Tunatamani kuwapenda wake zetu lakini tatizo lipo hapa
Kufua, kuosha vyombo, kupika, kusafisha nyumba, kunyoosha nguo hizo ni kazi za kina mama. Halafu unadhani tunaoamini hivyo ni sisi wanaume tu? Wala, mbona mpaka hao wanawake wenyewe wanaamini hivyo.