Mbrazili Simba anataka mabao 15 msimu huu

Friday September 27 2019

 

By THOBIAS SEBASTIAN

STRAIKA Mbrazili wa Simba, Wilker  Da  Silva, amecheza mchezo wa kwanza wa kimashindano jana Alhamisi dhidi ya Kagera Sugar.
Wilker ambaye aliingia dakika za mwishoni kwenye mechi hiyo ya ligi kuu iliyochezwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, alikuwa majeruhi aliyopata tangu timu hiyo ikiwa kambini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.
Da Silva alisema huo ni mwanzo kwake kupata nafasi ya kucheza ingawa kwa dakika chache lakini ana malengo yake ya kuhakikisha anafunga mabao 15 msimu huu.
"Kama mshambuliaji natamani kumaliza msimu nisiwe chini ya mabao 15, kama nikifanikiwa hili itakuwa furaha kubwa kwangu kutimiza malengo lakini nikishindwa itakuwa chachu kwangu kupambana ili niyafikie msimu ujao,"
"Kadri muda ambavyo unazidi kwenda naamini nitapata nafasi ya kucheza na kulitimiza hilo kwani si rahisi kutoka majeruhi na kuanza kwa kucheza kiwango cha juu moja moja," alisema Da Silva.

Advertisement