka 2008 baada ya kuuza tani 15,000 za karanga kwa Dola 424 za Marekani kwa tani na kubainika zilikuwa na uchafu mkubwa wa sumukuvu aina ya aflatoxin.
Bei hiyo ilikuwa ndogo kutokana na kasoro hiyo ikilinganishwa na mapato ambayo nchini nyingine ziliyapata. Afrika Kusini kwa mfano, mwaka huo iliuza karanga zake kwa Dola 1,473 kwa tani. Hii ni kwasababu hazikuwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu ambacho kingeweza kuhatarisha afya ya walaji.
Ushauri wa maofisa ugani ni muhimu na wakulima wanapaswa kuupa kipaumbele kuhakikisha mazao yanalimwa na kutunzwa kwa kufuata viwango vya kimataifa ili kuepuka hasara kama hii iliyojitokeza takriban muongo mmoja uliopita.
Kudhibiti sumukuvu
Zipo njia nyingi za kukabiliana na sumukuvu kuenea na kuathiri mazao. Nyingi ya namna hizi hufanywa baada ya mavuno ya nafaka husika. Kuhakikisha mahindi au nafaka zimekauka vizuri kabla ya kuzihifadhi ni moja ya kati ya njia hizo.
Kabla ya kuzihifadhi, inashauriwa kuzichambua nafaka husika ili kuondoa uchafu na kuzitenga zile hafifu, zilizopasuka na zilizoshambuliwa na wadudu. Lakini mkulima anaweza akaepuka kuanika mahindi au nafaka nyingine yoyote kwenye udongo. Wataalamu wanashauri kutumia kichanja, mkeka, turubai au sakafu safi ambayo haina unyevu wa aina yoyote.
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa hata wakati wa kwa kuzingatia mambo masuala kadhaa muhimu kwa usalama wa chakula. Eneo la kuhifadhi linapaswa kuwa safi na lenye mzunguko mzuri wa hewa wakati wote.
Jambo jingine muhimu ni kuepuka kuchanganya nafaka za zamani na zile mpya. Haishauriwi kuchanganya mazao kutoka mavuno ya misimu tofauti kwa usalama wa chakula husika. Hii inasaidia kutosambaza maambukizi, kama yako kwenye moja ya mavuno hayo.
Uhifadhi nao ni muhimu kuangaliwa kwa umakini. Wataalamu wanapendekeza nafaka zilizotayari zitunzwe kwenye magunia mapya na yapangwe mahali palipoinuka na siyo sakafuni.
Dawa za kunyunyiza ili kuziongezea maisha nafaka ulizonazo ni muhimu pia. Ikiwa unategemea kuzihifadhi kwa zaidi ya miezi mitatu, unashauriwa kupata ushauri toka kwa mtaalamu wa kilimo waliopo kwenye eneo lako kuhusu dawa nzuri ya kuhifadhia na namna ya kuitumia. Umadhubuti wa ghala au chumba cha kuhifadhia nafaka ni jambo jingine la kipaumbele wakati wa utunzaji ili kuepuka maambukizi ya sumukuvu. Chumba au ghala hilo linapaswa kuezekwa vizuri kiasi cha kuondoa uwezekano wa nafaka kuloa.
Tahadhari dona
Kutokana na uhamasishaji unaotolewa na wadau wa afya, kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kupenda kula ugali wa nafaka zisizokobolewa au dona. Waandaaji wa nafaka hizi wanapaswa kuwa makini wakati wa usagaji ili kuondoa uwezekano wa kuwamo kwa fangasi wa sumukuvu. Yapo mambo kadhaa muhimu kuyatambua. Kuchambua na kuzipepeta nafaka ili kuondoa uchafu na nafaka zilizoshambuliwa na wadudu ni miongoni mwa namna hizo.
Hatua nyingine ni kuosha mahindi au nafaka yoyote unayotaka kuisaga na kuianika mpaka ikauke vizuri. Hii husaidia kuhakikisha vijidudu vyote vimeondolewa kabla ya kusaga.
Ipo haja ya kuanika nafaka ulizonazo juu ya kichanja, mkeka au turubai ili kuzuia uchafuzi wa fangasi waliopo ardhini endapo utazinika chini. Hata baada ya kusaga unga uhifadhiwe kwenye chombo kisafi, kikavu na kisochoruhusu unyevunyevu kupenya. Ikiwezekana chombo chenye unga kiwekwe sehemu isiyo na unyevunyevu.
Hata hivyo, taarifa za kisayansi zinaonyesha kukoboa nafaka kunapunguza uchafuzi wa sumukuvu kwa kiasi kikubwa hivyo kushauri ulaji wa dona kwa ajili ya afya imara. Kwa kuwa mahindi na nafaka kwa ujumla ni chakula kikuu cha wananchi walio wengi nchini ni vema wadau wote kwenye mnyororo thamani wa chakula wakazingatia kanuni za afya kuepuka sumukuvu.
Kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo, kuanzia uhifadhi, usambazaji na usindikaji wa mahindi na bidhaa zake kutapunguza madhara yanayoweza kuikumba jamii kwa kula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu hivyo kuongeza uhakika wa maisha salama.